TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Wanabodi

Declaration of Interest
Tunapojadili jambo nyeti kama hili, ni vizuri ku declare interest ili kwanza kujenga imani kwenu wasomaji wangu kuwa mwandishi wa makala hii ni mtu wa kuaminika, hizi data kwenye bandiko hili ni data za kuaminika authentic, bonafide genuine from trusted sources na sio data za kuokoteza, data za kubuni, kuzua, au kuunga unga, hivyo ni vyema mimi nikajitambulisha kidogo kwenu, pia kwa sababu mtu unapotoa data nyeti from time to time katika mabandiko yako, huchelewi kunyooshewa kidole kuwa huyu jamaa ni TISS, hivyo na mimi kudhaniwa ni TISS, hivyo bandiko kama hili, litawafungua macho wengi humu kuwa huyu mtoa mada atakuwa ni TISS wa ajabu sana kuilaumu ofisi yake mitandaoni!.

Mimi Pascal Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo wa kuandika Investigative Stories, (IJ), ila pia nimepata bahati ya kuzaliwa na kukulia katika familia ya TISS kwa wazazi wangu wote wawili, baba na mama. Baba Mzee Andrew Mayalla (RIP) ameishatangulia mbele ya haki, na mama bado yuko hai, hivyo baadhi ya hoja zangu za kiitelijensia, sio kwasababu mwana wa nyoka ni nyoka, bali mtoto ukizaliwa kwa wazazi wote wawili ni wana inteligensia wa TISS, unazaliwa na natural intelligence ambayo ni tool muhimu sana kuweza kuwa Investigative Journalist.
Kaka Pascal Umenitisha sana mzee wa kitengo pale Saint Peters.
Mkuu Phillipo Bukililo, mtu wa kitengo, angeweza kuleta bandiko kama hili TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Au hili Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya? kwanini nilete humu nisipeleke ofisini?.

Mkuu wa TISS ni CinC, ningekuwa kule, baada ya kuona maisha ya CinC yako hatarini, kwanini nisiripoti kitengo, na badala yake nikaja kuripoti humu?, US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? mwisho wa siku you know what happened!, kwanini sikusaidia?.

Kinachofanya watu humu kunidhania, ni kufuatia wazazi wangu wote wawili, baba na mama both ni watu wa huko, hivyo watu kudhani mwana wa nyoka ni nyoka!, sisi tumezaliwa 8!, kama watoto wote wa kitengo wanaajiriwa kitengo, hicho kitengo kina watu wangapi?. Kati ya sisi 8, mwenye watoto wachache ni 6!, mimi ninao 10 wa home!, hicho kitengo kitakuwa na watu wangapi?.

P
 
Paschal wewe ni TISS tunakujuwa. Wakati mwingine unatumwa humu ndani kuja kmutuchokoza ili kupata our reaction or data ili mkazifanyie Kazi Kijitonyama.Mwisho wa Sikh mna mnakamata na kuteka watu na kuwatesa kisha kuwatupa mabwepande au Ruvu kama sio kubambikwa kesi za uchochezi. Mimi sikuamini kabisa na huwa nakuogopa. Sitaki kujadli chochotge kwenye Uzi huu
We ni mtu wa system kitambo sana
Duh...!. Wakuu kimsboy na Mr. Bigman , mimi ni verified member hapa JF, kama ni mtu wa huko, inamaana bandiko kama hili nimelileta humu kufanya nini?.

Issues kama hizi si zingekuwa ni issues za kumaliza ofisini, zimekujaje jf?, au kwa vile wale jamaa zetu wanapenyezwa kila mahali, hivyo mimi ndio ofisa wao ninayefanyia JF, hivyo mabandiko kama haya ni ya kuzuga tuu?. Na lile swali la siku ile pale mahali pia niĺikuwa kazini nikamzuga boss wangu?. Hivyo hata kile kiofisi changu cha PPR nacho pia ni cha kuzugia?.

Basi hii system ya enzi hii kiboko!.
P
 
Wanabodi

Kuna watu wanadhani Usalama wa Taifa TISS wao ni malaika na hawawezi kabisa kufanya makosa kama madudu haya wanayotuhumiwa nayo sasa. No!, TISS ni kweli kwa vile iko chini ya Ikulu, na Ikulu ni mahali patakatifu, TISS pia inapaswa kuwa ni idara takatifu, lakini kwa vile TISS inaendeshwa na binadamu na sio malaika, TISS inaweza kufanya makosa na uchafu huo ukawa ni kweli ni TISS, ndio maana katika bandiko hili nasisitiza tuhuma hizi dhidi ya TISS kama sii kweli, TISS ikanushe, kama ni kweli, TISS imechafuka na inahitaji kusafishwa!. Hii sii mara ya kwanza kwa TISS kuchafuka, huko nyuma kuliwahi kutokea matukio ya TISS kuchafuka na Ilisafishwa!.
Kuna watu huwa wanadhani hawa jamaa ni malaika, hawewezi kuboronga, kiukweli kabisa hawa jamaa nao pia ni binadamu na wanaweza kuboronga na kuondolewa ila kwa heshima!, inaonyesha Kipilimba aliboronga!, akaondolewa akatupwa ubalozini. Huyu naye kaboronga, baada ya kuboroga kule, akapelekwa Ikulu, that was a mistake!. Thanks God Mama kurekebisha makosa kabla jamaa hajaripoti!. Huyu apelelekwe tuu ubalozini!.
P
 
Mkuu Pascal mayalla heshma yako,maoni yako ni yapi ili kuweza kutibu swala zima la uadilifu na kuwajibika kwa viongozi wa umma?
Mkuu Emmanuel Mkwama , hili la uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa umma, niliisha shauri sana humu tangu kitambo mfano mzuri ni mabandiko haya matatu
  1. Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
  2. Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?
  3. TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Ukipata muda tembelea pia ujifunze jinsi awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa very seriously na issues za uadilifu na uwajibikaji.

P
 
TISS haikanushi au kukubali kitu chochote .
Hata wakati ule Mbowe alipotenguka mguu Dodoma akasema,"Watu wabaya hawa,walitaka nisishiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,",TISS haikukanusha,ingawa wakati ule Mbowe na Lema na Msigwa waliwatuhumu watu waovu. Ha ha ha .
 
Back
Top Bottom