TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!


Umesema TISS wanapaswa kuwa wasafi kama mke wa Kaisari, wakituhumiwa, wanahukumiwa.

Baadae unasema wakikaa kimya ni sawa na admission of guilt, wajitathmini, wajitokeze, wakane tuhuma, wajisafishe, warudishe imani ya public kwa taasisi yao. Yani kumbe tuhuma zinakanushika, zinasafishika.

Hivi mnapokuwa mnaandika term papers za shahada ya kwanza, au thesis za uzamili, au dissertation za uzamivu, wakufunzi wenu hawawaambii kijana hebu pitia tena hapa na pale na pale unyooshe logical disasters zilizomo ili ujifunze logic ndugu???

Eti watu wanadhani TISS inaajiri malaika lakini na wenyewe ni binadamu, wanakosea. Nani anadhani, sisi au WEWE ULIYESEMA TISS NI MKE WA KAISARI ???

Unachoandika aya ya pili, Paskalli, hakitakiwi kupingana ki- logic na aya ya 18. Tujifunze ku think na kuandika logically!
 
paskali wewe una vitu vingi sana tunapaswa kuvijua kupitia wewe. Thanks kwa habari na Somo pia
 
Mkuu Paskali naona ulijitoa kinaga ubaga ili kuweka mezaji hoja ya TISS achilia mbali kutupa story za Mzee Andrea (RIP) na mama pia.

So far, baada ya bandiko lako na hoja ya Bashe kuitaka Kamati ya Bunge chini ya DCI Mstaafu Balozi Adadi, nadhani suala hili lili-ishia chini ya carpet. Nadhani wakubwa walitumia busara ya kutomwaga mchele kwenye kuku wengi.

Paskali umetoa link ya mtu anajinasibu kama jasusi alie-deffect na sasa yuko uskochi. Kwa maelezo yake, Idara hizi huajiri intelligent people to do intelligence works.

Sina ushahidi kwenye sector zingine idara inafanya nini, ila kwenye kujenga uchumi endelevu wa mama Tanzania ni either hakuna unit mahsusi kwa ajili ya kukuza uchumi au sijui nisemeje.

Siku kadhaa zimepita, nimeona correspondence ya mtu mmoja na supplier wa aina fulani ya machine za kuchakata mazao ya kilimo. Imeshangaza kuona Rwanda imetoa dhamana ya USD 5mil kujenga kiwanda cha kuchakata tani laki 200 kwa siku. Kwa quick survey tuliyofanya na mhusika ni kuwa Rwanda hana capacity ya kuzalisha raw material, ila anategemea Tanzania ilime then yeye ananunua kwa bei poa, anachakata kwa soko la ndani na ku-export.

Sijawahi kumsikia Waziri wa Fedha au Viwanda wakiwa wana-spearhead uwekezaji wa kimkakati hata kwe agro-processing ambako tunaweza kuuza lots of tons ya finished products na kuingiza forez za kutosha. Jamani, kama masuala ya kijasusi ya mambo mengine yanafanywa, iko haja tukae, tujadiliane; na kama huwa wanajadili basi reports za BoT zinatuumbua kwa kutokuonesha utekelezaji. Kwani taarifa ya hivi karibuni unaonesha -ve kwenye export kwenda Kenya na exports zetu na mahindi, maharage.

Lini Bandari yetu aitakuwa busy ku-export processed products kupitia bahari hindi ili kuingiza forex. Usalama bila shaka wanafanya vyema, ila Key Performance Indicator kwenye kujenga uchumi endelevu na jumuishi....labda mimi sioni sawia. Na naomba kuoneshwa au basi tuoneshane namna gani ya kuhakikisha wengi wanafika nchi ya ahadi
 
Wakati mwingine afisa mmoja au baadhi ya maafisa wanaichafua idara (TISS) sababu tu hawana madili na walipata bahati ya kuwa maafisa. Ila mimi ninavyojua kati ya idara ambayo haipendi dhuluma kwa wananchi ni hii idara. Pengine kama ulivyosema watu wanafanya operations zao tu kama kikundi flan lakini wanaichafua idara . lakini ni kwa sababu ajira ndani ya idara zimekuwa za
Maadili ndani ya idara yamepungua sana. Baadhi ya maafisa wasio na maadili wanaichafua idara(TISS) hii ni kwa sababu vijana wanachomekwa kwa kujuana sio kama kwa kupimwa uwezo na uadilifu. Lakini kusema kwamba torture ni mbinu ya upelezi sio kweli. Wenzetu huko US wameendelea zipo mashine zinatumika kumhoji mtuhumiwa na kama anadanganya inatambua. Pia hata kutesana walishasahau.
 
Kwani kipindi hicho ulikuwa bado hujaitwa pale mjengoni kwa Ndugaye?
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Inawezekana viongozi wa juu hawajui yanauoendelea. Rafikiyangu shemeji yake alikuwa anasumbuliwa na matibabu nikauliza vipi akasema huyo kijana anafanya TISS na kapigwa risasi huko Musoma au Mwanza wakati wakijaribu kwenda kwa mfanyabiashara usiku bila kuwa na kibali. Mfanyabiashara huyu alifikiri ni wezi kibaya zaidi walikuwa hawajui kama na yeye ana bunduki wakanza kufetuliana na jamaa akapigwa risasi mbili amekuwa kama kilema na hakuna kesi maana hawakuwa wameenda kiutaratibu. Yaani familia ya huyo mdogo wake inashida sana sasa wana baba kilema. Hii ni ya ukweli kabisa nilikuwa nasikia tu lakini kumbe ni kweli
 
EEeh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…