TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Kaka Pascal Umenitisha sana mzee wa kitengo pale Saint Peters.
Mkuu Phillipo Bukililo, mtu wa kitengo, angeweza kuleta bandiko kama hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Au hili Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya? kwanini nilete humu nisipeleke ofisini?.

Mkuu wa TISS ni CinC, ningekuwa kule, baada ya kuona maisha ya CinC yako hatarini, kwanini nisiripoti kitengo, na badala yake nikaja kuripoti humu?, US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? mwisho wa siku you know what happened!, kwanini sikusaidia?.

Kinachofanya watu humu kunidhania, ni kufuatia wazazi wangu wote wawili, baba na mama both ni watu wa huko, hivyo watu kudhani mwana wa nyoka ni nyoka!, sisi tumezaliwa 8!, kama watoto wote wa kitengo wanaajiriwa kitengo, hicho kitengo kina watu wangapi?. Kati ya sisi 8, mwenye watoto wachache ni 6!, mimi ninao 10 wa home!, hicho kitengo kitakuwa na watu wangapi?.

P
 
We ni mtu wa system kitambo sana
Duh...!. Wakuu kimsboy na Mr. Bigman , mimi ni verified member hapa JF, kama ni mtu wa huko, inamaana bandiko kama hili nimelileta humu kufanya nini?.

Issues kama hizi si zingekuwa ni issues za kumaliza ofisini, zimekujaje jf?, au kwa vile wale jamaa zetu wanapenyezwa kila mahali, hivyo mimi ndio ofisa wao ninayefanyia JF, hivyo mabandiko kama haya ni ya kuzuga tuu?. Na lile swali la siku ile pale mahali pia niĺikuwa kazini nikamzuga boss wangu?. Hivyo hata kile kiofisi changu cha PPR nacho pia ni cha kuzugia?.

Basi hii system ya enzi hii kiboko!.
P
 
Kuna watu huwa wanadhani hawa jamaa ni malaika, hawewezi kuboronga, kiukweli kabisa hawa jamaa nao pia ni binadamu na wanaweza kuboronga na kuondolewa ila kwa heshima!, inaonyesha Kipilimba aliboronga!, akaondolewa akatupwa ubalozini. Huyu naye kaboronga, baada ya kuboroga kule, akapelekwa Ikulu, that was a mistake!. Thanks God Mama kurekebisha makosa kabla jamaa hajaripoti!. Huyu apelelekwe tuu ubalozini!.
P
 
Mkuu Pascal mayalla heshma yako,maoni yako ni yapi ili kuweza kutibu swala zima la uadilifu na kuwajibika kwa viongozi wa umma?
Mkuu Emmanuel Mkwama , hili la uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa umma, niliisha shauri sana humu tangu kitambo mfano mzuri ni mabandiko haya matatu
  1. Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
  2. Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?
  3. TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Ukipata muda tembelea pia ujifunze jinsi awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa very seriously na issues za uadilifu na uwajibikaji.

P
 
TISS haikanushi au kukubali kitu chochote .
Hata wakati ule Mbowe alipotenguka mguu Dodoma akasema,"Watu wabaya hawa,walitaka nisishiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,",TISS haikukanusha,ingawa wakati ule Mbowe na Lema na Msigwa waliwatuhumu watu waovu. Ha ha ha .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…