TMA yasema mvua kubwa kunyesha Dar es Salaam kwa siku 4 kuanzia Jumatano Nov. 15, 2023

TMA yasema mvua kubwa kunyesha Dar es Salaam kwa siku 4 kuanzia Jumatano Nov. 15, 2023

Acha kuropoka, watu wanashinda kwenye computer ku-study na ku-analyse weather foresting models halafu wewe unakuja hapa kuropoka!
Wewe acha ujinga, sisi wengine tunajua hali ya hewa na kutabiri itakuaje kwa kuangalia mawingu, joto, nyota, mwezi n.k. usifikiri me ni mjinga kama wewe na ukoo wako msioweza hata kusoma nyakati. Pumbaaav!
 
Baada ya mapumziko ya siku mbili, mvua kubwa za El Nino sasa zinarejea tena Jijini Dar es Salaam na zitanyesha kwa siku nne mfululizo kuanzia kesho Novemba 15 na zitaendelea hadi Jumamosi ya Novemba 18 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA ni kwamba, mvua hizo mbali ya Dar es Salaam pia zitapiga katika mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Visiwa vya Unguja na Pemba ikijumuisha visiwa vya Mafia.

Mikoa mingine itakayokumbwa na mvua hizo kwa Jumatano ya Novemba 15 ni Njombe na Ruvuma ambapo athari zaidi ikiwemo mafuriko na baadhi ya shughuli za kiuchumi kusimama zitajitokeza siku ya Ijumaa.

TMA pia imetahadharisha mvua hizo kuweza kuambatana na upepo mkali unaofikia kasi ya Kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili ukanda wa Pwani ya Kusini ya Bahari ya Hindi mikoa ya Lindi na Mtwara.

111.JPG

22222.JPG
 
zitanyesha kwa siku nne mfululizo kuanzia kesho Novemba 15 na zitaendelea hadi Jumamosi ya Novemba 18 mwaka huu
Ngoja nisubiri Mimi napenda mvua Ila bachukia matope tu, mvua ikinyesha matope alafu washenzi wanafunguliza vyoo kishenzi ni kunuka mavi tu
 
Back
Top Bottom