TMA: Hatujawahi kusema kuna Mvua za El-nino, wanaosema hivyo Wanapotosha

TMA: Hatujawahi kusema kuna Mvua za El-nino, wanaosema hivyo Wanapotosha

  1. PMO | Mwanzo
  2. Habari

Habari​

Serikali yatoa maelekezo 13 kukabiliana na El-Nino​


a4a197b876075320a90447abe3b4de6e

SERIKALI imetoa maelekezo 13 kwa umma, kamati za usimamizi wa maafa, Wizara, Taasisi, Mikoa, Halmashauri na sekta mbalimbali nchini, kwa ajili ya kujiandaa na kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino.

Imeelekeza maeneo yote hatarishi yatambuliwe mapema, tathmini za vihatarishi zifanyike na hatua stahiki zichukuliwe, ikiwemo kuwahamasisha wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi na kwenda maeneo salama.

Maelekezo hayo yametolewa hii leo (02 Septemba,2026) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-Nino.

Profesa Kabudi amesema Serikali imeelekeza kuhakikisha mvua hizo zinatumika kikamilifu kwa shughuli za uzalishaji, ikiwemo kilimo, ufugaji, uvunaji wa maji na uvuvi.

Aidha, amesisitiza wananchi wanapaswa kuelimishwa na kuhimizwa kuchukua hatua za kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo, ikiwemo kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo salama, kuweka akiba ya chakula, kutumia mbinu bora za kilimo na kuchagua mazao pamoja na mbegu bora kwa msimu wa Vuli.

“Kuandaa rasilimali kwa ajili ya kuzuia au kupunguza madhara, kujiandaa na kukabiliana na maafa yatakayotokea na kushirikisha wadau wote wa maafa, wakiwemo wananchi, taasisi na sekta binafsi katika maeneo yao,” amesema.

Ameongeza kuwa: “Serikali imeagiza kuandaliwa na kutekelezwa kwa mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kwa binadamu, wanyama na mimea.”

Profesa Kabudi amesema Wizara, Taasisi, Mikoa na wadau wengine wanaohusika na miundombinu wanapaswa kufanya ukaguzi wa miundombinu muhimu na kuhakikisha inaimarishwa na kusafishwa, ikiwemo madaraja, makaravati na mitaro.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu kabla, wakati na baada ya maafa kutokea, zikiwemo huduma za usafirishaji, maji na umeme.

Serikali pia imeagiza kuimarishwa kwa usimamizi wa mazingira, ikiwemo udhibiti wa taka ngumu, usafishaji na uimarishaji wa njia za maji, kingo za mito na mabwawa.

Aidha, imeelekeza kuhakikisha vifaa vya uokoaji, huduma za dharura na mifumo ya mawasiliano vinapatikana na kuwa katika hali ya utayari wakati wote.

Katika hatua nyingine, Serikali imeagiza kubainisha na kutenga maeneo salama yatakayotumika kwa ajili ya makazi ya dharura pindi maafa yatakapotokea.

Kwa upande wa sekta ya utalii, Serikali imeagiza kufanyika kwa ukaguzi na ukarabati wa miundombinu iliyopo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Jamii ili kuhakikisha shughuli za utalii zinaendelea wakati wote.

“Wizara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri zote zimeagizwa kufuatilia na kuzingatia maelekezo ya kitaalamu pamoja na taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ili hatua stahiki za kujiandaa na kukabiliana na madhara ya El-Nino zichukuliwe kwa wakati.”

KUHUSU BILIONI 730

Akizungumzia taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu makadirio ya matumizi ya Sh. bilioni 730 katika kujiandaa na kukabiliana na El-Niño, Profesa Kabudi amesema taarifa hiyo haikutoa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli zilizoainishwa katika mpango huo.

Amesema Sh. bilioni 730 ni makadirio ya fedha zinazohitajika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-Niño kabla, wakati na baada ya El-Nino kutokea.

“Kwa mujibu wa Mpango, makadirio ya fedha zinazohitajika kutumika katika kutekeleza Mpango huo ni Sh. bilioni 730,” amesema.

Hata hivyo, amesema fedha zilizotengwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hizo katika sekta zote ni Sh. bilioni 10.

Chanzo cha hii habari:
Halafu watu wa aina hiyo wanakuambia wana dira ya taifa ya 2025-2050. Kama wameshindwa kutabiri tukio la muda mfupi hivi, wanawezaje kupanga hayo ya muda mrefu hivyo? ChoiceVariable njoo chawa unayejifanya una data utetee huu upuuzi, maana ule wa kura 31m unauonea aibu. RoDrick RaY
 
Huyo Jamaa kitaalamu Yuko sahihi kabisa lakini ni vile Tu Sisi ni vichwa panzi akili ndogo, Ukija hata Kwa viongozi wetu ni vichwa maji, wakisimama majukwaani Utasikia mvua za el nino blah blah...Wananchi walipaswa kueleweshwa vizuri kuanzia ngazi za chini kabisa na sio kutishwa tishwa hovyo na viongozi majukwaani....jamani Sisi bado Sana akili VISODA kabisa.
 
Mamlaka ya ya hali ya hewa Tanzania(TMA) , imesema haijawahi kutangazia Umma kwamba kuna Mvua za El-nino.

Akiongea na Wasafi FM, Dkt. Mafuru Kantamla Meneja Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amesema wanaosema mvua za El-nino wanapotosha.

Kasema hivi, Namnukuu, "El-nino ni ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki la bahari ya Pasifiki. Lakini madhara yake ni madogo madogo kutokana na sehemu ulipo. Unajua tunakosea tunaposema mvua za El-nino, hilo ni kosa kubwa". Mwisho wa kunukuu

Amedai kwamba walisema kuna El nino si mvua ya El nino kwani El nino ilishaanza Tangu mei na itadumu kipindi kirefu 2027

TMA wamesema El nino ni hali ya hewa kutokana na sehemu. Sehemu zinginezo panawaka jua la El nino.

MY TAKE;
Mafisadi na Wala nchi ya CCM ndo walitia watu hofu ili wakope hela kwenye taasisi za kimataifa. Wamepewa hela wakagawana watu na Msoga rufiji na Zanzibar. Hela zimeisha na Miradi ya maendeleo imesimama. Kumbuka Serikali ya Tanzania ilitenga Bilioni 700 za kupambana na mvua kubwa za El nino. Walidai ni za kukarabati madaraja na kuzibua mifereji na zimeshaisha bila kufanyika chochote.

Kumbuka watu wamebomolewa nyumba zao kwamba nyumba zimeziba njia ya maji ya mvua za El - nino.
View attachment 3695977
Kwahiyo zile picha zilikua famba?
 
Mamlaka ya ya hali ya hewa Tanzania(TMA) , imesema haijawahi kutangazia Umma kwamba kuna Mvua za El-nino.

Akiongea na Wasafi FM, Dkt. Mafuru Kantamla Meneja Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amesema wanaosema mvua za El-nino wanapotosha.

Kasema hivi, Namnukuu, "El-nino ni ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki la bahari ya Pasifiki. Lakini madhara yake ni madogo madogo kutokana na sehemu ulipo. Unajua tunakosea tunaposema mvua za El-nino, hilo ni kosa kubwa". Mwisho wa kunukuu

Amedai kwamba walisema kuna El nino si mvua ya El nino kwani El nino ilishaanza Tangu mei na itadumu kipindi kirefu 2027

TMA wamesema El nino ni hali ya hewa kutokana na sehemu. Sehemu zinginezo panawaka jua la El nino.

MY TAKE;
Mafisadi na Wala nchi ya CCM ndo walitia watu hofu ili wakope hela kwenye taasisi za kimataifa. Wamepewa hela wakagawana watu na Msoga rufiji na Zanzibar. Hela zimeisha na Miradi ya maendeleo imesimama. Kumbuka Serikali ya Tanzania ilitenga Bilioni 730 za kupambana na mvua kubwa za El nino. Walidai ni za kukarabati madaraja na kuzibua mifereji na zimeshaisha bila kufanyika chochote.

Watu wamebomolewa nyumba zao kwamba nyumba zimeziba njia ya maji ya mvua za El - nino.
View attachment 3695977
Mabilion ya elnino sasa ,sijui inakuwaje?
 
Safi sana Maana Ma CHADEMA yalijua kuna mvua za El Nini ili yaanze kulala ndani bila kufanya kazi 😄😄
 
Huyo Jamaa kitaalamu Yuko sahihi kabisa lakini ni vile Tu Sisi ni vichwa panzi akili ndogo, Ukija hata Kwa viongozi wetu ni vichwa maji, wakisimama majukwaani Utasikia mvua za el nino blah blah...Wananchi walipaswa kueleweshwa vizuri kuanzia ngazi za chini kabisa na sio kutishwa tishwa hovyo na viongozi majukwaani....jamani Sisi bado Sana akili VISODA kabisa.
Wananchi wanapaswa kueleweshwa nini? Wizara ya elimu ni serekali hiyo, kwanini hao TMA hawakuwafuata na kuwaelisha kuwa Elinino sio mvua tu, hadi wakabadili ratiba za mitihani, na kufunga shule kuhofua mvua ya elinino. Acha jazba na kucheza naaneno.
 
Ukitaka kuamini kuwa UVCCM na CCM yote kwa ujumla kuwa wengi ni Vichaa na hawana hoja za msingi katika maendeleo ya taifa huwezi kumkuta hapa Tlaatlaah Wala Lucas Mwashambwa Yani wao utawakuta kwenye zile nyuzi zao za porojo kuhusu CHADEMA
Hapa hata Paschal Mayala au Robert Herieth Mtibeli huwezi kuwakuta. Imagine Mayala ni team Makonda, unatajia atie neno hapa? Uchawa ni janga jipya nchi hii.
 
"Mojawapo ya adhabu za kukataa kushiriki katika siasa ni kuishia kutawaliwa na watu walio chini yako kwa uwezo au uelewa".
Plato....

Binafsi natamani kuondoka hapa nchini
Watu wenye akili timamu ni ngumu sana kuishi hapa.
 
Tatizo mpaka sasa hivi taarifa zinaonesha El Nino + Positive Indian Ocean Dipole. Hii kitu ni mvua kwa upande wa East Africa.

Kinachosababisha mvua hakuna (hali ya ukame) ni Madden-Julian Oscillation ambayo ipo Phase 2. Ni temporary atmospheric disturbance ndiyo inapelekea suppression ya warm air & delay in cloud formation. Ikienda Phase 4 tutegee mzigo wa mvua kushuka wa maana.

Tusubiri November - December
 
Back
Top Bottom