Tizama picha hii ili ufahamu kuwa Rais Samia aliandaliwa na hajafika hapo alipo kwa kubahatisha

Tizama picha hii ili ufahamu kuwa Rais Samia aliandaliwa na hajafika hapo alipo kwa kubahatisha

Mimi nichukie watu kupewa $3 /day kumsifia mama Abdul?

Ushahidi gani unahitaji , nyie na lile group la Ummy Mwalimu akiwa waziri wa afya kuwalipa watu kusambaza hashtag mlidhani hamjulikani?
Endelea kuumia tu.Mama anapendwa na watanzania kwa hiyari ya mioyo yao.na siyo kulazimishwa au kwa malipo.
 
Ashindwe kwenye kufanya nini? Imeandikwa katika Biblia kuwa kwa kila jambo na majira yake na wakati kwa kusudi maalumu chini ya Mbingu. Unaifahamu safari ya sana wa Israel? Je nani aliwatoa kutoka Israel? Ni nani aliwafikisha Canaan?
Kwahio na wabakaji walawiti na vifo vya Albino vyote vina kusudi maalumu..., Na kwa nchi za mbali kufanya mababu zako watumwa na kuwafanyisha kazi hadi kuwaambia utamaduni wao ni wa kipumbavu na kuwaletea hio Imani yako unayotagaza leo ilikuwa ni mipango yake to what end....

Ukipenda kuchanganya imani na vitu factual usiingie na kutoka au kuchagua hiki na kile nenda mzima mzina (ila kwa taarifa yako it wont make logical sense)
 
Kwahio na wabakaji walawiti na vifo vya Albino vyote vina kusudi maalumu..., Na kwa nchi za mbali kufanya mababu zako watumwa na kuwafanyisha kazi hadi kuwaambia utamaduni wao ni wa kipumbavu na kuwaletea hio Imani yako unayotagaza leo ilikuwa ni mipango yake to what end....

Ukipenda kuchanganya imani na vitu factual usiingie na kutoka au kuchagua hiki na kile nenda mzima mzina (ila kwa taarifa yako it wont make logical sense)
Kwani hao maarubino wanaouwawa na nani kama siyo wanajamii wenyewe ikiwepo wazazi wa watoto husika.
 
Huyu chawa yupo jamaa mmoja jukwaani anamfahamu , anasema alimpambania sana 2022 apate ukarani kwenye sensa ya watu na makazi.

Ila alimuangusha sana kutokana na uduni wake kielimu maana ni class 7 dropout .

Sasa mtu kama huyu akipewa 7k kumsifia Makonda , Kafulila , na Samia anaona ndio kapata bingo.
Huyu ni mpuuzi sn hata mimi tunafahamiana vizuri sn
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huwa nawaambieni siku zote kuwa Rais Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuja kuliongoza Taifa letu.Hajafika hapo alipo kwa kubahatisha ,hajafika hapo alipo kwa bahati mbaya ,hayupo kwenye urais kama ajali,hakusukumizwa na kufika hapo alipo kimzobemzobe .

Amefika hapo kwa Mipango ya Mungu aliyemchorea Ramani na kuwapa watu maono na ndoto kwa ajili ya kumuandaa, kumpika,kumuivisha na kumkomaza kiuongozi. Ndio sababu tangia kuapishwa kwake hajawahi kuonyesha ugeni wala hofu wala uoga katika nafasi ya Urais .

Ndio sababu amekuwa mtu mtulivu na makini sana katika kuongoza Taifa letu.Ndio sababu ya kuja na 4R ,ndio sababu ya kuona Taifa halikukwama kusonga mbele na kuendelea na safari hata baada ya kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli Rais wa awamu ya Tano.

Ndio Maana mnaona ni kiongozi mwenye utulivu katika maamuzi.l,staha na unyenyekevu katika kuzungumza,misimamo ya kiuongozi,dira, muelekeo na Maono ya kiuongozi.ndio sababu mnaona anajuwa na kuelewa vyema sana wapi Taifa limetoka na wapi linapaswa kwenda na kuelekea na wapi lipite.

Hii ndio sababu hateteleki wala kuteteleshwa na vishindo vya aina yoyote ile.ndio sababu ameendelea kuwa madhubuti na imara sana katika kuliongoza Taifa letu na kulifanya Taifa letu kuendelea kutamalaki kwa amani na utulivu wakati wote huku umoja wa kitaifa ukiwa imara kuliko wakati mwingine wowote ule katika Historia ya Taifa letu.

Rais Samia aliingia Umakamu wa Rais Na hatimaye Urais akiwa ameiva kisawasawa kiuongozi.ndio sababu alifahamu wapi aanzie na hatua ipi achukue katika wakati upi na muda upi.ndio sababu alijuwa wapi pafanyiwe mabadiliko na maboresho,Ndio sababu mnaona aliposhika madaraka ya Urais hakuwa na maneno ya kulalamika lalamika au kumlaumu mtu au kuwakatisha watu tamaa au kuteteleka au kumtupia mtu shutuma.

Bali alianza kwa kuwapatia Matumaini watanzania,kuwaonyesha nuru na mwanga ya huko tuendako na kuwaonyesha kuwa Safari ni lazima iendelee na kwa mafanikio makubwa kwa Uweza wa Mungu Mwenyewe. Alianza kwa kuwaonyesha watanzania kuwa wapo katika mikono salama na wataendelea kuwa salama na wenye amani na utulivu.Alianza kwa kuwaleta pamoja watanzania na kuwaambia sisi ni Taifa moja na sote ni wamoja na tujenge Taifa letu kwa pamoja na yeye alikuwa yupo tayari na imara kutuvusha na kulivusha Taifa.

Na kwa hakika Rais wetu Mpendwa kipenzi chetu watanzania hajawahi kutuangusha na sasa kila mtu anajiona fahari kuzaliwa Tanzania,kuongozwa na Rais Samia na kuendelea kumuunga mkono ili aongoze tena muhula mwingine hapo Mwakani. Ndio maana mnaona wote waliokuwa uhamishoni walirejea haraka sana na kuendelea na ujenzi wa Taifa na hakuna mpaka sasa aliyejutia uamuzi wake wa kurejea NchiniView attachment 3108205

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mama Samia alikuwa anaishi Ikulu wakati wa JK.

Keyword: Anaishi.
 
Back
Top Bottom