BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa zinazoweza kuleta madhara zinatarajiwa kunyesha katika mikoa 11 ya Tanzania.
Mikoa hiyo ni Ruvuma, Njombe, Iringa, Morogoro, Mbeya, Songwe, Rukwa, Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara.
Katika taarifa iliyotolewa leo Desemba 27, 2022 na TMA, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia leo hadi kesho Desemba 28, 2022 katika mikoa hiyo ambapo baadhi ya maeneo yanaweza kupata athari.
Taarifa hiyo inasema athari zinazoweza kujitokeza baadhi ya maeneo ni kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za uchumi na usafirishaji, hivyo wananchi wanaoishi maeneo hayo wanatakiwa kuchukua tahadhari.