Toa neno lolote kuhusu michango ya Harusi

Toa neno lolote kuhusu michango ya Harusi

Daaaa.....michango hii inakera wakati nikitaka kuoa nilikuwa mzito sana kuomba michango kwa washkaji .ila nikajikaza nikawacheki wanangu kama wawili hivi ..oyaa mwenenu nataka kuchukua chombo nipeni support yenu ila kiukweli nlikuwa najua kabisa wana hawana mishe za kueleweka nlitaka tu wajue kuwa nimewaomba michango ila sikuzingatia sana......ila wengine wote niliwaambia tu naoa lakin sikuomba mchango kwa mtu wala ndugu...na budget yangu ya harusi ilikuwa 120k tu...... Nilijipanga kwa hilo sikutaka show off.hata ndugu kwenye vikao vyao niliulizwa bwana harusi unachangia ngapi katika budget nikasema hali mbaya lakin sio kweli.sikutaka mambo mengi.Na chakushangaza tunaishi gheto watu wanne na jamaa hawajui jamaa akioa tutaishi vipi.kumbe kuna kimjengo pemben nlishajenga kimya kimya na hela za kubutua .........


Harusi sio michango

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
Hongera!! Last year mwaka Jana nilimsimamia Harusi rafiki yangu aliekataa kuchangisha ilikuwa poa Tu watu wachache.
 
Mm nilishakataa mambo ya kuchangia harusi maana sio tukio la kushtukiza kama ugonjwa au kifo watu wanaplan kabisa kuoa sasa kwann usiandae budget yako unaanza sumbua watu.

Mi niko tayari kumchangia mtu hela ya kuanzia maisha kuliko hizo sherehe mtu anamaliza harusi anabaki na madeni mengi kumbe alikopa ili kufanikisha harusi ni heri tuwe tunawachangia hela hata ya kuanzia maisha.

Tuchangiane kwenye maendeleo kama kusoma, ujenzi n.k sio upuuzi huo kama huwezo endorse harusi yako mwenyewe bora usifanye sherehe fungal harusi isiyo na mbwembwe
Nimaliza
 
Mm nilishakataa mambo ya kuchangia harusi maana sio tukio la kushtukiza kama ugonjwa au kifo watu wanaplan kabisa kuoa sasa kwann usiandae budget yako unaanza sumbua watu. Mi niko tayari kumchangia mtu hela ya kuanzia maisha kuliko hizo sherehe mtu anamaliza harusi anabaki na madeni mengi kumbe alikopa ili kufanikisha harusi ni heri tuwe tunawachangia hela hata ya kuanzia maisha. Tuchangiane kwenye maendeleo kama kusoma, ujenzi n.k sio upuuzi huo kama huwezo endorse harusi yako mwenyewe bora usifanye sherehe fungal harusi isiyo na mbwembwe
Nimaliza
Ni kweli mkuu Jamii yetu kwa ujumla ni nadra kuchangia mtu ktk vitu vya msingi.
Mwaka Jana nilihudhuria Harusi ya rafiki yangu alijigharamia kujifanyia Harusi, ndugu ndio walikuwa wanataka mambo makubwa am glad alikuwa na msimamo Kila kitu kilienda alivyotaka.
 
Ni kweli mkuu Jamii yetu kwa ujumla ni nadra kuchangia mtu ktk vitu vya msingi.
Mwaka Jana nilihudhuria Harusi ya rafiki yangu alijigharamia kujifanyia Harusi, ndugu ndio walikuwa wanataka mambo makubwa am glad alikuwa na msimamo Kila kitu kilienda alivyotaka.
Muhimu mwanaume kuwa na msimamo ukitaka kuwa na familia yenye furaha sio baada ya honeymoon mnaanza kulipa madeni ya harusi ni ujinga uliopitiliza na mwanaume unakuwa umefeli kusimama kama kiongozi wa familia
 
Jambo baya nisilopenda mnoo, nnakoelekea ntatangaza rasmi kuachana na huu ujinga, tena mtu anakuadd tu bila kukuambia aisee mnaboaaaaaa
 
Kuchanga Kwa kinyongo huchangia sana ndoa kutodumu
 
Back
Top Bottom