PreGE2025 TLS yalipuka! Yalaani kukamatwa kwa Tundu Lissu, na kutoa mapendekezo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wanabodi,

Hili ni Tamko la TLS.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKAMATWA KWA WAKILI TUNDU A. LISSU
Baraza la Uongozi la Chama cha Sheria Tanganyika (TLS) linatoa taarifa hii kwa umma kuhusukitendo cha kukamatwa kwa Wakili Tundu Antipas Lissu.

Katika kutekeleza wajibu wake wa kikatiba na kisheria wa kulinda utawala wa sheria, kukuzahaki na kutetea heshima ya taaluma ya sheria, TLS imesikitishwa sana na mazingira yakukamatwa na kushikiliwa kwa Wakili Tundu Lissu. TLS imeshtushwa zaidi na tuhuma zaukiukwaji wa haki za kikatiba na taratibu za mwenendo wa mashauri ya jinai katika tukio hili.

UKIUKWAJI WA HAKI ZA KIKATIBA NA KISHERIA

TLS inalaani vikali kukamatwa kwa Wakili Tundu A. Lissu, ambapo kunaonekana kuwa namlolongo wa vitendo visivyo halali vinavyokwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Mwenendo wa Mashauri yaJinai, Sura ya 20, Toleo la 2022. Ukiukwaji huu unajumuisha:

a) Ukiukwaji wa Haki ya Kujiunga na Vyama au Vikundi

Kukamatwa kwa Bw. Lissu ni kinyume na Kifungu cha 20 cha Katiba kinachotoa haki yakujiunga kwa hiari. Kuwekwa kwake kizuizini kulizuia wananchi kutumia haki yao yakuhudhuria na kusikiliza mkutano wa kisiasa uliotambulika kisheria, hivyo kukiuka haki zao zakisiasa na ushiriki. Aidha, namna ya ukamataji huo ilimnyima haki ya kushiriki kwa uhuru kamakiongozi wa kisiasa.

b) Ukiukwaji wa Haki ya Uhuru wa Maoni

Kifungu cha 18 cha Katiba kinatoa haki ya kila raia kutoa maoni. Kukamatwa kwa Bw. Lissukama mwanasiasa mashuhuri wa upinzani kunaonekana kuwa ni jitihada za kimakusudi zakuzima haki yake ya kutoa maoni na kushiriki katika mijadala ya umma.

c) Kukosa Uzingatiaji wa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai

Taratibu nyingi za kisheria zilikiukwa, kinyume na masharti ya Vifungu vya 11, 12, 14, 21, 23na 54 vya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai. Hali hii ilijidhihirisha kwa:
  • Kushindwa kueleza kosa analotuhumiwa nalo kwa uwazi wakati wa kukamatwa;
  • Kukamatwa bila hati halali ya kukamatwa;
  • Kunyimwa haki ya kuwasiliana na wakili wake, familia au watu wa karibu;
  • Kutumika kwa nguvu kupita kiasi, kinyume na sheria zinazopiga marufuku matumiziya nguvu za kuweza kusababisha kifo au madhara makubwa ya mwili.
  • MAPENDEKEZO YA TLS KUTOKANA NA TUKIO HILI
    Kutokana na ukiukwaji huu wa haki za kikatiba na kisheria, na kwa kuzingatia umuhimu wakulinda taaluma ya sheria na misingi ya demokrasia nchini, TLS imeazimia yafuatayo:
    i. Kulaani Kukamatwa Kinyume cha Sheria
    TLS inalaani vikali kukamatwa na kushikiliwa kwa Wakili Tundu A. Lissu kama ukiukwaji wahaki za kikatiba na tishio kwa utawala wa sheria na demokrasia nchini.
    ii. Kukuza Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Amani
    TLS inawahimiza wanasiasa wote na umma kwa ujumla kudumisha amani na kutatuamigogoro kwa njia zisizo za vurugu, hasa katika kipindi hiki muhimu kuelekea uchaguzi mkuu.
    iii. Wito wa Mageuzi ya Kisiasa na Kisheria
    TLS inatoa wito wa kufanyika kwa mageuzi ya kisiasa na kisheria kwa haraka ili kuhakikishaushiriki wa haki, jumuishi na wa kisheria katika mchakato wa kisiasa wa kitaifa, na hivyokuimarisha utulivu wa kidemokrasia.
    iv. Utekelezaji wa Sheria kwa Misingi ya Ushahidi
    Vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia ushahidi wa kweli nakufuata kikamilifu taratibu za kisheria, hasa katika kushughulikia masuala yanayohusuwanasiasa au wanataaluma wa sheria.
    v. Kuzuia Kujitokeza kwa Taharuki ya Kitaifa
    Kukamatwa kwa wanasiasa kinyume na sheria kunaweza kusababisha upinzani na machafuko.Mamlaka zinapaswa kuchukua hatua za kisheria na za tahadhari ili kudumisha amani na umojawa kitaifa, na kuepusha hali ya hofu miongoni mwa wanasiasa kuelekea uchaguzi mkuu.
    vi. Kukuza Mazungumzo Kati ya Vyama vya Siasa
    TLS inahimiza mazungumzo ya wazi na ya kujenga kati ya vyama vya siasa kama njia yakupunguza mvutano na kukuza mshikamano wa kitaifa.
    vii. Kuimarisha Uwezo wa Kisheria katika Ofisi za Umma
    TLS inapendekeza kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mamlaka za Mashtakazizingatie viwango vya juu vya umahiri na weledi wa kisheria, hasa katika kushughulikiamasuala yenye mvutano wa kisiasa.
  • viii. Uchambuzi wa Kina wa Mashtaka ya Uasi
    Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anatakiwa kuhakikisha kuwa mashtaka mazito kama ya uasiyanaungwa mkono na ushahidi madhubuti na hoja za kisheria. Uongozi wa kisiasa pekeehauwezi kuchukuliwa kuwa ni kitendo cha uasi kwa mujibu wa sheria zilizopo.
    ix. Kuachiwa Huru Mara Moja kwa Wakili Tundu A. Lissu
    TLS inatoa wito wa kuachiwa mara moja na bila masharti yoyote kwa Wakili Tundu A. Lissu.Kukamatwa kwake kunadhoofisha heshima ya taaluma ya sheria na misingi ya haki. Kuendeleakushikiliwa kwake kunaashiria vitisho kwa wanasheria na washiriki wa siasa nchini. Iwapo witohuu hautazingatiwa, TLS inahifadhi haki ya kupendekeza kusitishwa kwa huduma za uwakilishiwa kesi za msaada wa kisheria (dock brief) na huduma nyingine za kisheria za kujitoleazinazotolewa na TLS na wanachama wake, kama njia ya amani ya kupinga vitendo vyaunyanyasaji na mashtaka yenye mlengo wa kisiasa.
    WITO
    Chama cha Wanasheria Tanganyika kinathibitisha tena dhamira yake ya dhati katika kuteteaKatiba, haki za binadamu na utawala wa sheria. Tunazisihi mamlaka husika likiwemo Jeshi laPolisi, Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kutekeleza majukumu yao kwa haki, usawa nakufuata sheria, hasa katika kushughulikia masuala yanayohusu siasa na ushiriki wa umma.
    “Haki haipaswi tu kutendeka; bali ionekane dhahiri kuwa inatendeka.”
    Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Sheria Tanganyika
    Boniface A.K Mwabukusi

    Rais TLS

View attachment 3302773View attachment 3302774
View attachment 3302776
Paskali
 
TLS imeamka usingizini kitambo imewaacha mawakili wa jinsi yako msiojulikana mpo upande gani mmelala.
 
NASHAURI RAIS WETU AJITOFAUTISHE NA HAWA WALIOMKAMATA TUNDU. ATOE MSIMAMO WAKE KAMA SI MUHUSIKA
 
T. L. S inatakiwa kulinda utawala wa sheria, kwa mujibu wa sheria Mahakama ndiyo inaamua kesi, au kuna baadhi wako juu ya sheria?au mlitaka Lissu asipelekwe Mahakamani, Ila achapwe viboko hadharani tu?
 
Halafu hiyo hati ya uchaguzi angesaini nani wakati mwenyekiti nyupo kizuizini? Au walifanya makusudi?
 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya hivi karibuni, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetoa tamko kali na lisilo na kificho dhidi ya vyombo vya dola kufuatia kukamatwa kwa Wakili na Mwanasiasa maarufu Tundu Antipas Lissu. Katika taarifa ya kushtua iliyotolewa leo, TLS imetaja hatua hiyo kama “ukiukwaji wa wazi wa Katiba, sheria na misingi ya utawala wa sheria nchini”.

Kilio kutoka kwa Wanasheria: “Haki haipaswi tu kutendeka, bali ionekane dhahiri kuwa inatendeka”: TLS imedai kukamatwa kwa Lissu kumeambatana na ukiukwaji wa haki za msingi, ikiwemo:​
  1. Kukamatwa bila hati ya kisheria;
  2. Kunyimwa haki ya kuwasiliana na wakili wake au familia;
  3. Kutumiwa nguvu zisizo halali na vyombo vya usalama;
  4. Kufifisha uhuru wa kutoa maoni na ushiriki wa kisiasa.

Kilio cha Mageuzi: TLS yataka DPP ajitathmini juu ya mashtaka ya uasi
Katika hatua nyingine kali,:
TLS imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuacha kutumia mamlaka kwa misingi ya kisiasa. Imesisitiza kuwa uongozi wa kisiasa hauwezi kuchukuliwa kama kitendo cha uasi, na hivyo kuitaka Serikali kuheshimu uhuru wa kisiasa na misingi ya ushahidi wa kweli.

TLS Yafunguka: “Tupo tayari kusitisha huduma zote za msaada wa kisheria kama upinzani wa amani”: Katika tamko hilo lenye uzito mkubwa, TLS imetishia kusitisha huduma zake za uwakilishi wa “dock brief” na msaada wa kisheria kwa wananchi ikiwa wito wake wa kumwachia huru Tundu Lissu hautazingatiwa.

Je, nchi inaelekea wapi? Uchaguzi Mkuu unakaribia, joto linapanda Kwa kuzingatia kuwa Tanzania ipo kwenye kipindi nyeti kuelekea uchaguzi mkuu, TLS imeonya kuwa hatua kama hizi zinaweza kuchochea taharuki ya kitaifa. Imetoa wito kwa mazungumzo ya kisiasa, mageuzi ya kisheria, na weledi wa kitaaluma miongoni mwa taasisi za dola.

Habari hii inaendelea kuchafua upepo wa kisiasa nchini. Je, serikali itasikiliza kilio cha wanasheria? Je, TLS itatekeleza adhma zake za kuvunja kimya kwa vitendo zaidi?

#LissuAchiwe #TLSYasema #UtawalaWaSheria
View attachment 3301585​
View attachment 3301586
View attachment 3301587
Kila mwenye mapenzi mema hawezi kunyamazia unyama huu
 
Kwisha habari yenu sasa mmegeuka TEC mgombea wao wa uraisi anaitwa nani katibu wa hao TEC kasaini fomu ya maadili kama hajasaini ni kwishnei kama chadema!
Wachumia tumbo mmefurahi sana. Sasa mtu kama wewe unapata nini?
 
Tanzania ina uzoefu wa kuengua wagombea, tujifunze kupitia historia lakini wakati wote wale waliomuengua Tundu Lissu, Boniface Mwabukusi au CHADEMA walifeli katika njama zao zinazofadhiliwa kiaina na chama dola tawala

TOKA MAKTABA

23 Machi 2018

Wagombea Urais TLS wameshatajwa, Jina TUNDU LISSU halipo

View: https://m.youtube.com/watch?v=6MtM_7tEyYs

10 March 2017

Waziri Dr. Harrison Mwakyembe amenizuia kugombea urais wa TLS
1744545653707.jpeg

Tundu Lissu 2017

Chama cha Wanasheria Tanzania TLS kinatarajiwa kumchagua rais mpya wiki ijayo, lakini kumekuwa na mivutano hasa baada ya waziri wa katiba na sheria Dr. Harrison George Mwakyembe kusema chama hicho hakiwezi kujiingiza katika siasa. DW imezungumza na mchambuzi wa maswala ya sheria, mwanasheria Hussein Sengu kutafuta ufafanuzi juu ya kufunguliwa kesi mbili tofauti kuhusu uchaguzi huo.

Wakati huohuo

Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS), kimemwandiki barua Waziri Dkt. Mwakyembe kumtaka kutoingilia uchaguzi wa​

........

March 2017​

Rungwe amtaka Mwakyembe asiivuruge TLS​

Thursday , 16th Mar , 2017

Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe kuacha kuingilia mambo yanayohusu chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) hasa kwenye suala uchaguzi wa kumsaka Rais wa chama hicho
Mwakyembe%20na%20rungwe.JPG

Rungwe na Mwakyembe
Akijibu maswali ya wananchi kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa katika ukurasa wa Facebook EATV, Mh. Rungwe amesema kuwa TLS ina utaratibu wake wa kuendeshwa na kamwe haiwezi kupelekwa kama jinsi waziri anavyotaka kwani chama hicho kinaongozwa kwa sheria na kanuni.

“Yeye kama Waziri maoni yake ni muhimu, lakini anasema vijana hawa wawili wana maoni ya kisiasa yaani Lissu na mwenzake lakini wakati huo huo yeye ni waziri na mpaka amefika hapo yupo ndani ya chama cha kisiasa. na amevaa kofia mbili. TLS haiwezi kuendeshwa kama anavyotaka yeye, huwezi kutengeneza utaratibu nje ya utaratibu. Tuheshimu pia taaluma za watu." Rungwe alifunguka.

Aidha Rungwe ambaye pia ni Wakili wa Mahakama Kuu na Mwanachama wa chama hicho ameongeza kuwa katika chama hicho hakuna sheria ambayo inamzuia mwanasiasa yoyote kugombea nafasi na kuongeza kwamba kuwazuia upinzani wakati waliomo kwenye chama tawala wanaruhusiwa ni kutengeneza chuki ndani ya jamii na nchi kwa ujumla Hashim Rungwe
Lissu%20na%20Masha.jpg

Miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais wa TLS, Lawrence Masha (kushoto) na Tundu Lissu
"Kutengeneza chuki kwa makusudi it's a great crime, hasa chuki ikitengenezwa na viongozi waliopo madarakani, ambao wamepewa dhamana ya kuwaongoza wananchi yeye atuache na TLS yetu, kama itaonesha watu hawa hawaruhusiwi kugombea basi watazuiliwa kwasababu watu wanaochuja wagombea ni sisi wenyewe". Amesema.

Hivi karibuni Waziri huyo wa Sheria na Katiba alinukuliwa akisema kuwa serikali haiwezi kuona (TLS) kinajiingiza katika siasa na kuongeza kuwa kama wanataka hivyo, basi serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha wanasheria...
 
Back
Top Bottom