Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Sasa kuzungumzia muungano wa ACT na Chadema si ndio umeizungumzia ACT ambayo Lissu anaona ni moja ya chama kinachotumika tu kuvuruga upinzani kwamba hakijawahi kuwa na shida na serikali. Kwa sababu kwa maelezo ya Lissu alisema kuwa 2015 ACT na aliyekuwa mgombea wao wakati huo Anna Mghwila,ni kwamba hawakuwa wapinzani bali waliwekwa tu ili kupambana na Lowassa. Na ndiyo maana Mghwila akaja kuzawadiwa cheo cha ukuu wa mkoa.Hivi watu wanazungumzia ACT au wanazungumzia "muungano" wa ACT na CHADEMA?! Na wanazungumzia ACT na CHADEMA kwa sababu CHADEMA wametangaza kumuunga mkono Maalimu Seif kule Zanzibar na hapa ililetwa habari kuhusu Zitto kutangaza makubaliano kati ya ACT na CHADEMA kwamba ACT imuunge Tundu Lissu!!
Sasa hilo suala linahusishwa na issue inayodaliwa hapa kwa sababu kwa muda mrefu UDP na TLP walitangaza kumuunga mkono JPM lakini kila zilipoletwa tetesi kuhusu ACT na CHADEMA ku-team up, NEC wakawa wanatoka mbele na kudai kwamba hiyo ni kinyume na sheria!
Ni kutokana na hilo, ndo maana watu wanaamini tangazo la UDP na TLP kutangaza kutomuunga tena JPM ni janja tu ya NEC kuepuka zile lawama kwanini hakuwahi kupinga suala la TLP na UDP kumuunga mkono JPM lakini wawe wanapinga suala la Lissu kumuunga mkono Maalimu Seif na Membe kumuunga mkono Lissu!!
Ndio maana nasema hiyo NEC haiwezi kusumbukwa akili na huo muungano wa vyama ambao chama kimoja ni pandikizi la chama tawala.