PreGE2025 TLS yalipuka! Yalaani kukamatwa kwa Tundu Lissu, na kutoa mapendekezo

PreGE2025 TLS yalipuka! Yalaani kukamatwa kwa Tundu Lissu, na kutoa mapendekezo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hatuwategemei 100%, wao ni taasisi ya haki. Na siku zote mdai haki ana nguvu hata ikicheleweshwa.
Pole sana mdogo wangu watatoa maoni kama wewe ni hiyari kusikilizwa au kupuuzwa nchi inaendeshwa kwa katiba hao TEC wako wana lipi!
 
Pole sana mdogo wangu watatoa maoni kama wewe ni hiyari kusikilizwa au kupuuzwa nchi inaendeshwa kwa katiba hao TEC wako wana lipi!
Ni kweli, na hiyo katiba inaruhusu ccm iwe inapora chaguzi za nchi.
 
Niliwahi kusema Saa100ni mtu hatari kuliko JPM.

TLS kazeni buti,kitaeleweka
 
Ni kweli, na hiyo katiba inaruhusu ccm iwe inapora chaguzi za nchi.
Kwani mnashiriki uchaguzi sasa hivi sitaki kujadili uchaguzi na watu wasio shiriki chama mfu lengo lake ni uhalifu na uasi!
 
Kitendo Cha chadema,kutokushiriki uchaguzi ni pigo kwa wananchi walio wengi ambao hawana vyama.
Samia ataongoza nchi kwa shida kubwa kuliko alivyo tarajia
 
Kwani mnashiriki uchaguzi sasa hivi sitaki kujadili uchaguzi na watu wasio shiriki chama mfu lengo lake ni uhalifu na uasi!
Chaguzi zinatumia kodi zetu. Wakati uchaguzi ni vyama vya siasa tu. Kaa humo boss.
 
Zaman ukiw kiongoz unakuw unawez shauri na watu wako wa karbu ambao wako faith ata waziz pia wazee ndan ya familia , ila sasa washauri ni machawa
 
Ccm imejaa wajinga wasio penda haki ila wanahubiri amani
 
Nyumba isio na baba lazima mambo ya hovyo na ajab ajab yatokee
 
CHAMA CHA SHERIA TANGANYIKA (TLS)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKAMATWA KWA WAKILI TUNDU A. LISSU
​

Baraza la Uongozi la Chama cha Sheria Tanganyika (TLS) linatoa taarifa hii kwa umma kuhusu kitendo cha kukamatwa kwa Wakili Tundu Antipas Lissu.

Katika kutekeleza wajibu wake wa kikatiba na kisheria wa kulinda utawala wa sheria, kukuza haki na kutetea heshima ya taaluma ya sheria, TLS imesikitishwa sana na mazingira ya kukamatwa na kushikiliwa kwa Wakili Tundu Lissu. TLS imeshtushwa zaidi na tuhuma za ukiukwaji wa haki za kikatiba na taratibu za mwenendo wa mashauri ya jinai katika tukio hili.

UKIUKWAJI WA HAKI ZA KIKATIBA NA KISHERIA

TLS inalaani vikali kukamatwa kwa Wakili Tundu A. Lissu, ambapo kunaonekana kuwa na mlolongo wa vitendo visivyo halali vinavyokwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20, Toleo la 2022. Ukiukwaji huu unajumuisha:

a) Ukiukwaji wa Haki ya Kujiunga na Vyama au Vikundi

Kukamatwa kwa Bw. Lissu ni kinyume na Kifungu cha 20 cha Katiba kinachotoa haki ya kujiunga kwa hiari. Kuwekwa kwake kizuizini kulizuia wananchi kutumia haki yao ya kuhudhuria na kusikiliza mkutano wa kisiasa uliotambulika kisheria, hivyo kukiuka haki zao za kisiasa na ushiriki. Aidha, namna ya ukamataji huo ilimnyima haki ya kushiriki kwa uhuru kama kiongozi wa kisiasa.

b) Ukiukwaji wa Haki ya Uhuru wa Maoni

Kifungu cha 18 cha Katiba kinatoa haki ya kila raia kutoa maoni. Kukamatwa kwa Bw. Lissu kama mwanasiasa mashuhuri wa upinzani kunaonekana kuwa ni jitihada za kimakusudi za kuzima haki yake ya kutoa maoni na kushiriki katika mijadala ya umma.

c) Kukosa Uzingatiaji wa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai

Taratibu nyingi za kisheria zilikiukwa, kinyume na masharti ya Vifungu vya 11, 12, 14, 21, 23 na 54 vya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai. Hali hii ilijidhihirisha kwa:

• Kushindwa kueleza kosa analotuhumiwa nalo kwa uwazi wakati wa kukamatwa;
• Kukamatwa bila hati halali ya kukamatwa;
• Kunyimwa haki ya kuwasiliana na wakili wake, familia au watu wa karibu;
• Kutumika kwa nguvu kupita kiasi, kinyume na sheria zinazopiga marufuku matumizi
ya nguvu za kuweza kusababisha kifo au madhara makubwa ya mwili.

MAPENDEKEZO YA TLS KUTOKANA NA TUKIO HILI​

Kutokana na ukiukwaji huu wa haki za kikatiba na kisheria, na kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda taaluma ya sheria na misingi ya demokrasia nchini, TLS imeazimia yafuatayo:

i. Kulaani Kukamatwa Kinyume cha Sheria

TLS inalaani vikali kukamatwa na kushikiliwa kwa Wakili Tundu A. Lissu kama ukiukwaji wa haki za kikatiba na tishio kwa utawala wa sheria na demokrasia nchini.

ii. Kukuza Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Amani

TLS inawahimiza wanasiasa wote na umma kwa ujumla kudumisha amani na kutatua migogoro kwa njia zisizo za vurugu, hasa katika kipindi hiki muhimu kuelekea uchaguzi mkuu.

iii. Wito wa Mageuzi ya Kisiasa na Kisheria

TLS inatoa wito wa kufanyika kwa mageuzi ya kisiasa na kisheria kwa haraka ili kuhakikisha ushiriki wa haki, jumuishi na wa kisheria katika mchakato wa kisiasa wa kitaifa, na hivyo kuimarisha utulivu wa kidemokrasia.

iv. Utekelezaji wa Sheria kwa Misingi ya Ushahidi

Vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia ushahidi wa kweli na kufuata kikamilifu taratibu za kisheria, hasa katika kushughulikia masuala yanayohusu wanasiasa au wanataaluma wa sheria.

v. Kuzuia Kujitokeza kwa Taharuki ya Kitaifa

Kukamatwa kwa wanasiasa kinyume na sheria kunaweza kusababisha upinzani na machafuko. Mamlaka zinapaswa kuchukua hatua za kisheria na za tahadhari ili kudumisha amani na umoja wa kitaifa, na kuepusha hali ya hofu miongoni mwa wanasiasa kuelekea uchaguzi mkuu.

vi. Kukuza Mazungumzo Kati ya Vyama vya Siasa

TLS inahimiza mazungumzo ya wazi na ya kujenga kati ya vyama vya siasa kama njia ya kupunguza mvutano na kukuza mshikamano wa kitaifa.

vii. Kuimarisha Uwezo wa Kisheria katika Ofisi za Umma

TLS inapendekeza kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mamlaka za Mashtaka zizingatie viwango vya juu vya umahiri na weledi wa kisheria, hasa katika kushughulikia masuala yenye mvutano wa kisiasa.

viii. Uchambuzi wa Kina wa Mashtaka ya Uasi

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anatakiwa kuhakikisha kuwa mashtaka mazito kama ya uasi yanaungwa mkono na ushahidi madhubuti na hoja za kisheria. Uongozi wa kisiasa pekee hauwezi kuchukuliwa kuwa ni kitendo cha uasi kwa mujibu wa sheria zilizopo.

ix. Kuachiwa Huru Mara Moja kwa Wakili Tundu A. Lissu

TLS inatoa wito wa kuachiwa mara moja na bila masharti yoyote kwa Wakili Tundu A. Lissu. Kukamatwa kwake kunadhoofisha heshima ya taaluma ya sheria na misingi ya haki. Kuendelea kushikiliwa kwake kunaashiria vitisho kwa wanasheria na washiriki wa siasa nchini. Iwapo wito huu hautazingatiwa, TLS inahifadhi haki ya kupendekeza kusitishwa kwa huduma za uwakilishi wa kesi za msaada wa kisheria (dock brief) na huduma nyingine za kisheria za kujitolea zinazotolewa na TLS na wanachama wake, kama njia ya amani ya kupinga vitendo vya unyanyasaji na mashtaka yenye mlengo wa kisiasa.

WITO

Chama cha Wanasheria Tanganyika kinathibitisha tena dhamira yake ya dhati katika kutetea Katiba, haki za binadamu na utawala wa sheria. Tunazisihi mamlaka husika likiwemo Jeshi la Polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kutekeleza majukumu yao kwa haki, usawa na kufuata sheria, hasa katika kushughulikia masuala yanayohusu siasa na ushiriki wa umma.

“Haki haipaswi tu kutendeka; bali ionekane dhahiri kuwa inatendeka.”​

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Sheria Tanganyika
Boniface Mwabukusi
Rais
 

Attachments

  • VID-20241210-WA0000.mp4
    2.4 MB
Back
Top Bottom