chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Nimeona Rais wa TLS akiwa anahojiwa na chombo cha habari akiwatusi watanzania kwamba wanafuata mambo ya hovyo na yasiyo ya maana, na akatoa mfano wa watanzania kuwa na mapenzi na simba na yanga kiasi kwamba wanaweza kutembea uchi
Hii ni dharau kubwa kwa klabu hizo ambazo zimejijenga kwa miaka mingi katika mioyo ya watanzania. Kama wao wanathamini demokrasia, kwa nini wanadharau machaguo ya watanzania na kuwapangia maisha?.
Pia mashabiki wa timu hizo ni watu wazima kiumri, kusema kwamba wanaweza kutembea uchi ni dharau kubwa nyingine kwa watu wa umri wa wazazi wake
Nani kawazuio wasiimarishe vyama vyao ili wananchi wavipende? Yaani watu hata harusini, mpirani, disco wasiende?
Nalaani sana kauli ya TLS kwa kuwa iko chini ya kiwango na inapaswa kulaaniwa na kila mzalendo, mwanamichezo wa nchi hii.
N. B:
Hata Mwabukusi hakuandamana, ila alitaka wengine waandamane, chichi dodo