Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwako Mwabukusi, TLS na wadau wote wanaoguswa na ukiukwaji wa haki za binadamu na udhalilishaji wa utu (dignity) wa mwanadamu nchini.
Hali za mahabusu na magereza hapa nchini ni ambazo hazifai kwa binadamu kuwekwa. Ni jambo ambalo kila mtu anajua kwamba mfumo wa mahabusu na magereza zetu ni ule wa kikoloni, ambao ulilenga katika kuadhibu na kumdalilisha mwafrika, kumtoa utu. Wazungu waliojenga mfumo huu hawakupelekwa huko pale walipofanya kosa au uhalifu, kwa sababu waliojenga walijua hakufai mwanadamu kuwekwa huko.
Soma: Hali ya Magereza Mahabusu na Wafungwa
Na mbaya zaidi serikali yetu, ikitambua magereza na mahabusu zetu hazifai kuwekwa mwanadamu, wameamua kuweka vyumba maalumu kwa "vigogo" wanapokuwa mahabusu gerezani. Yaani serikali imeamua kuna tabaka la watu nchini ambalo halipaswi kupelekwa kule ambako mwananchi wa kawaida atapelekwa huko mahabusu au gerezani!
Miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru bado tunafanya kitu kile kile huku tukiwalaani wakoloni kwa ukosefu mkubwa wa haki za binadamu na udhalilishaji wa mwafrika. Imefika sasa hili lipingwe mahakamani ili serikali ilazimishwe kubadili huu mfumo wenye kutojali utu wa Watanzania kama wanadamu wanaostahili heshima. Kwa mfano, kwa nini tuendelee kutumia mfumo wa kujisaidia ambao wakoloni waliutumia ili kutudhalilisha watu weusi?
Tuna mfumo wa mahabusu ambao kupelekwa huko ndio adhabu yako, mbali na kama ukifungwa. Tukumbuke huko mahabusu na magereza sio wote wanaopelekwa wanakuwa na hatia. Mhalifu adhabu yake inapaswwa kuwa kutengwa na jamii, sio kudhalilishwa na kuvuliwa utu wake kama mwanadamu.
Tungependa jambo hili lifikishwe mahakamani, ili hukumu rasmi itolewe kwamba mfumo wa mahabusu na magereza Tanzania upo kwa namna kubwa ya ukosefu wa haki za binadamu, kudhalilisha watu na kuwaondolea utu wao, iwe wana hatia au la.
Mwabukusi, tafadhali tusaidie katika hili.