TMA yatahadharisha mvua kubwa mikoa 11 Tanzania

TMA yatahadharisha mvua kubwa mikoa 11 Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa zinazoweza kuleta madhara zinatarajiwa kunyesha katika mikoa 11 ya Tanzania.

Mikoa hiyo ni Ruvuma, Njombe, Iringa, Morogoro, Mbeya, Songwe, Rukwa, Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara.

Katika taarifa iliyotolewa leo Desemba 27, 2022 na TMA, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia leo hadi kesho Desemba 28, 2022 katika mikoa hiyo ambapo baadhi ya maeneo yanaweza kupata athari.

Taarifa hiyo inasema athari zinazoweza kujitokeza baadhi ya maeneo ni kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za uchumi na usafirishaji, hivyo wananchi wanaoishi maeneo hayo wanatakiwa kuchukua tahadhari.
 
TMA sio wa kuwasikiliza, mara mvua chache, mara mvua nyingi, wala siwafuatiliagi kabisa
 
Si walisema msimu huu utakuwa na mvua chache vipi sasa wamebadili gia angani.
TMA huwa Wana awamu za utabiri,Kuna utabiri wa oktoba na disemba,hata hivyo siku moja kunyesha mvua kubwa haimaanishi msimu kuwa na mvua nyingi,be positive
 
Ukiwa mgeni TZ unaweza ukadhani TMA iko wizara ya kipara.
 
Mbona wapo sawa, kumbuka mvuwa siyo bomba mtu anafungua kama hauamini kafanye shughuli zako mabondeni ikukinyea utajuwa wapo sahihi au la
 
Nyesha mvua nyesha nyesha hata miaka kumi mfululizo nyesha mvua iondoe umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma,watu wapate ufahamu na hekima walahi [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom