inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,805
- 22,633
Ndiyo maana nimekuuliza ikiwa umewahi kuigusa QUR'AN,ungekua umeigusa QUR'AN usingeandika ulichoandika, waarabu waliupiga Vita uislam sababu ulikua kinyume na utamaduni wao,ama kuhusu issa na yesu naiamini Qur'an,siyo biblia ambayo habari za yesu zimeandikwa miaka 100 baada ya yesu kuondoka,huku ikijichanganya na kuwa na maandiko yanayopingana kimantikiUngejibu Kwanza swali ndipo uulize hayo maswali yako.
Lengo la Quran lilikuwa kuwaambia Waarabu kuwa Mungu ni mmoja na waache kuabudu miungu kwenye like Jiwe Jeusi ilipokuwa miungu 360. Zaidi ya hapo Quran haina jipya hata Kwa Waarabu wenyewe. Kwani mengine yote yalikuwa utamaduni WA Waarabu.
Sasa tusitoke kwenye mjadala.
Nioe hoja tatu kubwa zinazokufanya uamini Yesu ndiye ISA
Toleo la biblia la kiswahili la impremanto wewe umeliona!?..kaulize kanisani wakupe,toleo la biblia tulilotumia 1990s mwishoni tu limebadilishwa,maneno Kama swaumu, sikukuu ya IDD,kuwatawadha miguu wanafunzi yametolewa na kuweka mengine mfano kuwaosha miguu wanafunzi nk, nimekwambia kiebrania yesu akiitwa y'shua, kiebrania Ishmael wakati kiarabu ismail, tofauti ya sh na s, kwenyewe y'shua toa sh weka s ili upate kwa kiarabu jina litatamkwa vipi,au Ishmael siyo ismail!?..vizuri umeweka kigiriki hapo,linatamkwaje kigiriki kwa mujibu wa ulivyoandika?Sasa mbona Umeeleza vizuri lakini umeshindwa kui-drive Yeshua mpaka ifike Kwa Isa( eisa) wa Quran.
Uelewe pia hapa unazungumzia Fonetiki ya Lugha Kwa hiyo kama huna utaalam wa Lugha ni Bora uomne msaada uelezewe.
Ni Kwa nini Jesus iwe Yesu, au Yeshua kiebrania iwe Iesus Kwa kigiriki.
Mambo ya kusema Biblia ilibadilishwa ni uzushi kama hauna Biblia halisi ambayo haijabadilishwa.
Aramaic ni ya wasyria wakati Hebrew ni waisrael,zote ni semitic zenye misamiati sawa,ni Kama kisukuma na kinyamwezi,na hakuna herufi 'e' kwenye hizo lugha,herufi hiyo inawekwa na watu wa ulaya kufuata lugha zaoYeshua ni kiaramaic.... Kiebrania ni Yahushua
Jielimishe babu acha kubandika watu sifa ya uwongo, google tu 'jesus' name ni Hebrew' halafu uje uniambieHuu ni uongo..... Kiebrania inatamkwa kama Yahushua.......kama mtu anayetoa na kuvuta pumzi , ukitaka yi, unavuta au kutoa pumzi?
Acha kudanganya watu.
Sasa unabisha?Jielimishe babu acha kubandika watu sifa ya uwongo, google tu 'jesus' name ni Hebrew' halafu uje uniambie
Nimekuambia jina lake ni Yahushua kwani Kuna e apo?Aramaic ni ya wasyria wakati Hebrew ni waisrael,zote ni semitic zenye misamiati sawa,ni Kama kisukuma na kinyamwezi,na hakuna herufi 'e' kwenye hizo lugha,herufi hiyo inawekwa na watu wa ulaya kufuata lugha zao
Eliya anaitwa Eli-Yahu( YHWH /Yahu ni Mungu)Jielimishe babu acha kubandika watu sifa ya uwongo, google tu 'jesus' name ni Hebrew' halafu uje uniambie
Mimi nikiamua kujibu hakuna hoja hata moja ya nguvu uliyoitoa isipokuwa sikuwa na makusudio ya kuchangia mjadala huu, ila ukinitaka nichangie naweza na nitaanza kama ifuatavyo.Sasa Baada ya hayo maelezo jibu hoja za huu Uzi hata Moja ili Watu wajifunze.
Una Torati ,zabri na Injili ambazo hazijaharibiwa tufananishe na hiz ambazo zimeharibiwa?Mimi nikiamua kujibu hakuna hoja hata moja ya nguvu uliyoitoa isipokuwa sikuwa na makusudio ya kuchangia mjadala huu, ila ukinitaka nichangie naweza na nitaanza kama ifuatavyo.
Bismillah, kwa ufupi mkubwa mijadala ya kumtofautisha issa mwana wa mwaryam alayhi ssalaam na yesu imekithiri siku za karibuni, na malengo ya mijadala hii ni kupindisha ukweli kwa makusudi baada ya kushindikana kuvunja hoja kuwa uislamu umemtukuza masihi issa alayhi ssalaam na kumpa heshima kubwa kuliko ukristo uliomtweza na kumfanya msulubiwa tena aliyedhalilishwa mbele za watu.
Jambo la pili, mijadala hii pia imekithiri baada ya kuwa kule kuonekana masihi issa amani juu yake ndio uzi mwembamba baina ya uislamu na ukristo hivyo wahafidhina wakaona bora kusema huyu si yule ili kuhafifisha hoja za wapinzani wao, maana tukikubaliana sio mwana wa mungu na tukikubaliana hajasulubiwa kama uislamu ulivyoeleza basi hakuna ukristo tena.
Tukirudi kwenye mada, binafsi sio muumini wa hearsay's hivyo mapenzi yangu ni kutoa hoja kutoka kwenye certified source ni mamoja iwe kutoka kwenye maneno ya allah yaani Qur'an au hadithi sahihi za mtume swala na salaam ziwe juu yake zilizoshuhudiliwa na wanawachuoni wakubwa wa fani ya hadithi juu ya usahihi wake, kwa sababu hiyo hoja za kutoka upande huu zitabaki zenye nguvu zaidi daima kutokana na usahihi wa kule zinapotoka.
Masihi issa mwana wa mariam ni mtume wa allah na ndie mtume wa pili kutoka mwisho na baina yake yeye na mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yao ni miaka 600 takriban, yeye alitoa bishara ya kuja mtume muhammad na nabii ibrahiym alayhi ssalaam aliomba dua allah awapatie mtume pale alipoacha kizazi chake yaani mkewe haajar na mwanae ismail alayhi ssalaam, hivyo yeye mtume muhammad ni bishara ya ndugu yake issa mwana wa mariam na dua ya baba yake ibraahiym juu yao swala na amani.
Turudi nyuma kidogo bila kurefusha sana maneno, nabii zakariyyah alayhi ssalaam alikosa mtoto kwa muda mrefu mpaka akafikia uzee na yeye ndio alikuwa mlezi na muangalizi wa mariam bint imraan mama yake na nabii issa, wakati fulani aliyaona mambo yasiyo ya kawaida kwa mariam na habari hii imeelezwa vizuri katika Qur'an pale allah aliposema.
"Hakika allah alimteua adam na nuhu na ukoo wa ibrahim na ukoo wa imran juu ya walimwengu wote."
"Ni kizazi wao kwa wao,na allah ni mwenye kusikia na mwenye kujua."
"Aliposema mke wa imran, mola wangu mlezi! nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu, basi nikubalie! hakika wewe ndiye mwenye kusikia mwenye kujua."
"Basi alipomzaa alisema: mola wangu mlezi! nimemzaa mwanamke! na allah anajua sana aliyemzaa, na mwanaume si sawa na mwanamke, na mimi nimemwita mariam, na mimi namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na shetani aliyelaaniwa."
"basi mola wake mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya zakariyyah kuwa mlezi wake, kila mara zakariyyah alipoingia kwake alimkuta na vyakula, basi alimwambia: ewe mariamu! unavipata wapi hivi? naye akasema: hivi vinatoka kwa allah, na allah humruzuku amtakaye bila ya hisabu."
"basi hapo zakariyyah akamwomba mola wake, akasema: mola wangu mlezi! nipe kutoka kwako uzao mwema, hakika wewe ndiye unayesikia maombi."
"Basi akamuita yeye malaika na hali ya kuwa amesimama akiswali kwenye mihrabu "hakika anakubashiria {kupata mtoto aitwae} yahya, atayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa allah, ni bwana na mtawa na nabii kwa watu wema."
Qur'an 3:33-39
Mpaka mwisho wa habari hii, nimeleta aya hizi kwa makusudi kuonesha ufanano wa matukio ya zakariyyah, maryam, yahya na issa mwenyewe amani iwe juu yao, watu hawa kamwe haiwezekani kuwatenganisha kwasababu kwa uhakika hasa hilo haliwezekani.
Torati, injili, na zaburi vyote ni vitabu vimetoka kwa allah na ni maneno yake na si ya mwanadamu katu, ila tu hivyo vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono ya watu wakayabadili mengine na mengine wakayafuta, na uwezekano wa kuyafuta yote ni mdogo ndio maana utaona tofauti ya majina ya kihebrania lakini yanawiana na yaliyotajwa kwenye Qur'an kwasababu yote ni majina ya kiajemi, na issa mwana wa mariam atarudi mwisho wa zama na atakufa kama wanavyokufa wanadamu wengine.
"Na mayahudi wanasema uzeir {ezra} ni mtoto wa allah, na wakristo wanasema, masihi ni mtoto wa allah, hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao, wanayaiga maneno ya waliokufuru kabla yao, allah awaangamize! vipi wanageuzwa? {kuacha ukweli kuulelekea uongo}."
Qur'an 9:30
Nahofia kurefusha zaidi faida ikawa ndogo, tuanzie hapa.
Uislamu una matobo Sana ,mfano hii hoja ya Isa sio Yesu ,unaona inavyoshindwa kujiteteaUzuri ni kuwa Imani ya uislamu haitaji approval kutoka Kwa watu wa dini nyengine. Amini utakavyoamini lakini Imani yako haibadilishi chochote juu Imani ya uislamu. Uislamu utakuwa vilevile.
Hakuna 'hu' kwenye jina la yesu kiebrania babuNimekuambia jina lake ni Yahushua kwani Kuna e apo?
Koran imeandika habari za Isa baada ya miaka mingapi baada ya Isa kuwepo?ama kuhusu issa na yesu naiamini Qur'an,siyo biblia ambayo habari za yesu zimeandikwa miaka 100 baada ya yesu kuondoka,huku ikijichanganya na kuwa na maandiko yanayopingana kimantiki
Ni iliyahu/iliyabu ..hakuna 'e'Eliya anaitwa Eli-Yahu( YHWH /Yahu ni Mungu)
Yesu anaitwa Yahu-shua (YHWH/Yahu anaokoa)
Qur'an ni wahyi(ufunuo toka kwa Mungu mmoja asiye na mshirika,hakuzaa Wala kuzaliwa,Hana mwana Wala baba,ana wivu)...miaka mingapi baada ya issa kuwepo Hilo Sina hakika,Ila Wana historia wanadai Isa aliondoka duniani akiwa na miaka 33 wakati Muhammadi kapata utume 610ADKoran imeandika hanari za Isa baada ya miaka miangapi baada ya Isa kuwepo?
Tafadhali jibu kama swali nilivyoliuliza
Hayo maelezo umetoa kwenye chapter gani ya biblia?Ndio maana nikakuambia hata mambo Subiri wakubwa wako wajadili.
Nimejadili jina Yeshua etymological, asili yake nikakuambia ni tofauti na isa.
Kisha nikaelezea maana ya jina Yeshua ni Mwokozi, Semantically ambayo ni tofauti na ISSA.
Nikikuambia ueleze maana ya jina Issa Kwa mujibu wa Quran utaeleza?
Acha uvivu kijana. Ingia hata youtube andika "how to pronounce Jesus in aramaic" halafu uone kama itakuja uongo uliouandika.Kiaramaic aliitwa Yeshua ambalo Kiebrania ni Yahushua ambalo Kiarabu ni Yusha,
Hapana hakuna na baadhi ya maneno ndio hayo yako kwenye hiyo inaitwa biblia, na kwa kubadilishwa huku sisi tumetoshelezwa na Qur'an kwasababu imekuja kutueleza baadhi ya habari za torati na injili na zaburi pia, bali hizo zilikuwa sheria za wana wa israeli sisi ni umma na zama nyingine wala zisitufae tena, baadhi ni kama aya hii.Una Torati ,zabri na Injili ambazo hazijaharibiwa tufananishe na hiz ambazo zimeharibiwa?
Sent using Jamii Forums mobile app