TMA wakitoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa shule zifungwe kwa kipindi hicho, tusisubiri wengine wazame tena

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu, salama huko ulipo?

Wataalam wa hali ya hewa wakitoa tahadhari ya mvua kubwa kunyesha shule zifungwe kufuatia matangazo hayo, kama tangazo hili lililotolewa juzi.

Wote tunajua ni hatari kipindi hiki, kwanini shule hazichukui iniative kuongeza usalama kwa watoto.

Halafu cha kushangaza mzazi akimzuia mtoto kwenda shule, siku inayofata mtoto atakula fimbo kwa kutega.

Tunasubiri janga lingime lotokee ndio tuwe tunachukua tahadhari? Utasikia wengine wanakuja na visingizio leo kuna mtihani, sasa kwani huo mtihani hauwezi kusogezwa mbele ukafanyika siku nyingine, kwamba usipofanywa siku hiyo basi shule inaboka na kkla kitu kinasimama?

20240423_070444.jpg

Huyu mwanafunzi hapa kaloa chapa hata shule hata shule hajafika, hapa tu tayari ni ni hatari kwa afya, bado shida za barabara kufungwa, bado hajakutana na madereva wehu, embu tuwe serious kidogo na maisha ya watoto hawa.

Sio kila kitu mpaka msubiri serikalo itoe tamko kwani hamna vichwa mkaona hii ni hatari inabidi tuchukue hatua?
 
Mzazi Usalama wa mwanao uko mikonoi mwako, na unapaswa kuhakikisha anakuwa salama. Kama ulivyotaarifiwa kuchukua tahadhari ya Mvua kwanini usimpeleke mwanao shule? Kwanini usimtafutie namna mbadala iliyo salama?

Haya umeshindwa vyote umekosa hata 1500 ya kununua mwamvuli kwa mwanao ajikinge na mvua?? Mvua ni kubwa mpigie mwalimu wake simu uombe ruhusa weweeee.

Acha kulalamika, wajibika ipasavyo.
 
Mwamvuli wa 1,500 unauzwa wapi?
Watu wana shida zao bana wewe.
 
Na rainboots
Ndio! Lakini wanawaacha wanatembea peku viatu vinabaki nyumbani visiharibike na mvua
Mwavuli unasaidia nini kwenye hii mbua kali + upepo?
Kuwapa watoto likizo kwa kisingizio cha mvua hilo halipo kaa ukijua sababu hizi mvua ni za muda mrefu

Muhimu ni kila mzazi kuhakikisha anampeleka na kumfata mtoto shule anaweza kumtumia hata mfanyakazi
Labda watoto wanaotumia madaraja kwenda shule tena yawe yamejaa ndio wanaweza kupumzika na hilo ukisubiri serikali watangaze utakesha..!
 
Inategemea wapi ni salama wengine nyumbani ndo siyo salama maji yanafika hadi juu ya bati
 
Mzazi Usalama wa mwanao uko mikonoi mwako, na unapaswa kuhakikisha anakuwa salama. Kama ulivyotaarifiwa kuchukua tahadhari ya Mvua kwanini usimpeleke mwanao shule? Kwanini usimtafutie namna mbadala iliyo salama?
Haya umeshindwa vyote umekosa hata 1500 ya kununua mwamvuli kwa mwanao ajikinge na mvua?? Mvua ni kubwa mpigie mwalimu wake simu uombe ruhusa weweeee.
Acha kulalamika, wajibika ipasavyo.
Hii mvua hata mwamvuli haufui dafu. Taifa linalojali watoto wanafunga shule kukiwa tahadhari ya mvua kubwa etc, lakini serikali ipo kimya. Huyo mtoto hata kama kuna usafiri anawahije shule na mibarabara yenye mashimo na kujaa maji.
Jana kuna wanafunzi hadi saa nne wako barabarani hakuna usafiri. Wangine leo wameloa ausbuhi eti wanaenda shule ,hivi mtoto anasomaje ?
 
Saa 4 usiku mtoto yuko barabarani halafu mzazi uko wapi?? Narudia Kuzaa si kazi, Kazi kulea! Wazazi tuwajibike. Watoto wengi wapo hapo barabarani hawana hata nauli wanasubiri lifti tu huko majumbani hamuwapi nauli. Halafu unajiita mzazi shiiiiit
 
Kwa foleni ya jana huyo mzazi angepita wapi kwenda kumchukua huyo mtoto . Maana magari yalikuwa hayaendi mbele wala nyuma toka saa tisa mchana
 
Wazazi muwanunulie watoto miamvuli, au na hili mnawasubiri Ccm?
Hata mwavuli haufai kitu hapo, rain jackets na gumboot hapo anaweza kutoboa! Allah atuepushe mabalaa ya mvua hizi
 
Usalama unaanzia kwa wazazi
Jana mikocheni B kuna mtoto
Mwanafunzi kasombwa na maji
Kapelekwa kwenye mtaro
Na kapoteza maisha

Ova
 
Selikali haiwezi tangaza shule kufungwa kwa kuwa matokeo ya mvua yanautofauti wa kimazingira kwa kila sehemu. Kuna sehemu hata hiyo mvua hawaijui kabisa. Kuna maeneo mengine ni adimu sana mvua kunyesha mchana. Kuna mazingira mengine asubuhi huwa ni jua tu mfano mkoa wa mwanza
 
Ndio! Lakini wanawaacha wanatembea peku viatu vinabaki nyumbani visiharibike na mvua

Kuwapa watoto likizo kwa kisingizio cha mvua hilo halipo kaa ukijua sababu hizi mvua ni za muda mrefu

Muhimu ni kila mzazi kuhakikisha anampeleka na kumfata mtoto shule anaweza kumtumia hata mfanyakazi
Labda watoto wanaotumia madaraja kwenda shule tena yawe yamejaa ndio wanaweza kupumzika na hilo ukisubiri serikali watangaze utakesha..!
Basi ni vyema kwenye ratiba ya mwaka shule zifungwe myongo wa mvua kubwa.
 
Back
Top Bottom