TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hivi ninyi watanzania ni nani kawapumbaza kiasi hiki!? Wewe unaona hao wahanga walichokifanya walihatarisha usalama wa nchi!? Wahanga hawa wengi wamekuwa ni wahanga wa watu binafsi na cyo nchi... Mfano tu huwezi kusema Shilawadu wangeweza kuhatarisha usalama wa nchi hadi ipelekee wao kuvamiwa. Au Roma Mkatoliki unasema nae alihatarishaje usalama wa nchi!?

Je, kusema na kuikosoa serikali ni kuhatarisha usalama wa nchi au ni kuiokoa nchi isitumbukie kusiko?

Usalama wa Taifa kama wana uwezo huo wa kufanya watu wawe vilema au kupotea kabisa kwanini wasingewafanyia hayo mafisadi? Walishindwa nini kuhakikisha viwanda vyetu, ndege zetu, fedha zetu hazipigwi na wachache!? Katika Biblia kuna kisa cha mtu mmoja aliyekuwa ametundikwa msalabani pamoja na Yesu Kristo, badala ajitetee akawa anamdhihaki Yesu. Hata sisi watanzania tuna kasoro kubwa sana ya kujikomba na ndo maana nchi imeendelea kuwa masikini na watu wake
 
Duh Paskali umenikumbusha State Research Bureau (SRB) ya Uganda enzi za Idd Amin! Mungu atuepushe na madhila kama hayo!
 
TISS ni taasisi exceptional eti ikanushe! Unategemea tiss waanze kuitisha vipress conference na kuanza kukanusha upuuzi wa mitandaoni? Yaani muanze kuwajadili mpk elimu zao humu!!!!

Point of correction makirikiri hawajavamia clouds bali waliingia na silaha. Sifa za kuvamia hazipo kwenye tukio lile.
 
Hivi Upelelezi wa Lissu kupigwa Risasi za kutosha umefikia wapi?
 
"TISS inatakiwa kubadilika na kuunda kitengo madhubuti cha ujasusi wa kiuchumi, mfano, tuna Balozi zetu katika nchi zote zinazochenjua Mchanga wa makinikia, TISS wangekuwa wa maana, by now tungeisha jua hao Acacia wanapata nini kwenye Mchanga wetu, gharama za uchenjuaji container la Mchanga ni kiasi gani na kila kinachopatikana!, lakini wao wamekalia kudukua tuu simu, badala ya kudeal na serious issues za kiuchumi!. Kiukweli ile bili ya trilioni 190 ya TRA sio realistic, rais wetu ataonekana mjinga, Waziri Kabudi ataonekana mjinga, na nchi nzima tutaonekana ni taifa la wajinga, wakati ukweli utakapobainika, kitu ambacho TISS makini ingeweza kuzuia"

Hapa hutawaona, wako bize kudukua simu na favce book
 
Sioni ni wapi watanzania wamepumbaa. Kama kutoa maoni yenye kukinzana na ya mtu mwingine ni upumbavu, basi mwenye kuona hivyo ndiye mpumbavu!
Kuna kukosoa au kutukana au kukashifu. Unapotukana au kukashifu, je, huoni kama huwa unajihatarishia maisha mwenyewe kutoka kwa unayemtukana au kumkashifu? Unatarajia reaction gani kutoka kwa unayemtukana? Akiwa muungwana, atakubeza au kumuachia Mungu. Akiwa mbabe au mfitini, utakiona cha mtema kuni! Akiwa mpole, atakupeleka kwenye vyombo vya sheria au kukusamehe!
Aidha ukiwa mhanga wa kuhatarisha usalama wa watu binafsi wenye nchi, ni dhahiri unahatarisha usalama wa nchi! Anzia hapo!
 

We we ni zaidi ya mwandishi. Uko well informed.
 
Uhayawani huu....Paskali umekuwa mtu wa hovyo kabsa!!
 
Shida anaewalipa anapenda majungu, ndio maana usiku na mchana kazi ni kudukua watu hili apate umbea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…