TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Kwa maana ya Intelligence, hakuna kumumunya maneno.
Intelligence ni outfit ya intelligent people, watu wenye IQ nzuri tu na wenye kuonyesha si ufaulu turasani bali hata socially acceptable people, si zombies.

Mimi nimesoma nao, so good at their jobs kiasi kwamba ukiambiwa jamaa yuko TISS huwezi amini.
Mwalimu alikuwa akiwa recruit on merits, toka wakiperform vizuri toka madarasani.

Miaka baada ya Mwalimu sijui upepo ulibadilika.
Wenye TISS wakaanza kuingiza ndugu zao, watoto wao, vigezo vimebadilika!
Sasa hivi si nadra kukuta kijana akiwatishia wenziwe kwa ku fkash kadi yake kuonyesha yuko TISS na anaweza kumfanyizia.

TISS outfit lazima ibaki na majukumu yake kikatiba, yaani data collection, dissemination(intelligent), na ku advise uongozi.

Nakubaliana na Pasko, extortion of data, intimidation na hata torture katika ulimwengu wa sasa, utapata data za kuwafurahisha viongozi lakini zaweza kuwa irrelevant and false.

TSS vilevile ikiingia kuchukua corrective measures itaingilia enforcement.
Matukio ya hivi karibuni ya watu wasiojulukana, by all means haiwezi kuwa kazi ya TISS, bali wanasiasa.

Cha kusikitisha ni kwamba Polisi mara nyingi inaboronga mno katika utendaji, hivyo kuathiri intellijensia wanayopata.
Mfano hatari wa hivi karibuni ni Mkuranga/Ikwiriri/Kibiti.

Sidhanii kwamba vyombo husika havikuwa na intellijensia ya yanayoendelea huko.

Tunashukuru kwa joint task force, na seriousness ya uongozi kukabili tatizo lililo anza kuonekana haliwezekani.

Wengi tuna imani kubwa na TISS, lakini vyombo vya enforcement, Polisi, Mahakama, DPP huko kuna ukakasi.

RED:
Napata tabu sana kila mtu analalamika na kila kitu kipo wazi kuanzia uniform zao refer clouds uvamizi, magari yao refer Lissu na kibiti , Wanakopelekwa refer Roma, ben ni kulekule kwenye makazi yao na kila mtu anakujua, utasemajie hawahusiki?

BLUE:
Liko wazi vyombo hisika hawakuwa na hiyo intelejensia na mimi nilishwawahi kuhoji ndugu na jama na marafiki walio huko, kikubwa n fedha hakuna ya kufanya hiyo kazi, uwekezaji mkubw aumewekwa kwqenye intelejensia ya kuwafuatilia wanasiasa badala ya hayo mengine yenye tija.

na ukitaka kujua hawana weledi ni hay ya Maiti kuokotwa coco na kule ruvu. how come chombo chenye uwezo kweli kikafanya matkio kama yale yanayoacha footprint kila kona.
 
Duh!!, umenikumbusha mbali sana kwa habari ya sekeseke la Kigoto, ilikuwa ni zaidi ya gereza la Guantanamo na kibaya zaidi mateso yaliyokuwa yanaendelea hapo enzi hizo yalijulikana hata na watoto wadogo binafsi nimekulia Mwanza (Mabatini) na huyo mzee mhanga mmojawapo marehemu Mazegenuka alikuwa jirani yangu in fact ktk suala la tuhuma za mateso na mauaji ya Kigoto yaliyosimamiwa na maafisa waandamizi wa polisi na Idara ya usalama Mzee Nyerere (RIP) kama head of state alionyesha concern ya kipekee sana ktk kuwatetea raia wake wanyonge dhidi ya udhalimu huo ktk sakata hilo lililokuwa na mvuto wa kipekee karibu nchi nzima enzi hizo, maamazi aliyochukua Mwl. Nyerere dhidi ya watuhumiwa yalimjengea heshima kubwa sana mbele za raia wake na hata taasisi za haki za binadamu kimataifa.

JF raha sana!

“Operesheni Mauaji” 1976 vs "Operesheni Tokomeza" 2013
 
Mkuu Pascal unayo hoja nzito. Kipo kingine kinachojitokeza ambacho ni muhimu kukiangalia kwa umakini mkubwa.

Hii inayoitwa vita ya kiuchumi, ni mpambano mkubwa wa kimaslahi, kushughulika na watu ambao wanauza almasi huko Ulaya na kupata mabilioni ya shilingi halafu leo hii biashara inaingia mchana, kwa kweli hao wafanya biashara wanao uwezo wa kuiharibia nchi heshima yake.

Miaka yote watu wanafaidika na madini yetu halafu leo hii ghafla bin vuup wanakuta mambo yamebadilika, ni lazima wafanye umafia kwa nguvu zote wakiwa na matarajio ya kuibuka washindi.

Nadhani ndio maana hata hao jamaa wa usalama wapo kimya, hawaongei mara kwa mara. Zipo taarifa k
wamba kwenye masuala ya ukachero Tanzania inashika nafasi ya saba duniani. Hivyo pamoja na makosa mengi wanayofanya hao jamaa, bado wanao uhalali wa kuaminiwa kwenye maamuzi na nyendo zao.

Historia hizo, hiyo ilikuwa enzi za mwalimu hasa wakati wa mapambano ya kupigania Uhuru huko kusini mwa janga la sahara.
 
Aiseee hiv intelligence agency za nchi zingine wanafanya kama wanayofanya hawa wa hapa kwetu au ni sisi tu tupo kipekee
 
Si wewe wala Lissu amethibitisha pasipo shaka kwamba wahusika kwenye hayo matukio ni TISS. Kilichopo ni nadharia tu ambazo si sahihi tukazitumia kukichafua chombo nyeti kama TISS. Na hata ingekuwa imethibitika kuwa ni TISS, wao wana procedure zao za kuwajibishana kisheria na si kama Lissu anavyoropoka bungeni. Tuache ujuaji na kuingilia idara zisitokiwa kuingiliwa.

wale wale!
 
Ila umetiririka Ngosha! Kinoma noma..
Yasemwayo...
Twajuwa USA na nchi za mgharibi wanateka na kutesa kichini chini, huku wakikanusha vikali..
Russia na nchi za Ulaya Mashariki, kwa Waaarabu na Asia usiombe, jiue kabla hawajakukamata!
 
Nadhani si vema kuongea kwa mihemuko. Una ushahidi pasipo shaka kwamba TISS ni kikundi cha kigaidi? Una ushahidi pasipo shaka kwamba TISS inahusika na hayo matukio unayoyasema? Ushukuru kwamba Max anahangaika mahakamani kuwatetea watu kama wewe wenye tabia za kuropoka hovyo na kuzichafua idara zetu za ulinzi na usalama kwa maslahi yenu ya kisiasa. Hizi tabia zinanikera mno watu kujitoa ufahamu na kuona siasa ni bora kuliko usalama wa nchi.

yani zina kuuma kuliko hata TISS wenyewe sio?
si ajabu nikisem awewe utakuwa ni mwanasiasa unayefaidika na hayo matendo nitakuw asijakosea.
Ila jiulize mwisho wa haya ni nini?
 
Ila cha kujiuliza ni...hivi kwani Nape, huyo Roma, sijui Bashe na wengineo ambao inasadikiwa kuwa ama walitekwa, waliteswa, au kutishwa na hao TISS, walitendewa hayo ili iweje hasa?

Walitendewa hayo ili kutuma ujumbe kwa wengine na kuwajaza uoga au?

Na ni kweli hayo matendo yanafanywa na TISS au yanafanywa na wengine halafu TISS wanaishia kusingiziwa tu?

Na kama kweli TISS ndo wapo nyuma ya hayo yote, ina maana serikali ya Magufuli haiwezi kukabiliana na wakosoaji wake kwa nguvu za hoja na matokeo ya vitendo vya kazi zake na badala yake inatumia hoja za nguvu?

Halafu kwani hao TISS wao ni watu wa aina gani? Wana mapembe? Hawaishi huku uraiani tuishipo wengine? Ukimtandika mmoja wao ngumi ya kwenye taya hataenda chini kulamba mchanga? Wao wana DNA tofauti na sisi wengine au? Damu yao ni ya kijivu?

F them.....
Watu wa kawaida sana. Tunaishi nao mitaani humu humu. Tena sio mmoja....hata watatu au wanne unaweza kuwapiga ngumi. Ukiwajua hawa watu raha sana. Unaishi kwa amani....nielewe.....watu wa kawaida sana....wengine ni visichana vya kawaida tu.

Kuna mmoja nilikua namlia timing nimtongoze....akaniomba nimsindikize mahali fulani....nikasema yes...fursa si ndio hii....nafika kule kumbe ndio bwanake alikuwa anamsubiri. Kufika pale kanaona aibu kunitambulisha...na mchizi naye akawa haelewi mi nani na kwanini nimekuja na demu wake. Akanigwaya.....nikasepa zangu.
 
Ni ujinga kuamini kuwa eti usalama wa Taifa unateka watu na unaua watu, mbona sisi hatujatekwa, watu wamejaa barabarani, wamejaa mashambani mbona hawajatekwa wala kuuwawa? Mbona hata wewe hujauwa wala kutekwa? Leo hii unaibuka na post ya kijinga jinga. Amajweli post za kunukuu ujinga uliotolewa na mjinga flani tena wa upinzani ambaye yeye ameajiriwa kupinga tu. Jitu lililokataliwa kutokana na ufisadi. Lowasa hatakuwa Rais hata mkilala mnaota.

Asilimia 80 ya Watanzania tupo kama wewe. Akili zetu, uwezo wetu wa kuchanganua mambo, maono na mienendo yetu ipo sawa sawa kabisa; ndio maana hata baada ya miaka 50 ya uhuru hali zetu ndio hizi.
Tupo wengi zaidi yao hao vibaraka, mafisadi na wapinzani wa kila kitu hivyo hawatatushinda. Tupige tu kazi na raisi wetu hatayumbishwa kwa namna yeyote ile!!!
 
Mayalla,

You are avoiding details (seems like purposely) on how the organization became the fist of the ruling party (CCM), thus put
under direct party control. No other oversight existed over it. What existed at the centre "structurally" was the *political police*. Main Tasks included:

1. Suppression and oppression of all kinds of political opposition in the country. A young state had to focus on "Unity and order"...

2. Total control over the society.

No Parliament sitting adopted law/s to determine the activities of the security services, or at least the laws were vague. Basically, the activities of the organization were activities defined and guarded by Revolutionary Party (CCM).

I am in contrary to Zitto et al thinking on dissolving TISS. Dissolving the organization would be disastrous to the Nation because doing so would fulfil the objectives of organized criminals. Many of the would be former intelligence agents would be recruited by numerous mafia groups. They would extend an informal network, support each other, support their ex- bosses, and worse - if united they would be able to easily form even a private army. Let's not forget that we live in a society where informal institutions are stronger than formal ones. Its why we are categorised as a "problematic state", only one level up from being a "failed state". A problematic state is the one that lacks rule of law (instead under a big man rule), and dominated by informal institutions (absence of strong formal institutions).

What needs to be done instead?

-The parliament should adopt relevant laws to guide its activities.

-A parliamentary oversight should be established and it should involve experienced parliamentaries in security matters.

- TISS needs to be depolitized. There should be a ban on party associations for the staff; there should also be prohibition of any political related activity within the working
places of TISS).

- Centralized oversized security apparatus needs to be dismantled.

- There should be a reduction of the number of the staff down to the real needs of the national
security.

- TISS should be put under a more sophisticated controlling system i.e
Parliamentary, administrative and, judicial.

- There's a need of establishing"judicial control" over the use of secret means and methods which can penetrate or infringe the rights and privacy of the citizens.

- Goals and purposes of TISS need to be redirected and restructured
along new directions;

- Recruitment of new intelligence officers should only base onprofessional merits.

- There has to be transparency on its budget sources and also an independent control above them.

- TISS needs to join the intelligence-security community of the "democratic world".

- TISS needs to intensively participation in combating the global security challenges, especially international terrorism.

In the final analysis, CCM and the State should no longer be held in " synonymous ".
Mchambuzi umegonga pale pale...
Kwa kweli sina la kuongeza zaidi ya kupiga makofi na ku-bow..
Tunakubaliana nawe 110%..
 
Mkuu Crabat, naunga mkono hoja. Ila hili la Kanda ya Ziwa, sii kweli, mnamsingizia tuu, na nimelizungumza hapa
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi!
P
ni kweli wasukuma hawana hii tabia ya ukabilia wa maringo. ..tena ni kwa majority hawana tabia hii.
sometimes weakness ya mtu mmoja mkubwa kutojiamini inamfanya aweke ndugu zake karibu kwa fikra labda wata msaidia zaidi na kumlinda lakini sio kweli Watanzania kwa pamoja wakikunga mkono unakua huna waswas
 
ni kweli wasukuma hawana hii tabia ya ukabilia wa maringo. ..tena ni kwa majority hawana tabia hii.
Ni kweli Wasukuma hawana ukabila kabisa, ila wamezungukwa na makabila yenye ukabila. Hivyo akitokea Msukuma mwenye ukabila, ni either amechanganya kabila na majirani zetu, au ni wale waliohamia Usukumani miaka mingi nyuma, wakalowea Usukumani, wakakulia Usukumani, wakasomea Usukumani na kuongea Kisukuma lakini...
P
 
Wanabodi

TISS ni idara nyeti, uadilifu wake unapaswa kuwa wa kiwango cha juu kabisa ambao haupaswi kutiliwa shaka yoyote, unapaswa kuwa ni uadilifu wa kiwango cha mke wa Kaisari, ile kutuhumiwa tuu ni kosa tosha hata bila kuthibitishwa, anahukumiwa!.

Hivyo ndivyo zilivyo tuhuma za TISS wetu, kuwa wale makirikiri wa Bashite ni TISS!, na yule mpuuzi wa Nape ni TISS!. Hivyo kama wale makirikiri wa Bashite waliovamia Clouds TV sio watu wao, TISS wasikae kimya wajitokeze na kukanusha!. Kama yule mpuuzi aliyemtishia Nape kwa bastola sio mtu wao, wajitokeze wakanushe. Huku kukaa kimya kunachukuliwa ni admission of guilt!.

Kama tuhuma dhidi ya TISS zimefika hadi kwenye Bunge letu Tukufu, na TISS iko chini ya Ikulu yetu, na Ikulu ni mahala patakatifu, tuhuma tuu kumhusu mke wa Kaisari zinatosha kumuondoa Ikulu asije akapanajisi patakatifu petu!. Hiyo TISS isikae kimya lazima ijitathimini na kujisafisha na uchafu wa makandokando haya!.

Huu mjadala unaoendelea kuhusu utekaji, utesaji na mauaji ambavyo vinahusishwa na idara yetu nyeti ya Usalama wa Taifa, TISS ni uthibitisho tosha kuwa TISS imechafuka inahitaji au kujisafisha au kusafishwa!.

Pamoja na Tanzania kuridhia mkakati wa Open Government Initiatives lakini kuna vitu huwezi kuvijadili openly lakini bado unaweza kuvichunguza na kuvifanyia kazi kimya kimya ila public ikaona matokeo na kurudisha imani.

Kuna watu wanadhani Usalama wa Taifa TISS wao ni malaika na hawawezi kabisa kufanya makosa kama madudu haya wanayotuhumiwa nayo sasa. No!, TISS sio malaika kwa sababu nayo inaongozwa na binadamu!.

Tiss huko nyuma iliwahi kufanya makosa ya utekaji, utesaji na hata uuaji, na ikafumuliwa!. Hivyo kwa vile tayari tunayo precedence ya vitendo viovu vya TISS huko nyuma, hivyo kwa kuutumia uthibitisho wa uovu huo, una justify kuwa kuna uwezekano ikawa ni kweli TISS is behind huu uovu na uchafu unaozungumziwa sasa Bungeni.

Lakini pia inawezekana sio TISS as TISS bali ni acts za individual members wa TISS wakifanya a "stand alone operations" bila kupokea command yoyote kutoka juu, hivyo vitendo vya wachache, vikaichafua TISS yetu collectively kwenye a collective responsibilities formula.

Pia inawezekana kabisa vitendo hivi vinafanywa na wahuni fulani, ambao wana pose as TISS just to make believe kuwa ni TISS kumbe sio TISS bali ni just impostors wanaochafua the good image ya TISS wetu waadilifu.

Whichever the case, TISS ijitokeze iwakane na kurudisha imani na TISS wetu

Hebu kwanza msikilizeni Tundu Lissu anasema nini kuhusu utekaji na utesaji wa TISS, hao anaowatetea ndio wenye bahati who could live to tell, hivyo ndio waliosalimika, only God knows kwa wale wasio na bahati hatima yao ilikuwaje because they couldn't live to tell!.

Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu! .

Hii sio mara ya kwanza kusikia serikali inafanya torture!. Hapa chini ni kisa cha kweli kabisa cha udhalimu wa TISS wa enzi hizo ambacho kilimhusu member wa familia yangu kujaribu kuwanusuru watuhumiwa wa torture na katika kufanya wema, wema wake ulimponza, RIP Mzee wangu Andrew Mayalla.

Kitendo kilichofanywa Clouds Media ni uthibitisho wa uhuni kama huu wa gross abuse of power na Nape alipotaka kufanya wema kuikingia kifua serikali yake isijinasibishe na uchafu huu, wema wake ulimponza.

Mwaka 1976 kule Mwanza kwenye eneo la Kigoto, watuhumiwa wa mauaji ya vikongwe walikuwa tortured na maofisa wa polisi.

Mzee wangu, Andrew Mayalla akiwa RSO wa Mwanza, akawanusuru watuhumiwa wawili, Masanja Makula Mazengenuka na Isaak Mwanamkoboko kutoka eneo la Kigoto baada ya mateso makubwa, wakiwa njiani wakamweza hawajala chochote kwa muda wa siku 3 za mateso ya usiku na mchana!.

Akaamua kuwapeleka Bugando, on their way akasimama mahali kuwanunulia soda na kitafunio, soda waliweza kunywa, kutafuna walishindwa.

Bugando akawakabidhi kwa Dr. Nkulila. The next day they were both dead, mtuhumiwa wa kwanza ni aliyewaleta!.

Hizo ni enzi za Nyerere, tulikuwa tukiishi Isamilo ya chini, next door ni RPC alikuwa akiitwa Mkwawa, nyumba ya tatu ni DSO. Just imagine majirani watatu wanaishi nyumba zinazofuatana wanapokutwa na kisanga.

Baada ya Taarifa kumfikia Nyerere, kuanzia Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi alipoteza uwaziri, IGP wa wakati huo Pundugu alipoteza kazi, Mkurugenzi wa Tiss, Mzena, alipoteza kazi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo, alipoteza kazi,

Mzee wangu, Mzee Mayalla, RSO, RPC, DSO na OCD wa Mwanza wote walistaafishwa kwa manufaa ya umma, tulihamishwa usiku usiku na kurudishwa kijijini (detention fulani za Nyerere).

Wakati yote haya yakifanyika, mimi nilikuwa mdogo sana, sikujua hili wala lile, hadi ilipoanza kuunguruma, Kesi ya Mauaji Mwanza, ndipo niligundua dingi alikuwa nani!, na thanks God, mtu pekee aliyenasuka ni Mzee Andrew Mayalla (RIP) kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na wakili Murtaza Lakha.

Kwa wale tuliofuatilia ile kesi ya Uhaini ya mwaka 1982 tulisoma jinsi TISS wanavyoteka, wanavyo tesa na wanavyo ua yakiwemo mauaji ya Martin Tamimu. Utekaji wa Hatty Magee, kule jijini Nairobi, etc.

Mahakama ndio Mhimili pekee wa haki ndani ya katiba yetu, kwenye kesi hiyo ya uhaini, tumeshuhudia watuhumiwa wakitoa ushuhuda jinsi walivyoteswa na TISS kwenye torture chambers zao na kulazimishwa kukiri, hivyo kupelekwa kwa Walinzi wa Amani kukiri kuhusika kwao halafu walipofika mahakamani wakavikana viapo vyao kwa Walinzi wa Amani na kusema waliteswa ndio maana wakakiri.

Japo torture ni kinyume cha sheria, polisi na TISS zote duniani wanatumia mbinu hizo kuhoji ambazo nyingine ni halali na nyingine ni haramu.

Marekani ndio inayoongoza kwa kutumia torture na kuihalalisha ila kwa vile ni kinyume cha sheria za nchi hiyo, wanalitumia gereza la Guantanamo Bay lililoko kwenye kisiwa cha Cuba ambako sio ardhi ya Marekani kufanya ushenzi huo.

Hivyo kama tuhuma hizi za Lisu ni kweli, hii sio mara ya kwanza kwa TISS kuhusishwa na makando kando ya ajabu!. Ya Ulimboka tuliyasoma Mwanahalisi, hadi yakamuibua msemaji wa Tiss ya wakati huo Jack Zoka.

Ya Kibanda nilishikwa sikio na mtu tete a tete ila hii nilielezwa ni wale vijana wa Kijitonyama ila it was a personal social issue!.

Yaliyotokea Clouds TV wote tumeyashuhudia kupitia CCTV, na yale makirikiri tumeyaona, na ya Nape Mnauye tumeyashuhudia live mubashara kwenye TV huku huyo mpuuzi akionekana wazi hadi sura watu wanamjua.

Naunga mkono TISS isijadiliwe na Kamati ya Bunge kwa uwazi kama ambavyo bajeti yao na ile ya defence hazijadiliwi, lakini bado wanaweza kuchunguzwa, na Sheria ya Usalama wa Taifa, sheria namba 15 ya mwaka 1996 ina mapungufu makubwa, imepitwa na wakati na kila siku sio tu inavunjwa na TISS wenyewe, bali pia inatumiwa vibaya na wanasiasa kuanzia Mkuu mwenyewe kuitumia kama bakora ya kuwachapia wapinzani!.

Just imagine, Mkuu wa nchi mwenyewe, anatamka hadharani kuwa simu za watu zinadukuliwa, bila wanaharakati kupiga kelele wakati inafahamika wazi kabisa, udukuzi kwa simu za wanasiasa ni kosa kisheria!, kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2) cha sheria ya usalama wa Taifa kinaizuia TISS kumfuatilia mtu yeyote wala kumpekua pekua au kumfanyia ujasusi kwa sababu ya msimamo wake kisiasa au Uhuru wake wa kuipinga Serikali. TISS inavunja sheria kila wakati kwenye eneo hili, rais anatangaza wanadukua simu za watu, by implication, waelewa wote, walielewa aliyedukuliwa!, kisha rais akasema kwa hasira, wasaliti wa aina hii, hawawezi kuachwa hivi hivi na kutolea mfano wa kinachowapata wasaliti wa jeshini, then mara mtajwa, yanamkuta ya kumkuta!, hata mtoto mdogo lazima atadhania ya kudhania!.

TISS inatakiwa kubadilika na kuunda kitengo madhubuti cha ujasusi wa kiuchumi, mfano, tuna Balozi zetu katika nchi zote zinazochenjua Mchanga wa makinikia, TISS wangekuwa wa maana, by now tungeisha jua hao Acacia wanapata nini kwenye Mchanga wetu, gharama za uchenjuaji container la Mchanga ni kiasi gani na kila kinachopatikana!, lakini wao wamekalia kudukua tuu simu, badala ya kudeal na serious issues za kiuchumi!. Kiukweli ile bili ya trilioni 190 ya TRA sio realistic, rais wetu ataonekana mjinga, Waziri Kabudi ataonekana mjinga, na nchi nzima tutaonekana ni taifa la wajinga, wakati ukweli utakapobainika, kitu ambacho TISS makini ingeweza kuzuia!.

Serikali yetu lazima ifanye damage control kwa msemaji wa TISS kuibuka na kumkana yule mpuuzi aliyemtisha Nape Bastola na kuwakana wale makirikiri wa Bashite!.

Huu ukimya wa Mwigulu, na serikali ni uthibitisho kuwa serikali has a hand kwenye hayo!. Ili kuonyesha kuwa serikali haihusiki na uhuni,upuuzi na ushenzi huu, rais Magufuli lazima akasirike kama Nyerere alivyo kasirika idara ya TISS inapochafuliwa, aliifumua mwanzo mwisho bila huruma.

Ukiondoa hizo torture za TISS zilizoibuliwa mahakamani, torture za jeshi la polisi ndio isiseme kabisa, innocent (until proven guilt) people have been tortured to death, hakuna kesi and nobody cares as if polisi are doing the right thing!.

Tukio la mwisho ni gunning down waendesha bodaboda wawili na abiria wao wawili kisa wamesimamishwa pale daraja la Mkapa wakapitiliza!. Polisi wakawaripoti hivyo walipofika next check point walimiminiwa tuu na kumaliza kazi hapo hapo, hawakukutwa na silaha yoyote!.

Haya ya polisi tumeisha yapigia sana kelele humu jukwaani.

IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!. Utampeleka JK The Hague-Part II!

Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This

Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Na kwa wale wenye interest na TISS kuijua zaidi, tembelea
Namna ya kujiunga na usalama wa Taifa | JamiiForums | The Home of

Kujiunga na Chuo cha Usalama wa Taifa kilichopo Mbweni, Bunju

Afisa usalama wa taifa "shushushu" ni nani? Anafanya shughuli gani

Shushushu (Afisa Usalama wa Taifa) ni mtu wa aina gani .

Natafuta Kazi Usalama Wa taifa | JamiiForums | The Home of Great .

Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa ...

Dr. Hassy Kitine, aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa .

Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE ...


Paskali
Update
Mkuu Mchambuzi
thanks very much for this, its very objective naona kama umemaliza kila kitu!.

It's true kuna lots of details nime avoid kutokana na uzalendo, pia nimemtaja Mzee wangu tuu kwa sababu alihusika direct, lakini sikumtaja mama yangu ambaye she is still alive and retired (hawaritayi kabisa) wala sikusema kuwa hata mimi almanusura!. Anyway haya tuyaache.

Although mhusika mkuu hataisoma kutokana na lingua uliyotumia, wahusika wenyewe wamesoma, na wamesikia labda waendelee tuu kutia pamba masikioni kwa sababu kujadili jambo lolote kuhusu TISS was considered a taboo hivyo bandiko hili kwa TISS ni kama abomination!.
Thanks again.
Paskali
Hawa wahanga wa mateso ya TISS ni watu wa aina gani? Je, wanapaswa kufanya wanayoyafanya na kwa staili ya aina hiyo wanayoyafanya hadi kuwa wahanga wa TISS? Je, huoni kwamba madhara yanayoweza kutokea kwa taifa na watu wake kutokana na vitendo vya hawa wahanga wa TISS ni makubwa kuliko mateso yao?
Tanzania kwanza, wahanga baadaye!
Linda usalama wako mwenyewe kwa kuwa muungwana, kwani usalama wako ndio usalama wa mwingine na taifa kwa ujumla!
 
Back
Top Bottom