We ndo hujielewi babu. Sijui huko shule ulikua unaelewaje. Huku mtaani mifereji imefukuliwa sana na pia shule zinafungwa .apema mwaka huu kwa sababu ya mvua kubwa za elninyo kwa tangazo la TMAEl nino sio mvua tu ata ongezeko la joto nadhani shida na uelewa wa wananchi na sio TMA
Halafu watu wa aina hiyo wanakuambia wana dira ya taifa ya 2025-2050. Kama wameshindwa kutabiri tukio la muda mfupi hivi, wanawezaje kupanga hayo ya muda mrefu hivyo? ChoiceVariable njoo chawa unayejifanya una data utetee huu upuuzi, maana ule wa kura 31m unauonea aibu. RoDrick RaY
- PMO | Mwanzo
- Habari
Habari
Serikali yatoa maelekezo 13 kukabiliana na El-Nino
SERIKALI imetoa maelekezo 13 kwa umma, kamati za usimamizi wa maafa, Wizara, Taasisi, Mikoa, Halmashauri na sekta mbalimbali nchini, kwa ajili ya kujiandaa na kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino.
Imeelekeza maeneo yote hatarishi yatambuliwe mapema, tathmini za vihatarishi zifanyike na hatua stahiki zichukuliwe, ikiwemo kuwahamasisha wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi na kwenda maeneo salama.
Maelekezo hayo yametolewa hii leo (02 Septemba,2026) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-Nino.
Profesa Kabudi amesema Serikali imeelekeza kuhakikisha mvua hizo zinatumika kikamilifu kwa shughuli za uzalishaji, ikiwemo kilimo, ufugaji, uvunaji wa maji na uvuvi.
Aidha, amesisitiza wananchi wanapaswa kuelimishwa na kuhimizwa kuchukua hatua za kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo, ikiwemo kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo salama, kuweka akiba ya chakula, kutumia mbinu bora za kilimo na kuchagua mazao pamoja na mbegu bora kwa msimu wa Vuli.
βKuandaa rasilimali kwa ajili ya kuzuia au kupunguza madhara, kujiandaa na kukabiliana na maafa yatakayotokea na kushirikisha wadau wote wa maafa, wakiwemo wananchi, taasisi na sekta binafsi katika maeneo yao,β amesema.
Ameongeza kuwa: βSerikali imeagiza kuandaliwa na kutekelezwa kwa mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kwa binadamu, wanyama na mimea.β
Profesa Kabudi amesema Wizara, Taasisi, Mikoa na wadau wengine wanaohusika na miundombinu wanapaswa kufanya ukaguzi wa miundombinu muhimu na kuhakikisha inaimarishwa na kusafishwa, ikiwemo madaraja, makaravati na mitaro.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu kabla, wakati na baada ya maafa kutokea, zikiwemo huduma za usafirishaji, maji na umeme.
Serikali pia imeagiza kuimarishwa kwa usimamizi wa mazingira, ikiwemo udhibiti wa taka ngumu, usafishaji na uimarishaji wa njia za maji, kingo za mito na mabwawa.
Aidha, imeelekeza kuhakikisha vifaa vya uokoaji, huduma za dharura na mifumo ya mawasiliano vinapatikana na kuwa katika hali ya utayari wakati wote.
Katika hatua nyingine, Serikali imeagiza kubainisha na kutenga maeneo salama yatakayotumika kwa ajili ya makazi ya dharura pindi maafa yatakapotokea.
Kwa upande wa sekta ya utalii, Serikali imeagiza kufanyika kwa ukaguzi na ukarabati wa miundombinu iliyopo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Jamii ili kuhakikisha shughuli za utalii zinaendelea wakati wote.
βWizara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri zote zimeagizwa kufuatilia na kuzingatia maelekezo ya kitaalamu pamoja na taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ili hatua stahiki za kujiandaa na kukabiliana na madhara ya El-Nino zichukuliwe kwa wakati.β
KUHUSU BILIONI 730
Akizungumzia taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu makadirio ya matumizi ya Sh. bilioni 730 katika kujiandaa na kukabiliana na El-NiΓ±o, Profesa Kabudi amesema taarifa hiyo haikutoa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli zilizoainishwa katika mpango huo.
Amesema Sh. bilioni 730 ni makadirio ya fedha zinazohitajika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-NiΓ±o kabla, wakati na baada ya El-Nino kutokea.
βKwa mujibu wa Mpango, makadirio ya fedha zinazohitajika kutumika katika kutekeleza Mpango huo ni Sh. bilioni 730,β amesema.
Hata hivyo, amesema fedha zilizotengwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hizo katika sekta zote ni Sh. bilioni 10.
Chanzo cha hii habari:
Kwahiyo zile picha zilikua famba?Mamlaka ya ya hali ya hewa Tanzania(TMA) , imesema haijawahi kutangazia Umma kwamba kuna Mvua za El-nino.
Akiongea na Wasafi FM, Dkt. Mafuru Kantamla Meneja Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amesema wanaosema mvua za El-nino wanapotosha.
Kasema hivi, Namnukuu, "El-nino ni ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki la bahari ya Pasifiki. Lakini madhara yake ni madogo madogo kutokana na sehemu ulipo. Unajua tunakosea tunaposema mvua za El-nino, hilo ni kosa kubwa". Mwisho wa kunukuu
Amedai kwamba walisema kuna El nino si mvua ya El nino kwani El nino ilishaanza Tangu mei na itadumu kipindi kirefu 2027
TMA wamesema El nino ni hali ya hewa kutokana na sehemu. Sehemu zinginezo panawaka jua la El nino.
MY TAKE;
Mafisadi na Wala nchi ya CCM ndo walitia watu hofu ili wakope hela kwenye taasisi za kimataifa. Wamepewa hela wakagawana watu na Msoga rufiji na Zanzibar. Hela zimeisha na Miradi ya maendeleo imesimama. Kumbuka Serikali ya Tanzania ilitenga Bilioni 700 za kupambana na mvua kubwa za El nino. Walidai ni za kukarabati madaraja na kuzibua mifereji na zimeshaisha bila kufanyika chochote.
Kumbuka watu wamebomolewa nyumba zao kwamba nyumba zimeziba njia ya maji ya mvua za El - nino.
View attachment 3695977
Kwa hiyo wananchi kwa kukosa uelewa ndio waliamua kufunga shule, kuhama mabondeni, kupanua madaraja? Au TMA ndio hawatoi ufafanuzi wa kueleweka kwa taarifa za tabiri zao?El nino sio mvua tu ata ongezeko la joto nadhani shida na uelewa wa wananchi na sio TMA
Mabilion ya elnino sasa ,sijui inakuwaje?Mamlaka ya ya hali ya hewa Tanzania(TMA) , imesema haijawahi kutangazia Umma kwamba kuna Mvua za El-nino.
Akiongea na Wasafi FM, Dkt. Mafuru Kantamla Meneja Ofisi Kuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) amesema wanaosema mvua za El-nino wanapotosha.
Kasema hivi, Namnukuu, "El-nino ni ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki la bahari ya Pasifiki. Lakini madhara yake ni madogo madogo kutokana na sehemu ulipo. Unajua tunakosea tunaposema mvua za El-nino, hilo ni kosa kubwa". Mwisho wa kunukuu
Amedai kwamba walisema kuna El nino si mvua ya El nino kwani El nino ilishaanza Tangu mei na itadumu kipindi kirefu 2027
TMA wamesema El nino ni hali ya hewa kutokana na sehemu. Sehemu zinginezo panawaka jua la El nino.
MY TAKE;
Mafisadi na Wala nchi ya CCM ndo walitia watu hofu ili wakope hela kwenye taasisi za kimataifa. Wamepewa hela wakagawana watu na Msoga rufiji na Zanzibar. Hela zimeisha na Miradi ya maendeleo imesimama. Kumbuka Serikali ya Tanzania ilitenga Bilioni 730 za kupambana na mvua kubwa za El nino. Walidai ni za kukarabati madaraja na kuzibua mifereji na zimeshaisha bila kufanyika chochote.
Watu wamebomolewa nyumba zao kwamba nyumba zimeziba njia ya maji ya mvua za El - nino.
View attachment 3695977
Mifereji ilifukiliwa kujiandaa na JOTO kali. KwishaaaWe ndo hujielewi babu. Sijui huko shule ulikua unaelewaje. Huku mtaani mifereji imefukuliwa sana na pia shule zinafungwa .apema mwaka huu kwa sababu ya mvua kubwa za elninyo kwa tangazo la TMA
700b imeshakwendaWalisha tengeneza mazingira ya kuidhinisha 700 billions, saizi wanatengeneza justification jinsi mounga ulivyo kwisha
so it true what they say, some choose to be foolish in the day light π€£Safi sana Maana Ma CHADEMA yalijua kuna mvua za El Nini ili yaanze kulala ndani bila kufanya kazi ππ
UpuuziSafi sana Maana Ma CHADEMA yalijua kuna mvua za El Nini ili yaanze kulala ndani bila kufanya kazi ππ
Wananchi wanapaswa kueleweshwa nini? Wizara ya elimu ni serekali hiyo, kwanini hao TMA hawakuwafuata na kuwaelisha kuwa Elinino sio mvua tu, hadi wakabadili ratiba za mitihani, na kufunga shule kuhofua mvua ya elinino. Acha jazba na kucheza naaneno.Huyo Jamaa kitaalamu Yuko sahihi kabisa lakini ni vile Tu Sisi ni vichwa panzi akili ndogo, Ukija hata Kwa viongozi wetu ni vichwa maji, wakisimama majukwaani Utasikia mvua za el nino blah blah...Wananchi walipaswa kueleweshwa vizuri kuanzia ngazi za chini kabisa na sio kutishwa tishwa hovyo na viongozi majukwaani....jamani Sisi bado Sana akili VISODA kabisa.
Hapa hata Paschal Mayala au Robert Herieth Mtibeli huwezi kuwakuta. Imagine Mayala ni team Makonda, unatajia atie neno hapa? Uchawa ni janga jipya nchi hii.Ukitaka kuamini kuwa UVCCM na CCM yote kwa ujumla kuwa wengi ni Vichaa na hawana hoja za msingi katika maendeleo ya taifa huwezi kumkuta hapa Tlaatlaah Wala Lucas Mwashambwa Yani wao utawakuta kwenye zile nyuzi zao za porojo kuhusu CHADEMA