Tiwa Savage: Mchepuko ulinidanganya, najuta kuvunja ndoa yangu, nampigia magoti mume wangu anisamehe

Tiwa Savage: Mchepuko ulinidanganya, najuta kuvunja ndoa yangu, nampigia magoti mume wangu anisamehe

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Aman iwe kwenu akina mama na akina Baba wote wa jamiiforum

Huko kwa wakuitwa TIWA SAVAGE kimeumana

Baada ya mchepuko kumpiga sound naye akajaa leo ndo kaanza kulia Lia na kumkumbuka mume wake wa ndoa

---
Msanii maarufu wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage amesema anajutia kuachana na mume wake, Tunji Balogun maarufu kama Teebillz na kuanzisha uhusiano na mwanaume mwingine.

Msanii huyo amebainisha hayo wakati akifanya mahojiano na jarida la Elle South Africa na kusema hiyo ndio moja ya kosa kubwa ambalo amewahi kufanya.

"Nilimfanya mume wangu asijisikie kuwa mwanaume kwa sababu nilianza kutoka na mwanaume mwingine, bado nampenda na najua nilimkosea lakini nataka kurekebisha mambo na turudiane,” amesema

"Sina uhakika kuwa anaweza kunirudisha tena na sikuwahi kutaka kumpa talaka lakini mwanaume mwingine alinihadaa nimuache mume wangu niwe naye.”

Tiwa ameongeza kuwa sio rahisi mwanamke aliyemwacha mumewe kuolewa na mwanamume mwingine huku akiwasihi wanawake kutofanya alichokifanya.

Mwananchi
 
Hivi kwani hakuna wanaume wanaoshawishiwa na michepuko yao na kuachana na wake zao kisha mambo yakigeuka wanawarudia wake zao, au yakimtokea mwanaume ni sawa ila yakimtokea mwanamke ndio hana akili ili mradi tu mwanamke ndio aonekana ana shida, hebu pelekeni stress zenu huko wapumbavu wapo jinsia zote siyo wanawake tu mada inamhusu tiwa savage majitu yanakuja kusema wanawake hawana akili kawaambieni hivyo mama zenu
 
Una hoja nzuri sema umeandika kwa jaziba sana

Andika vizuri ueleweke

Kwahiyo wewe ni mke mwema siyo mjinga mjinga kama TIWA SAVAGE?
 
Ebu weka kwanza picha ya huyo Tiwa, maana usidhani sisi wote tunapajua huko Sauzi kama sio Naija...😐
artist-thumbnail-tiwa-savage.jpg
 
Back
Top Bottom