TMT show ya kina Monalisa on ITV

TMT show ya kina Monalisa on ITV

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Jumapili moja moja nimekuwa nikifuatilia hii show ya TMT. Watangazaji wake (Joti na Lulu) kwa kweli nawakubali, wamejipanga vizuri.

Majaji mmh, namkubali mmoja tu, Monalisa. Richie na yule sijui Sarungi wananiboa, hawana mvuto wa kuongea.

Richie najua na bongo muvi mzoefu, tena wa siku nyingi lakini ameshindwa kuonyesha uzoefu wake ktk nafasi ya ujaji.

Huyu mwenzake Sarungi (sina hakika sana na hili jina) ndo kabisaaa, hajiwezi!! Ila natamani kumjua zaidi, so kwa aliye na details zake tafadhali tumwagie, binafsi sijawahi kumuona bongo muvi.

Nionavyo mimi: Mwenye kipindi amefanya mabadiliko kwenye safu ya majaji, hawaondoe Richie na mwenzie halafu aweke vifaa vingine kama kina J.B, Wema and the like.

Nahisi kipindi kingekuwa na mvuto wa kutosha na wadhamini wangejitokeza kwa wingi.

Huu ni mtizamo wangu jamani, msinishambulie.
 
Jumapili moja moja nimekuwa nikifuatilia hii show ya TMT. Watangazaji wake (Joti na Lulu) kwa kweli nawakubali, wamejipanga vizuri. Majaji mmh, namkubali mmoja tu, Monalisa. Richie na yule sijui Sarungi wananiboa, hawana mvuta wa kuongea. Richie najua na bongo muvi mzoefu, tena wa siku nyingi lakini ameshindwa kuonyesha uzoefu wake ktk nafasi ya ujaji. Huyu mwenzake Sarungi (sina hakika sana na hili jina) ndo kabisaaa, hajiwezi!! Ila natamani kumjua zaidi, so kwa aliye na details zake tafadhali tumwagie, binafsi sijawahi kumuona bongo muvi.

Nionavyo mimi: Mwenye kipindi amefanya mabadiliko kwenye safu ya majaji, hawaondoe Richie na mwenzie halafu aweke vifaa vingine kama kina J.B, Wema and the like. Nahisi kipindi kingekuwa na mvuto wa kutosha na wadhamini wangejitokeza kwa wingi.

Huu ni mtizamo wangu jamani, msinishambulie!!!
anzisha chako
 
Kama we huwakubali kuna wenzio wanawakubali ambao wanafatilia daily.MTU mwenyewe ushasema huwa unafatilia j2 moja moja.hata hapo we ulipo kuna wanaokukubali na wanaokuchukia uwepo wako mkuu.km unaona we huwapendi basi usitazame hicho kipindi.acha wenzio tusonge mpk tujue nani anakuwa mshindi
 
Huyo unayomsema hawezi ujaji(roy sarungi) amepata tuzo 45 za kimataifa ni msomi ana degree ya sheria ameanzisha vipindi naijeria na vinapendwa sana huko kwa wapopo ni moja ya wataaalamu ktk tasnia ya bongo movie.
 
Mmh.mpango wa director huo jamn.tusubr vngne tu.hcho kshapta..
 
ungewakosoa Mona na Richie lakini sio Roy mbona ndo roho ya Yale mashindano binafsi naimani ataipeleka mbali tasnia ya filam yaani yule jamaa simpingi miaka 1000 tena huyo kitambi jb haingii kwa Roy wema na jb hadhi yao saint kayumba Roy ni kiwango kingine
 
majaji wanajua sana... mleta uzi inaonyesha wewe huwa ndo unaanza kuwajudge
washiiriki hata kabla ya ma- judge kuwachambua...! thats y unawaona wanakosea..!!
 
Wema nae awe judge kwa lipi hasa wakati yeye mwenyewe hata kuigiza hawezi

sema wewe nikisema mimi nitaambiwa mchawi, kuigiza kwenye huyo mama ubaya kumemshinda haya uo u judge ata judge nini? we mwambie kucheza kigodor mtaelewana
 
Huyo unayomsema hawezi ujaji(roy sarungi) amepata tuzo 45 za kimataifa ni msomi ana degree ya sheria ameanzisha vipindi naijeria na vinapendwa sana huko kwa wapopo ni moja ya wataaalamu ktk tasnia ya bongo movie.

U judge ni natural talent, ebu muone monalisa aki judge anavyojiachia yaani yupo free kuji express hisia zake kwa kiwango kinachotakiwa, hajazubaa mchangamfu na haboi.

Huyo roy anaweza kuwa hata na ma phd lakini u judge usi mfit, Yes the guy is boring somehow, japokuwa namkubali sana nadhan ni mmoja wa ma boss wa tmt, inshort kampuni yao imejipanga vibaya, kwanza inaendeshwa na watu wasomi na wanaojielewa, kingine wapo financially strong na wako serious na wanachokifanya, nadhan wataleta mapinduzi kweny mambo ya film
 
sema wewe nikisema mimi nitaambiwa mchawi, kuigiza kwenye huyo mama ubaya kumemshinda haya uo u judge ata judge nini? we mwambie kucheza kigodor mtaelewana

Na sidhani hata hicho kigodoro anakiweza.Yani kile kisauti ndo kinachonichefuaga kabisaaa na kujidai kitoto wakati umri umeishamtupa mkono
 
U judge ni natural talent, ebu muone monalisa aki judge anavyojiachia yaani yupo free kuji express hisia zake kwa kiwango kinachotakiwa, hajazubaa mchangamfu na haboi.

Huyo roy anaweza kuwa hata na ma phd lakini u judge usi mfit, Yes the guy is boring somehow, japokuwa namkubali sana nadhan ni mmoja wa ma boss wa tmt, inshort kampuni yao imejipanga vibaya, kwanza inaendeshwa na watu wasomi na wanaojielewa, kingine wapo financially strong na wako serious na wanachokifanya, nadhan wataleta mapinduzi kweny mambo ya film

We umenielewa vizuri sana, ulichokisema ndo hasa nachomaanisha! Big up mkuu Gosspcopwarumi
 
Last edited by a moderator:
majaji wanajua sana... mleta uzi inaonyesha wewe huwa ndo unaanza kuwajudge
washiiriki hata kabla ya ma- judge kuwachambua
...! thats y unawaona wanakosea..!!

Hujanielewa mkuu, mi sisemei kuhusu maamuzi yao, kasoro ninayoiona ni namna wanavyoongea kama majaji.

Hebu soma comment ya mdau hapo No.14 ujue nilichomaanisha, amefafanua vizuri sana, namnukuu hapa ....U judge ni natural talent, ebu muone monalisa aki judge anavyojiachia yaani yupo free kuji express hisia zake kwa kiwango kinachotakiwa, hajazubaa mchangamfu na haboi.

Huyo roy anaweza kuwa hata na ma phd lakini u judge usi mfit, Yes the guy is boring somehow......
 
Kama we huwakubali kuna wenzio wanawakubali ambao wanafatilia daily.MTU mwenyewe ushasema huwa unafatilia j2 moja moja.hata hapo we ulipo kuna wanaokukubali na wanaokuchukia uwepo wako mkuu.km unaona we huwapendi basi usitazame hicho kipindi.acha wenzio tusonge mpk tujue nani anakuwa mshindi

we unaongea kishabiki and not realistic way
 
Back
Top Bottom