Tito Magoti: Waziri Mkuu unajisikiaje kuwa Kiongozi wa Serikali usiyetaka kuwajibika?

Anaandika Tito Magoti.​

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Nakuandikia barua ya wazi kwa heshima kubwa sana!

Ni mwaka wa saba tangu uwe Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CEO JTM hapa chini). Kuna mambo mengi unayojivunia. Pengine ndio maana umedumu katika nafasi yako hadi sasa.

Lakini Mheshimiwa, umewahi kujiuliza wananchi wanasemaje kuhusu utendaji wako kama Waziri Mkuu? Je, umewahi kutathmini umuhimu wa nafasi yako, unachofanya dhidi ya ufanisi unaotarajiwa?

Mhe Waziri Mkuu, bila mpangilio, niruhusu nikukumbushe yafuatayo:

Mwaka 2018 watu zaidi ya 130 walifariki katika ajali ya MV Nyerere, Ukerewe. Ukiwa CEO wa JMT, ulisitisha uokoaji kwakuwa giza liliingia. Serikali ikaenda kulala. Lakini Wananchi walipanda mitumbwi wakawasha ‘karabai’ zao kwenda kuwatafuta na kuwaokoa ndugu zao. Serikali ilikwenda kulala kwa udhuru wa giza, kana kwamba hilo lingesitisha maafa hata kwa nukta moja. Uliunda Tume. Ripoti unayo. Hakuna aliyewajibika.

Nov ‘22, ukiwa CEO JTM, ndege (Precision Air) imepata ajali ziwa Viktoria, Bukoba. Badala ya kuharakisha kuokoa uhai wa abiria, wewe na Serikali yako yote mliamua kuwapa adhabu ya kifo kwa uzembe na kutojali. Watu 19 walikufa kikatili huku wakitarajia msaada wako.

Ni kweli na inasikitisha kwamba haukujali hata kidogo. Uliendelea na shughuli zako. Baadaye sana ukaenda Kagera kupiga picha na manusura wa ajali. Na kusimamia mazishi. Ulionesha utayari na mamlaka katika kusimamia ‘sherehe ya mazishi’ kuliko kuokoa maisha ya watu. Ni sahihi kusema kwamba, ukiwa CEO JMT, kwa uzembe na kutojali, uliruhusu maisha ya watu 19 yadhulumiwe. Inasikitisha!

1*K3vuYFpkgX-ISV4GASX3vA.jpeg

Ndege ya shirika la Precision Air ikiwa imezama ndani ya ziwa Viktoria, Kegera.​

Mheshimiwa Waziri Mkuu, sio hayo tu!

Mlima Kilimanjaro umeriporiwa kuungua moto majuzi. Haukuitikia tukio hilo kwa wakati. Kuna haja ya kuliandikia UNESCO kuhusu uzembe huu unaojirudia.

Sept 2022 Polisi waliua raia watatu nyumbani kwetu Mara. Pia walimdhalilisha kingono binti mmoja kwa kumvua nguo wakimtaka afanya mapenzi na baba yake aliyevuliwa nguo vilevile. Binti yuko wapi? Serikali ambayo wewe ni CEO wake imefanya nini kando ya ule mzaha wa polisi?

Jan 2022 mfanyabiashara wa madini aliuliwa na Polisi Mtwara. Uliunda Tume. Ripoti yake haijulikani ilipo. Zipo taarifa kuwa makachero waliofunguliwa kesi watakuwa huru, ni suala la muda. Ripoti iko wapi. Nini kimefanyika zaidi?

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Una mamlaka makubwa sana kama CEO JMT. Lakini umekuwa ukitoa maagizo mengi ambayo ni maigizo. Mazingaombwe! Ni maigizo kwakuwa hayatekelezwi kwa vitendo. Kauli zako hazipewi uzito wowote, nikwambie ukweli.

Tangu uwe CEO JMT, umeunda Tume nyingi sana. Ni mara chache utasikia ama kuona Ripoti ya Tume hii ama ile imewekwa wazi kwa umma kusoma na kushiriki utekelezaji. Maagizo yako yanakuwa maigizo kwa mtindo huu.

Machi 2021, wakati wananchi wanamtafuta kiongozi wao, ulilitangazia Taifa kuwa Rais Magufuli ni mzima anachapa kazi. Ulisema ukiwa msikitini. Kumbe Rais alikuwa mgonjwa mahututi. Ukikumbuka tukio hili huwa unajiambia nini?

Mwaka 2016/20 mlitangazia vita ya kiuchumi. Sheria za ulinzi wa rasilimali zikaandikwa ghafla. Mkawaweka wafanyabiashara jela. Mkaunda Tume. Mkaanzisha kampuni ya madini. Juzi mmekiri sehemu ya ulaghai mliofanya katika vita ya kiuchumi. Baadhi ya sheria mmerekebisha. Ulikuwa CEO JMT na bado unadumu.

1*iD3mWsFzQfdffg6p9l1tgg.jpeg

Profesa Kabudi akikiri kwamba vita ya kiuchumi ilikuwa ni ulaghai​

Mwaka 2018/19 na kuendelea, ukiwa CEO JMT, ulishuhudia serikali yako ikifanya dhuluma dhidi ya wakulima wa zao la korosho. Biashara ya korosho hadi leo ni mazingaombwe matupu.

Mwaka 2019 kulitokea tetemeko la ardhi Kagera. Hakuna jambo la maana linalokumbukwa zaidi ya matumizi mabaya fedha za waathirika na kauli za kizembe kama: ‘sikuleta tetemeko,’ na nyingine za ajabu. Ulikuwa CEO JMT.

Tangu 2015 mmetunga Sheria lukuki kwa hati ya dharura. Sheria nyingi zinazobana ufurahiwaji wa haki za kisiasa na kiraia na kiuchumi. Mmeweka rekodi ya kuwa Serikali iliyotunga na kurekebisha baadhi ya sheria hizohizo ndani ya muda mfupi. Ukiwa CEO JMT, jiulize, mlibeba maslahi ya nani?

Ukiwa CEO JMT, maelfu wametupwa jela kwa kesi za uongo. Wapo waliotekwa, walioteswa na kupewa ulemavu wa kudumu. Kuna waliouwawa kikatili. Kuna waliofutiwa kesi baada ya kukaa jela muda mrefu. Yamefanyika ukiwa CEO JMT. Sijawahi kukusikia ukiomba radhi, kujuta ama kuhofia.

Ukiwa CEO JMT, wananchi wengi wamepotezwa. Hawajulikani walipo. Wamo wakosoaji wa serikali. Haujawahi kujishughulisha kuwatafuta ama kuomba msaada wa kuwatafuta.

Sep 2017, Wakili Mwandamizi Tundu Lissu alipigwa risasi 36 jijini Dodoma na ‘watu wasiojulikana.’ Jaribio la kudhulumu uhai wa mtu kiasi kile lilifanywa ukiwa CEO JMT. Hakuna jambo lolote la maana umewahi kufuatia tukio hilo.

Tangu 2016 ukiwa CEO JMT uliruhusu uwepo wa kundi la ‘watu wasiojulikana.’ Waliendesha ‘oparesheni’ dhidi ya wakosoaji wa serikali na zaidi. Watu walitekwa, kuuwawa na wengine hawajulikani walipo.

Ukiwa CEO JMT, umeshuhudia uporaji wa fedha za watu waliopewa kesi za uongo kwa jina la ‘plea bargain.’ Ukiwa CEO JMT, juzi mmeunda tume kuchunguza mwenendo wa zoezi la plea baragain. Unawezaje kuwa na ufanisi?
1*8OpHWjgKEYSBu4jQ_JNwRA.jpeg

Waendesha Mashitaka wakiwa na lundo la fedha za ‘plea bargain.’​

Ripoti za CAG kila mwaka zinaonesha ubadhilifu wa fedha za umma uliokithiri. Hakuna jambo lolote la maana umewahi kulifanya juu ya ripoti hizo. Hata maazimio ya Bunge kufuatia Ripoti za CAG haufuatilii utekelezaji wake. Haujawahi kujisikia vibaya kufuatia uzembe katika usimamizi unaopelekea wizi unaoandikwa na CAG kila mwaka tangu uwe CEO JTM. Ujasiri wa kipekee sana!

Ukiwa CEO JMT na mshirika wa CCM, kati ya 2016/20, ulishiriki jitihada zote za kuua demokrasia nchini Tanzania. Leo hatuna Bunge sababu ya ubinafsi wenu. Mahakama hali kadhalika. Utamaduni wa ‘uchawa’ nchini ni matokeo ya hofu zenu. Si jambo unalohofia ama kujutIa. Maana hadi leo mnalea viongozi wanaotishia na kuhujumu uhuru wa fikra nchini. Hii ni mbaya sana.

Matukio ya raia kuuwawa wakiwa chini ya polisi ni mengi. Mauaji yanatekelezwa na Polisi. Ukiwa CEO JMT, haujawahi kuitisha uchunguzi wowote huru dhidi ya matukio haya, wala kuchukua hata hatua za kisiasa.

Mwaka 2018 ukiwa CEO JTM, ulishuhudia polisi wakimuua mwanafunzi Akwilina Aqwilini kwa kumpiga risasi. Mliwashitaki ila baaadaye mkawafutia kesi. Hii ndiyo heshima mliyomchagulia Aqwilina. Hakustahili zaidi?

MKIRU na zaidi na matishio ya ugaidi yamedhulumu uhai wa watu wengi sana. Hakuna taarifa yoyote rasmi ya serikali ambayo wewe ni CEO wake kuhusu oparesheni ya MKIRU, idadi ya watu waliopoteza maisha na mwito wa usalama zaidi. Watu waliofunguliwa kesi za ugaidi kufuatia matukio haya wengi hawajashitakiwa. Wako mahabusu miaka sasa. Azory Gwanda aliuwawa katika muktadha huo pia. Tumejifunza nini. Ufanisi wenu kama Serikali ni upi?

Ukiwa CEO JMT, watumishi wa umma wamefukuzwa kwa uhakiki wa vyeti. Hivi karibuni mmeahidi kuwalipa fidia. Nani alisikiliza hizi kesi, kuna uhalifu, na kwanini fidia? Hamjawahi kuwa na umakini hata kidogo.

Ukiwa CEO JMT, watumishi wa umma wamedhulumiwa stahiki zao kwa miaka sita na zaidi, wakiwemo wastaafu. Hivi, Mheshimiwa, wewe umewahi kuishi bila mshahara ama marupurupu kwa angalau siku moja?

Mwaka 2019/20 Ukiwa CEO JMT, mlifuta haki ya Wananchi na AZAKI kufungua mashauri katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, hata bila aibu kwamba Mahakama hii muhimu ipo nchini, Arusha. Uamuzi huu umelisaidia nini taifa?

Ukiwa CEO JMT, umeshiriki kupuuza utekelezaji wa hukumu za Mahakama za Kimataifa, ikiwemo ya Afrika na ya Afrika Mashariki ambazo Tanzania ni mshirika. Mmeiweka nchi yetu sawa na mataifa yasiyojua wajibu wao kimataifa.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Kwakuwa orodha ni ndefu, ninaomba nikuulize tena, Mheshimiwa, unajisikiaje na unawezaje kuwa kiongozi wa Serikali iliyofeli, japo kwa haya machache?

Ninajua sina umri wa kukushauri ujiuzulu. Lakini nafurahi kukumbusha tulikotoka!
ubarikiwe sana mkuu
ilikuwa inaniuma sana nilipokuwa nakuona mahakamani
hatimaye mungu alisikia dua zangu hapo tarehe 17/3/2021
hakika nilifurahi sana usiku ule, acha mungu aitwe mungu
 
Viongozi wetu, kwa maneno yao wenyewe, wanastahili ma vi8 mapya kuendana na hadhi yao, na "walitusamehe" tozo, pia kwa maneno yao wenyewe.

Tuwashukuru na sio kutegemea zaidi kwa kutaka watuokoe tunapopatwa majanga.
 
Tunajua kuna njama za kumtoa ili makamba aje achukue kitu, kozi yeye anaonekana ndio tishio kwao,CCM mnalaana nyie , wa TZ wanashida mpaka basi mnashindwa kuwatimizia mahitaji Yao , nyie mnawaza kuendelea kubaki madarakani forever nyie NI 🚮🚮
 
Natamani kuongea ila acha tuendelee kupiga kazi… Mama endelea kusimamia mipango yako, wananchi wanakutegemea sana kuwavusha… hiki ni kipindi cha kuwavusha watanzania
 
Magoti!! magoti!!..... huyu! huyuuu!! aliyetekwa kizembe na Vibinti vi- Polisi kutoka chuo cha polisi Moshi au? Pale Mwenge?? Umeanza kunenepa tena, na mi-haki yako ya ubinadamu wote ni sawa siyo!

Unataka Majaliwa asilale? kisa ni ntoto mmakonde! wajiri Nkuu?? nini maana ya mgawanyo wa kazi?? anajua ku delegate power, au hukusoma weye mjita??...... Ngoja reo tunakuja kuku arrest na ri-afande Beatrice!!!

Naona mdomo sasa umeanza kunawiriii!...yaani kwa vile ni waziri Mkuu! basi afanye kila kitu! wewe unapika na kuogesha watoto nyumbani kwako?? km unafanya ivo utaitwa unagubu! hujui kuoa!

ukianguka chooni Majaliwa aende! mkeo akikunyima aende! au aka-ingilie kati!.....Km Jiwe alikuwa mripukaji/Mgonjwa wa akili basi mnamuweka na yeye huyo Majaliwa!...

Mbona wewe ulitekwa na vibinti tu! vikiwa mazoezini hatusemi kuwa ulikuwa mzembe?! kure kwenu kure kidume kufanyiwa ivo! ni fedheha kubwa sana! anaweza kufa! weye mbona hujafa unasubiri nini??

Acha unoko wa kijita/kiruri huo!! weee jamaa! unatafuta umaarufu nenda Somalia! Nigeria,Madagascar unasikia??...

weye Ule Muziki wa kimbiza kimbiza unaujua na weakness zako tunazo!! jifarague tu! tunajua pa kukushikia, safari hii hatutaki kuliliwa km litoto lidogo tunafanya kweri!....sasa endelea...najua unajua kuwa tutaonana LIVE!!

Msarighoko! si unamjua wewe na siku ile usiku ulimtaja!....
Punguza ujinga usio na manufaa.Ni mzigo tu kwako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna siku Watanzania watapata wokovu na haki yao kwa kuandikaandika, kubweka bweka na kulialia.

Haki inapatikana kwa watu kujitoa na kwa damu kumwagika, msidanganyike kuna siku haki itakuja mezani kama lunch box, haki hupiganiwa usiku na mchana mitaani na mabarabarani sio JF na kwenye keyboard.
 
Punguza ujinga usio na manufaa.Ni mzigo tu kwako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Bora mjinga!! siku akijifunza ataelewa!! kuliko weye Mpumbavu! kamwe hutaelewa kitu chochote hata tukikutwanga upya tukakuumba!.....Ni Makosa kuropoka hovyo kuhusu Waziri wako Mkuu!

Zama za udikteta unapotezwa faster! kafanye kazi ukome kumuongelea Waziri Mkuu! humpangii cha kufanya weye km nani kwanza?? unajua majukumu ya waziri wa kawaida kweli weye? au umeamua kuropoka tu??

Yeye Majaliwa ange wafufua wafu hao, kwa kuhudhuria kwake pale??...yeye ndoa aliwaua siyo?? kosa afanye Jiwe mkamuogopa!... leo mnamlilia Majaliwa??
 
Ww mapessa kila siku uzi wako ni PM tu?

Huyo Tito Magoti nae akili hana. Siyo kila kitu uanaharakati tu.

Majaliwa amekaliwa vibaya sana na Vijana wa Lumumba aka Buku 7, Vijana Wa Zanzibar, Nape Nnauye, J. Makamba, Mama Mkubwa, J.K. Kuna kijana mmoja dalali wa Siasa Zitto Zuberi Kabwe, juzi kwenye mdahalo wa Gesi kamdhihaki PM. Genge ni kubwa mnoo kumsakama PM. Wana hofu nae 2025.

Hivyo basi, Watanzania tusiwe wapumbavu na bendera fuata upepo..eti Kila baya Kassim Majaliwa. Aahh Hapana Aisee!!

Majaliwa usijibu. Komaa hivyo hivyo hadi 2025 tukupe nchi wa Bara.

Afu PM awe Anthony Mtakama.
Makamu wa Rais , Luhaga Mpina.
 
Ulionesha utayari na mamlaka katika kusimamia ‘sherehe ya mazishi’ kuliko kuokoa maisha ya watu.
Watu wa Musoma mna tatizo la msingi wa kujua kiswahili ivo ile waona ilikuwa ni sherehe ya Mazishi?? hujuikutofautisha sherehe na Msiba na hujui maana zake?

weye uliona tunafuraha pale?? iombe ofisi ya Waziri Mkuu samahani na mie ntasimamia zoezi hilo! Mapesa =Magoti!= ngoja kwanza!
 
Machi 2021, wakati wananchi wanamtafuta kiongozi wao, ulilitangazia Taifa kuwa Rais Magufuli ni mzima anachapa kazi. Ulisema ukiwa msikitini. Kumbe Rais alikuwa mgonjwa mahututi. Ukikumbuka tukio hili huwa unajiambia nini?
Hili jamaa nalo lina mtindio wa Ubongo nachelea kusema ivo kwa sababu zifuatazo!

1).Muheshimiwa Majaliwa Yeye siyo Daktari wa Binadamu na wala hajawahi kusomea somo lolote linalo husu tiba!..Lkn Magoti anataka Waziri atoe matamko ya kidaktari! huo ni ujinga magoti kasome tena!!

Madaktari wao km wao! ni kutoa matumaini kwa wauguzaji, hiyo ni sehemu ya tiba pia! waziri mkuu akiwa mmoja wao kwa hiyo madaktari walikuwa wanatibu tema nzima kwa kuwapa wao matumaini! kuhusu afya ya Mgonjwa!

2) Yeye km waziri alisomea wapi huo ufahamu wa kujua huyu ni mahututi na huyu si mahututi?? kitaalamu (Death comfirmations??) wataka sema majaliwa alijua jiwe atakufa?? na km alijua hivo kwa nini alimtoa kwa hao madaktari!

Kusema ni mzima na anaendelea na shughuli ni kweli kwa sababu tulimpelekea Forms zilizo kuwa zinahitaji signs zake akafanya kweli! lkn hali ikabadilika baadaye sana, ulitaka tuseme amekufa?? sasa hayo ni mawazo yako si yetu!

Ndo nasema weye Magoti tangu uanze kukubali kutumiwa akili yako haiko sawa! imekaa tenge katibiwe hutaki!
 
Punguza ujinga usio na manufaa.Ni mzigo tu kwako.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Ww mapessa kila siku uzi wako ni PM tu?

Huyo Tito Magoti nae akili hana. Siyo kila kitu uanaharakati tu.

Majaliwa amekaliwa vibaya sana na Vijana wa Lumumba aka Buku 7, Vijana Wa Zanzibar, Nape Nnauye, J. Makamba, Mama Mkubwa, J.K. Kuna kijana mmoja dalali wa Siasa Zitto Zuberi Kabwe, juzi kwenye mdahalo wa Gesi kamdhihaki PM. Genge ni kubwa mnoo kumsakama PM. Wana hofu nae 2025.

Hivyo basi, Watanzania tusiwe wapumbavu na bendera fuata upepo..eti Kila baya Kassim Majaliwa. Aahh Hapana Aisee!!

Majaliwa usijibu. Komaa hivyo hivyo hadi 2025 tukupe nchi wa Bara.

Afu PM awe Anthony Mtakama.
Makamu wa Rais , Luhaga Mpina.
Wahuni wamejipanga, na mpunga umeshatembea, nyumba ikikosa wakubwa au wakawepo na wasisikizwe, ni tafrani tu.
 
Mwaka 2016/20 mlitangazia vita ya kiuchumi. Sheria za ulinzi wa rasilimali zikaandikwa ghafla. Mkawaweka wafanyabiashara jela. Mkaunda Tume. Mkaanzisha kampuni ya madini. Juzi mmekiri sehemu ya ulaghai mliofanya katika vita ya kiuchumi. Baadhi ya sheria mmerekebisha. Ulikuwa CEO JMT na bado unadumu.
Kwani ukiwa waziri ndo usiwe mbunifu?? au usipeke waaarifu mahakamani?? sheria za Mahakama si ndi njia rahisi au hiyo ni serikali yako?? kuunda tume ni kutafuta kutenda haki ktk misingi ya sheria kosa lao nini?

huna lolote bana wee usitafute umaarufu!
 
Anayenishangaza zaidi ni Rais. Ina maana ameshindwa kumpata mtu mwingine ambaye angeimudu vema hiyo nafasi kuliko huyu ambaye inaonekana hana mipango wala maono, bali hushtuliwa na matukio?
Mkuu, tangu kifo, aliyeshika usukani anachofanya ni kusafiri na ku-twiti, akipata jukwaa, mipasho inarindima!

Waliopewa makali unawaona wakilindima tuwatakavyo, waliokuwa FIRM walitolewa kwa kigezo cha kuwaweka karibu kaka zangu ilhali ni kufuta alama za mtangulizi.

Ingawa pia nakubali kuwa, utendaji wa PM umedhihirisha wazi kuwa unategemea na Supervisor aliyenaye! Kwa sasa, mtindo wake ndo wa supervisor wake.
 
Ukiwa CEO JMT, wananchi wengi wamepotezwa. Hawajulikani walipo. Wamo wakosoaji wa serikali. Haujawahi kujishughulisha kuwatafuta ama kuomba msaada wa kuwatafuta.
watu kupotea kwani yeye ndo kawapoteza inawezekana weye unajua kitu unaweza kutusaidia walipo tuwafuate popote Duniani Watu hupotea mpka leo hawajapatikana hata mifupa sasa sie bongo si kisiwa au sie siyo Malaika wa kujua kila kitu!
 
Back
Top Bottom