twahil
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 4,100
- 2,795
Hahahaa dah!!! Watu mkishiba amani mnaanza kucheua shibe...Hawa TISS walishapoteza hadhi ya kuitwa Usalama wa Taifa. Taifa letu haliko salama hata chembe na matukio ya hivi karibuni yanathibitisha hivyo. Wanakula tu pesa za walala hoi chungu nzima wakati hawastahili tena kuwepo. Huwezi kusema kuna taasisi ya usalama wa Taifa nchini halafu Watanzania tuishi kwa taharuki kubwa kiasi hiki kila kona ya nchi yetu.
Unazungumza kana kwamba sasahivi nchi hii ni sawa na Somalia au Kongo.
Yani unasema nchi haiko salama hata chembe wakati huo umekaa umerelax kabisa hapo kwako ukiwa unabofyabofya keyboard yako bila hata kusikia kakishindo hata kwa mbaaali ka bomu...
Watanzania hebu tuwe makini na watu wa namna hii....ni hatari sana. Kauli zao sio salama....mie nimeangalia taarifa ya habari sasahivi walau nione kama kuna sehemu ya nchi yetu limepigwa bomu hata moja hakuna sijasikia. Sasa wewe nguchiro unaesema nchi haiko salama hata chembe unamaanisha Tanzania au Somalia?
Ufipa kauli zenu hizi hazitatufanya watanzania tuwaamini kuwapa nchi. Bado hamjastahiri hata kufikiriwa kuwapa nchi muiongoze kwakuwa fikra zeni bado zipo down sana...