TISS mnatuangusha tunaowaamini kwa kutomsaidia Rais na Mali za Taifa letu

TISS mnatuangusha tunaowaamini kwa kutomsaidia Rais na Mali za Taifa letu

Bila kuchukua hatua stahiki, tusitegemee lolote !!!
 
20230820_101918.jpg
take note
 
Jina TISS lilikua siri kubwa ,utendaji kazi wao ulikua impartial na smart, na ilikuwa ipo respected na iliwatia hofu mafisadi na wezi wa pie yetu, Leo hii hata kuficha number plates za magari yao ni zero, na upuuzi mkubwa kuweka double number plate kwenye gari moja na why mnatumia SA number plates kwenye magari yenu?
Wale Zacharia aliowalamba risasi kule Mara nao walikuwa hao hao au ni Tessy chocolate?
 
Unataka tisii wainuke waseme mama kwanini unamtuma huyu yankii kwa yoeli kuongelea mali zetu za huko chini ardhini ?

Au oops mbona unapanda gari la raia huko hewani mama?

Au waende roma wakamkamate papa oops sasa imekuwaje mnaongea ukweli ?

Nao upande wanasema .. pombe ni tamu .. ngoja tutaona mwisho ..
 
TISS inawezekana vipi Mtu anakopa au anaiba Pesa za Watanzania na Kukimbia nchi halafu hamjui?

TISS kuna Matukio mengi sana yanaendelea nchini ambayo mna Dhamana nayo Kiusalama ila huwa hakuna hatua mnazochukua Kukabiliana nazo.

Hivi TISS mnajua kuwa mnaaminika n kuheshimika sana na Watanzania kuliko hata Taasisi zingine nchini?

TISS kama kweli mngekuwa imara Kiutendaji Wala jana ( Mama / Rais ) asingelalamika vile huku akiwa na Masikitiko makubwa.

TISS kama mnaweza Kufuatilia mambo mengine ( hata yale yasiyokuwa ya Msingi ) mnashindwa nini Kukabiliana na Hawa Wanaoitafuna Kiulini Keki ya Tanzania?

TISS hivi Wengine ( Watu wa Kawaida ) hapa JamiiForums ( hasa Mimi GENTAMYCINE ) tukiwa tunawapeni Changamoto na Ushauri huwa mnaufanyia Kazi japo mnaweza kuwa mnatudharau mkiamini hatuna a,b,c's za Mambo ya Kiusalama?

TISS Wengine tunaumia kwa tunayoyaona na mambo kuharibika huku mkiwepo kwakuwa mmetulea ( hasa Kifamilia ) na tunajiuliza mbona TISS ya kuanzia Uhuru au aliyomaliza nayo Mzee ( Family Friend ) Marehemu Cornel Apson Mwang'onda ( Baba Jimmy ) aliyewahi kuwa DGIS ilikuwa Imara na kamwe haikutiliwa mashaka kama TISS ya sasa?

Mwisho ni Ombi langu tu GENTAMYCINE Kwenu TISS kuwa hebu rejeeni na ule mtindo wenu wa Kuajiri Watu Werevu hasa, wenye Vimelea vyote vya Kimuonekano kuwa wanafaa kwa Kazi yenu hiyo Kubwa na Nyeti lakini achaneni na Mtindo Siri wa sasa wa Kuajiri Watu wenu ( wa Idara ) kutoka UVCCM au kwa Vimemo vya Watawala Wastaafu, Watoto wao wenye Ushawishi, Wakuu ( Wakurugenzi wenu ), Wakuu wa Taasisi zingine za Kimedani, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Mahawara.

Japo mna Mapungufu yenu kadhaa ya Kiutendaji ila bado GENTAMYCINE nina Imani Kubwa nanyi na natambua pia Uwajibikaji wenu Uliotukuka katika Usalama wa Taifa letu hili zuri la Tanzania.

Unajaribu sema nini?? kwamba kama jamaa wasingeshikilia kipando cha rais (ndege) TISS wangeliona mapema na kushauri kitumike kipando kingine cha umma na kuachilia kile cha sirikali kikawa salama na mateka ya mwarabu?!!
 
Back
Top Bottom