TLS Yatoa Tamko Kulaani Ukamataji Holela wa Viongozi wa Siasa, Wanaharakati na Makundi ya Kiraia , na Kuonya Kuhusu Hatari ya Kuvuruga Amani ya Taifa

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318

View: https://youtu.be/FfitG5qRW2M?si=HcUhPfFnt9Wh7XCX

Katika taarifa iliyojaa msisitizo na ufundi wa kisheria, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu mwenendo wa jeshi la polisi katika kukamata viongozi wa kisiasa, mawakili, waandishi wa habari, na wanaharakati, hasa kutoka mikoa ya Iringa na Mbeya. TLS imetoa wito kwa mamlaka husika kuheshimu haki za kikatiba za kujieleza, kukusanyika, na kujumuika, huku ikilaani vikali hatua za jeshi la polisi ambazo zinaonekana kulenga kuzima sauti za wapinzani na makundi ya kiraia.​

PIA SOMA: Thread 'Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa'

TLS imesema kuwa matukio haya ni ukiukwaji wa wazi wa Ibara ya 18 na 20(1) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatoa uhuru wa kujieleza na kujumuika. Chama hiki pia kimebaini kuwa vitendo hivi vinaweza kuzua rabsha na hasira miongoni mwa raia, hali inayoweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi.

Baraza la Uongozi la TLS limeelekeza kuwa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya maafisa wote wa polisi waliohusika katika ukiukwaji huu, kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji na matumizi bora ya madaraka katika ofisi za umma. Kwa kuongezea, TLS imesisitiza umuhimu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake bila upendeleo, ili kujenga imani miongoni mwa Watanzania.

Tamko hili limekuja wakati ambapo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikihimiza maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko, na ujenzi mpya wa taifa (4Rs). Hata hivyo, TLS inaona kuwa matukio ya hivi karibuni yanatishia juhudi hizo na kupunguza imani ya umma kwa serikalipia imeweka wazi kuwa wataendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya hali hii na kutoa msaada wa kisheria kwa wote waliokamatwa kwa mujibu wa sheria za TLS.

TAMKO 👇🏼
IMG_5843.jpeg

IMG_5844.jpeg

IMG_5845.jpeg

12 Aug 2024
TAARIFA KWA UMMA
KULAANI UKAMATAJI WA MAKUNDI YA KIRAIA KWA LENGO LA KUMINYA UHURU WA KUJUMUIKA NA KUJIELEZA
.​

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinalaani kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa hususan Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mawakili, waandishi wa habari waliokuwa wakitekeleza majukumu yao na wanaharakati mbalimbali kulikofanywa na Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Iringa na Mbeya. TLS imebaini kuwepo kwa kamata kamata iliyo kinyume cha sheria kwa siku za karibuni yenye lengo la kuyanyima makundi hayo haki yao ya msingi na ya Kikatiba ya uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kujumuika.

Aidha, katika siku za hivi karibuni kumeibuka Utekelezaji na usimamizi wa sheria unaofanywa na vyombo vyenye wajibu huo kwa misingi yenye viashiria vya ubaguzi au tafsiri inayoashiria upendeleo na ubaguzi kwa baadhi ya watu, hasa wanapotoa Matamko ya Kisiasa. Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imekuwa na Uzito mkubwa katika kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika hasa pale zinapotolewa kauli zenye viashiria vya uhalifu kutoka kwa upande wa viongozi wa Chama Tawala.

Ibara ya 18 na 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatoa haki na uhuru wa watu kujieleza, kukusanyika na kujumuika. Haki hizi zimelindwa pia kwenye Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda ambayo Tanzania imeiridhia na hivyo ina wajibu wa kuziheshimu na kuzitekeleza ipasavyo.

TLS inasikitishwa na ukiukwaji huu wa Katiba na ukamatwaji huu unaoendelea ambao unafifisha uhalisia wa 4Rs (Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding) za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa tafsiri ya maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya ambazo zimekuwa kauli mbiu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu alipoingia madarakani.

Viongozi wa kisiasa, mawakili, waandishi wa habari na wanaharakati wanayo haki ya kujieleza, kukusanyika na kujumuika. Vitendo vya kuwazuia na kuwakamata kama ilivyofanyika kwenye maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na Morogoro na kuwazuia wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa ACT Wazalendo (Dar es Salaam) vilivyofanyika tarehe 10,11 na 12 Agosti 2024 ni ukiukwaji wa wazi wa Katiba na sheria tulizojiwekea kama watanzania.

Ukiukwaji huu wa haki ya kujumuika au usimamizi wa kibaguzi wa sheria kuhusiana na haki ya kujumuika kunaweza kuzua rabsha na hasira miongoni mwa makundi hayo inayoweza kupelekea kuhatarisha amani ya nchi au madhara makubwa zaidi ya hayo kama ilivyoweza kutokea katika nchi zingine hivi karibuni.

TLS inatoa wito na kulisihi Jeshi la Polisi nchini, kuheshimu utawala wa sheria na mara zote lijielekeze katika kulinda raia na mali zao na kuacha kuingilia shughuli za vyama vya siasa ambazo kimsingi zinaongozwa na sheria ya vyama vya Siasa (Political Parties Act Cap 258 R.E 2002). Hivyobasi, tunalisihi Jeshi la Polisi kuacha mara moja matendo yenye kuashiria uminyaji wa haki ya kujumuika na kujieleza jambo ambalo ni uvunjwaji wa Katiba na sheria za Nchi.

Tunavitaka vyombo vya usalama hususan Jeshi la Polisi viimarishe uwezo wao wa kulinda makundi haya wakati yanapotaka kutumia haki zao za Kikatiba katika shughuli zao kwa mujibu wa taratibu na sheria zetu na watambue kwamba wajibu wao ni kutoa Ulinzi na kama kuna viashiria vya uhalifu wavidhibiti na siyo kuzuia vyama au makundi ya kiraia kujumuika kwasababu za kiujumla zisizo na maelezo yanayojitosheleza.

TLS imepitia maelezo ya Jeshi la Polisi na vilevile imepitia maelezo ya kile kinacholalamikiwa kuwa kauli yenye kuhatarisha usalama na kufikia hitimisho kwamba hakukuwa na sababu yeyote ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kama ilivyofanya kwani kauli zile zilikuwa za kiujumla na za kisiasa zisizokuwa na viashiria au uthibitisho wa uhalifu ndani yake na kwa msingi huo, tunataka kuachiwa mara moja bila masharti yeyote wote waliokamatwa kwa kutekeleza haki yao ya kikatiba na kwamba kuendelea kuwashikilia ni kukiuka Katiba na sheria za nchi.

TLS kupitia Kamati maalum ya mawakili imeelekeza kufanyika tathmini na kuchukuliwa kwa hatua stahiki za kisheria kwa kila Afisa aliyehusika kusababisha kadhia hii kwa jina lake na kuhakikisha utii na uzingatiwaji wa matumizi bora ya madaraka katika Ofisi za Umma.

TLS inatoa wito pia kwa viongozi wengine wa nchi na wa kisiasa, kuacha mara moja kutoa matamko au matamshi ambayo yanaweza kuleta taharuki katika jamii na kuchochea hasira au malalamiko kutoka makundi mengine ya jamii ambayo hayakubaliani na matamko au matamshi hayo. Hii itasaidia kuongeza amani, utulivu na utekelezaji wa Katiba na Sheria zetu kwa mujibu wa taratibu tulizojiwekea kama Watanzania.

TLS inatoa wito pia kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi yake kwa mujibu wa Katib ana Sheria bila upendeleo wowote. Hii itajenga imani kwa jamii kwamba Ofisi hii ipo kwa dhati kabisa kwa masilahi ya vyama vyote vya siasa nchini.

TLS inaendelea kufuatilia vitendo hivi kwa ukaribu kwa kushirikiana na wanachama wetu katika maeneo husika ili kubaini na kuamua hatua stahiki za kuchukua ili kuwapa msaada wa kisheria watu wote waliokamatwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002).​

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Boniface A.K Mwabukusi Rais​
 
Tukio la kushikiliwa na kupigwa kwa viongozi wa chadema limeendelea kugonga vichwa vya habari dunia ambapo ukiacha TLs ambao wao leo wameweka wazi kuwa wanajipanga kuwashitaki wahusika wa uhalifu huu kwa majina yao na sio vyeo vya TLS

Hata hivyo TLS imesema wazi kuwa hakuna kosa wala sheria yeyote ile iliyovunjwa na watanzania hao ambao walikuwa wanatekeleza haki zao za kikatiba!

Pia Shirika la democract union of Africa limelaani na kutaka kuachiwa mara moja viongozi hao
Pia IDU -international democratic Union limelaani vitendo vinavyo endelea nchini kwa ni kinyume na demokrasia

Matamko yao
…………….
 
Attachments

  • IMG_2806.jpeg
    IMG_2806.jpeg
    599.8 KB · Views: 4
  • IMG_2805.jpeg
    IMG_2805.jpeg
    613.6 KB · Views: 2
  • IMG_2807.jpeg
    IMG_2807.jpeg
    319.4 KB · Views: 3
  • IMG_2811.jpeg
    IMG_2811.jpeg
    1.4 MB · Views: 1

Tamko murua kabisa
 
Chama kongwe dola kinakemewa na dunia nzima, CCM imekuwa shetani kwa kukemewa, kulaaniwa na ulimwengu wote. Hakika CCM imefikia tamati ya safari yake ndefu ya kisiasa ya miaka 70 (Kuasisiwa mwaka 1954 - kupumzishwa RIP 2024)
 
Kuna washikaji zangu walikuwa hawasikii wa kuambiwa kuhusu huyu mama....yaani ni mama mama mama....sasa hivi wamenywea sana, wanaanza kumchukia.
 
Tukio la kushikiliwa na kupigwa kwa viongozi wa chadema limeendelea kugonga vichwa vya habari dunia ambapo ukiacha TLs ambao wao leo wameweka wazi kuwa wanajipanga kuwashitaki wahusika wa uhalifu huu kwa majina yao na sio vyeo vya TLS

Hata hivyo TLS imesema wazi kuwa hakuna kosa wala sheria yeyote ile iliyovunjwa na watanzania hao ambao walikuwa wanatekeleza haki zao za kikatiba!

Pia Shirika la democract union of Africa limelaani na kutaka kuachiwa mara moja viongozi hao
Pia IDU -international democratic Union limelaani vitendo vinavyo endelea nchini kwa ni kinyume na demokrasia

Matamko yao
…………….
Viongozi wa dini, kimya!
 
Hii ndiyo sababu ya Emmanuel Nchimbi kutaka WanaChadema waachiwe kwa upuuzi wa Policcm ingawa dhahiri walitumwa, kuwa sasa wanaanza kulaniwa Dunia nzima.

NB; Ziara na mialiko kwa bimkubwa zitapungua kwa udikteta huu.
 
Tukio la kushikiliwa na kupigwa kwa viongozi wa chadema limeendelea kugonga vichwa

Hili lilikuwa jaribio la kuteka watu 520 kwa mpigo, walianza mmoja mmoja 2020 - 2023, sasa Chama kongwe kimeamua kufanya utekaji wa halaiki ya watu wa mamia .
 
CCM pia kupitia Katibu Mkuu, kachukizwa kabisa, hatupendi kabisa fyoko fyoko za kisiasa
 
View: https://youtu.be/FfitG5qRW2M?si=HcUhPfFnt9Wh7XCX

Katika taarifa iliyojaa msisitizo na ufundi wa kisheria, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu mwenendo wa jeshi la polisi katika kukamata viongozi wa kisiasa, mawakili, waandishi wa habari, na wanaharakati, hasa kutoka mikoa ya Iringa na Mbeya. TLS imetoa wito kwa mamlaka husika kuheshimu haki za kikatiba za kujieleza, kukusanyika, na kujumuika, huku ikilaani vikali hatua za jeshi la polisi ambazo zinaonekana kulenga kuzima sauti za wapinzani na makundi ya kiraia.​

PIA SOMA: Thread 'Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa'

TLS imesema kuwa matukio haya ni ukiukwaji wa wazi wa Ibara ya 18 na 20(1) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatoa uhuru wa kujieleza na kujumuika. Chama hiki pia kimebaini kuwa vitendo hivi vinaweza kuzua rabsha na hasira miongoni mwa raia, hali inayoweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi.

Baraza la Uongozi la TLS limeelekeza kuwa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya maafisa wote wa polisi waliohusika katika ukiukwaji huu, kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji na matumizi bora ya madaraka katika ofisi za umma. Kwa kuongezea, TLS imesisitiza umuhimu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yake bila upendeleo, ili kujenga imani miongoni mwa Watanzania.

Tamko hili limekuja wakati ambapo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikihimiza maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko, na ujenzi mpya wa taifa (4Rs). Hata hivyo, TLS inaona kuwa matukio ya hivi karibuni yanatishia juhudi hizo na kupunguza imani ya umma kwa serikalipia imeweka wazi kuwa wataendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya hali hii na kutoa msaada wa kisheria kwa wote waliokamatwa kwa mujibu wa sheria za TLS.

TAMKO 👇🏼

12 Aug 2024
TAARIFA KWA UMMA
KULAANI UKAMATAJI WA MAKUNDI YA KIRAIA KWA LENGO LA KUMINYA UHURU WA KUJUMUIKA NA KUJIELEZA
.​

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinalaani kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa hususan Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mawakili, waandishi wa habari waliokuwa wakitekeleza majukumu yao na wanaharakati mbalimbali kulikofanywa na Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Iringa na Mbeya. TLS imebaini kuwepo kwa kamata kamata iliyo kinyume cha sheria kwa siku za karibuni yenye lengo la kuyanyima makundi hayo haki yao ya msingi na ya Kikatiba ya uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kujumuika.

Aidha, katika siku za hivi karibuni kumeibuka Utekelezaji na usimamizi wa sheria unaofanywa na vyombo vyenye wajibu huo kwa misingi yenye viashiria vya ubaguzi au tafsiri inayoashiria upendeleo na ubaguzi kwa baadhi ya watu, hasa wanapotoa Matamko ya Kisiasa. Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imekuwa na Uzito mkubwa katika kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika hasa pale zinapotolewa kauli zenye viashiria vya uhalifu kutoka kwa upande wa viongozi wa Chama Tawala.

Ibara ya 18 na 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatoa haki na uhuru wa watu kujieleza, kukusanyika na kujumuika. Haki hizi zimelindwa pia kwenye Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda ambayo Tanzania imeiridhia na hivyo ina wajibu wa kuziheshimu na kuzitekeleza ipasavyo.

TLS inasikitishwa na ukiukwaji huu wa Katiba na ukamatwaji huu unaoendelea ambao unafifisha uhalisia wa 4Rs (Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding) za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa tafsiri ya maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya ambazo zimekuwa kauli mbiu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu alipoingia madarakani.

Viongozi wa kisiasa, mawakili, waandishi wa habari na wanaharakati wanayo haki ya kujieleza, kukusanyika na kujumuika. Vitendo vya kuwazuia na kuwakamata kama ilivyofanyika kwenye maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na Morogoro na kuwazuia wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa ACT Wazalendo (Dar es Salaam) vilivyofanyika tarehe 10,11 na 12 Agosti 2024 ni ukiukwaji wa wazi wa Katiba na sheria tulizojiwekea kama watanzania.

Ukiukwaji huu wa haki ya kujumuika au usimamizi wa kibaguzi wa sheria kuhusiana na haki ya kujumuika kunaweza kuzua rabsha na hasira miongoni mwa makundi hayo inayoweza kupelekea kuhatarisha amani ya nchi au madhara makubwa zaidi ya hayo kama ilivyoweza kutokea katika nchi zingine hivi karibuni.

TLS inatoa wito na kulisihi Jeshi la Polisi nchini, kuheshimu utawala wa sheria na mara zote lijielekeze katika kulinda raia na mali zao na kuacha kuingilia shughuli za vyama vya siasa ambazo kimsingi zinaongozwa na sheria ya vyama vya Siasa (Political Parties Act Cap 258 R.E 2002). Hivyobasi, tunalisihi Jeshi la Polisi kuacha mara moja matendo yenye kuashiria uminyaji wa haki ya kujumuika na kujieleza jambo ambalo ni uvunjwaji wa Katiba na sheria za Nchi.

Tunavitaka vyombo vya usalama hususan Jeshi la Polisi viimarishe uwezo wao wa kulinda makundi haya wakati yanapotaka kutumia haki zao za Kikatiba katika shughuli zao kwa mujibu wa taratibu na sheria zetu na watambue kwamba wajibu wao ni kutoa Ulinzi na kama kuna viashiria vya uhalifu wavidhibiti na siyo kuzuia vyama au makundi ya kiraia kujumuika kwasababu za kiujumla zisizo na maelezo yanayojitosheleza.

TLS imepitia maelezo ya Jeshi la Polisi na vilevile imepitia maelezo ya kile kinacholalamikiwa kuwa kauli yenye kuhatarisha usalama na kufikia hitimisho kwamba hakukuwa na sababu yeyote ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kama ilivyofanya kwani kauli zile zilikuwa za kiujumla na za kisiasa zisizokuwa na viashiria au uthibitisho wa uhalifu ndani yake na kwa msingi huo, tunataka kuachiwa mara moja bila masharti yeyote wote waliokamatwa kwa kutekeleza haki yao ya kikatiba na kwamba kuendelea kuwashikilia ni kukiuka Katiba na sheria za nchi.

TLS kupitia Kamati maalum ya mawakili imeelekeza kufanyika tathmini na kuchukuliwa kwa hatua stahiki za kisheria kwa kila Afisa aliyehusika kusababisha kadhia hii kwa jina lake na kuhakikisha utii na uzingatiwaji wa matumizi bora ya madaraka katika Ofisi za Umma.

TLS inatoa wito pia kwa viongozi wengine wa nchi na wa kisiasa, kuacha mara moja kutoa matamko au matamshi ambayo yanaweza kuleta taharuki katika jamii na kuchochea hasira au malalamiko kutoka makundi mengine ya jamii ambayo hayakubaliani na matamko au matamshi hayo. Hii itasaidia kuongeza amani, utulivu na utekelezaji wa Katiba na Sheria zetu kwa mujibu wa taratibu tulizojiwekea kama Watanzania.

TLS inatoa wito pia kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi yake kwa mujibu wa Katib ana Sheria bila upendeleo wowote. Hii itajenga imani kwa jamii kwamba Ofisi hii ipo kwa dhati kabisa kwa masilahi ya vyama vyote vya siasa nchini.

TLS inaendelea kufuatilia vitendo hivi kwa ukaribu kwa kushirikiana na wanachama wetu katika maeneo husika ili kubaini na kuamua hatua stahiki za kuchukua ili kuwapa msaada wa kisheria watu wote waliokamatwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002).​

Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Boniface A.K Mwabukusi Rais​

TLS inayoongozwa na Mwanachama wa CDM, Mwabukusi haina la maana kwa sasa kwa kuwa ni tawi la Chama cha CDM.
 
Boniface A.K Mwabukusi Rai​

Wanabeep halafu wanalia?
Wakaushe tu
 
Back
Top Bottom