wana bodi, nianze na mshangao kwanza, watu wanasoma habari imetoka mahakamani washindwa kuielewa!! mbona watu wamekuwa wagumu kuelewa? hawa ndo ma GT wa JF?
Tiss, wametajwa kuhusika maana ki usalama, walipaswa kushirikishwa, na kwa maelezo ya mtuhumiwa Mkurugenzi wa TBA walishirikishwa!! TBA ni idara ya serikali ina bodi ambayo ndo inapitisha miradi mikubwa kama huo. Bodi inateuliwa na raisi wa nchi, msimamizi ni wizara ya ujenzi. mawaziri wawili kwa nyakati tofauti wameusifia na kuutolea maelezo mradi huo. Magufuli na kawambwa, sasa mradi umechukua zaidi ya miaka 3 kukamilika, leo umekamilika mkurugenzi anashitakiwa.
Ndugu ma-GT, tujiulize mambo kiasi, jengo lilipo 75% ya mawaziri wanaliona jengo daily, viongozi wengi wanakaa masaki, mikocheni mbezi nk njia yao kuu ni ocean road jengo linaonekana, mh Rais na waziri mkuu, ofisi zao ziko mita chache kutoka lilipo jengo hilo. je nani alipaswa kulisimamisha?
Labda swali jingine je kesi ni kutoa kibali cha ujenzi au kujenga jengo linalokiuka taratibu za ujenzi wa eneo husika? Pengine tusogee mbele hatua moja tena, mkurugenzi wa TBA naye anaomba kibali cha ujenzi kwenye mamlaka husika, yaani wizara, JIJI na wilaya, je huko walitoa vibali gani? walijua ujenzi huo? moja zaidi je nani anawajibu wa kuzuia/kusimamisha ujenzi endapo mwekezaji amekiuka maelekezo?
Mwisho kwa mtazamo wangu, hapo hamna kesi, jamaa watatoka hapo na kesi itaisha, na hao pia watamwanga mboga/ maana TAKUKURU wamemwaga ugali. Tegemea kusikia majina makubwa TISS tayari wametajwa na leo wanakalia ghorofa tatu za juu. Mawaziri ni wapangaji, mengine mengi yanakuja.
SP