TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam

Wale mbwa hata ikibidi kunyongwa ni sawa tu hawana utu kabisa wamemdharirisha sana yule binti.
Inasemekana polisi wameshampata binti kwa mahojiano ili watuhumiwa wapatikane ila nimesikia kuna dada yake kwa uchungu amekunywa sumu hata hivyo wasamaria wema wamemkimbiza hospital.
 
Umesikiaaaaa
Anyway
wale si mbwa na ni watu wanahaki zao.
Wanapaswa kupelekwa mahakaman nao wasikilizwe ili mahakama itende haki
 
Ila nimeshtuka sana nilipoona polisi imetoa namba za simu kuomba isaidiwe kuwapata. Jeshi lenye kila aina ya nyenzo linaombaje kusaidiwa na raia kuwakamata washenzi kama wale? Wakija wahalifu wakubwa kama kina Carlos jeshi litafanyaje?
Jeshi halijawahi na halitakaloshindwe
Mtego huo mkuu
 
Ni kosa kisheria kumpiga mtu kipara alafu ukajorekodi na ukasambaza so hata kama hawakumlazimisha hiyo bado ni kesi, kimsingi hapo kuna kesi zaidi ya moja hao majamaa hawana pakutokea, mfano yule alosema atamla jokeri nae asishitakiwe ? Eti me nikiingia nakula mavi, nakula jokeri daaah 😂😂😂
 
Kwa haraka haraka pana kesi tatu
Gang rape
Kusambaza.
Kufira
 
Sizan kama ni kazi yao
 
Na ndio nilikua naandika kile ninachoona ni sahihi kwangu.
Unarukaruka kijana, huku upo kule upo.
Mara useme tusubiri mara na wewe unajaa tena kua unaandika kilicho sahihi kwako kabla ya mahakama kutoa hukumu kama ulivyojishauri.
 
Shule,shule hakuna.
 
Nakubaliana na wewe kabisa, wale unakuta ni form 4 graduates kabisa, halafu ndio wanatabia zile.
Wanajiita majeshi kunoga,wao hutumia nguvu badala ya akili,nimesikia mwenye mme ni kapteni nimeshangaa afisa wa jeshi kuwa mjinga namna ile.
 
Lakini kwa upande mwingine huenda yawezekana hao waliofanya hivyo walikuwa wapo sahihi, kwa sababu nasikia kwamba hao ni Askari, na walifanya kitendo hicho baada ya kupewa amri na Kamanda wao mwenye cheo Cha Kapteni. Sijui taarifa hii Ina ukweli gani, lakini kama taarifa hizi zitakuwa zina ukweli maana yake ni kwamba hao wahusika walikuwa wanatekeleza 'amri halali kutoka kwa Kamanda wao.' Tukumbuke kwamba utendaji katikà Jeshi huongozwa na AMRI kutoka kwa Mkubwa wako aliye juu, kupinga kutekeleza amri kutoka kwa Kamanda wako aliyekuzidi Cheo inahesabika Kama kosa baya Sana la insurbonation au Uhaini.

Aidha, pia wa-Tanzania wakumbuke kwamba mambo kama hayo yamekuwa yakifanyika Sana kwenye hivi 'Vyombo vyetu' vinavyotuhumiwa na mkasa huu. Mathalani, baadhi ya Watekwaji ambao wamekuwa wakitekwa na wale 'Watu wasiojulikana' , wakati wakibahatika kurejea uraiani baadhi ya hao Watekwaji imejulikana kwamba kwa wakati fulani fulani waliteswa kwa 'kufanyiwa vitendo viovu vya namna hiyo' kama alivyofanyiwa huyo binti. Hata yule Bosi aliyekuwa Wizara ya Fedha ambaye alitekwa na Kisha maiti yake ilionekana na kuokotwa huko Mkuranga, malalamiko ya kufanyiwa vitendo vya namna hiyo pia yalisikika. Kwa wale waliofuatilia kisa hicho nafikiri mtakuwa mnakumbuka.
 
Duuh, aisee sio kwa ubaya lakini hii ni non sense kabisa, kwamba unataka kusema kisa ni amri ndo wafanye hivyo?🤔. Unalichukulia jambo kiwepesi sababu hayajamkuta mtu unayemfahamu, ingekua uyo dada ni ndugu yako sidhani kama ungewaza ayo mambo ya uhalali na uchwara mwingine unaojaribu kuutetea. NON SENSE​
 
Laanaa inatutafuna jaman
 

uko sahihi.
kuna maswali mengi sana yanahitaji majibu makini.
kwasasa watu wanapiga kelele tu. tuache uchunguzi ufanyike.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…