Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 14,677
- 18,561
Ndio Yesu anauwezo wa Kusamehe dhambi kwakuwa ndiye Mungu. Tatizo lako unamwangalia Kimwili kama baadhi ya Wayahudi.Alipokua anasulubiwa alisema 'Baba wasamehe,hawajui walitendalo'... unamaanisha alikua anajiambia mwenyewe!?..'huwezi kufika kwa Baba bila kupitia Mimi' napo alikua kavurugwa Kama wewe!?...huwa unafikiri kweli!?
Soma Qura 19:28
Inasema Mama wa Isa ni Mariam dada wa Haruni na Musa.
Na ni kweli Imrani alikuwa na watoto watatu. Musa, Haruni na Miriam.
Wewe kichwani una togwa tu!!..Mimi nimekuuliza aliposema 'Baba wasamehe hawajui walitendalo'..alikua anamwambia Baba wa nani!?Ndio Yesu anauwezo wa Kusamehe dhambi.
Marko 2:5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,
7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi.
Una swali lingine ujibiwe ?
Injili hizi zinaeleza maisha ya Yesu, kifo chake na jinsi alivyofufuliwa na Mungu Mkuu na kupaa Mbinguni.Hiki kitabu ndio umeamrishwa ukifuate kikupatie muongozo katika maisha yako yote?.
Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.
32 Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?
33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.
Tukusikilize wewe au alicho waambia ndugu zake Wayahudi ?
Tokea lini Mariamu awe dada wa Haruni Kwa Imani?Hebu tuangalie Quran Aya 19:27-28 “Baadaye akamleta yule (mtoto) kwa watu wake akiwa amembeba (mikononi mwake). Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta jambo la ajabu! Ewe dada yake. Hakika baba yako hakuwa mtu mwovu, wala mama yako hakuwa mwanamke kahaba.
Hakuna makosa katika Aya za Tukufu hapo juu!.
Hebu tuangalie Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema nini kuhusiana na Aya hii tukufu:
Mughira b. Shu’ba amesimulia:
“Nilipokuja Najran, waliniuliza (Wakristo wa Najran): Umesoma “Ewe dada yake Harun (Harun)” (yaani Mariamu) katika Qur’ani, ambapo Musa alizaliwa muda mrefu kabla ya Yesu. Niliporudi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ziwe juu yake) nilimuuliza kuhusu hilo, akasema: (Watu wa uzee) walikuwa wakiwapa majina kwa majina ya Mitume na wachamungu. waliowatangulia.” (Tafsiri ya Sahih Muslim, Kitabu cha Tabia ya Jumla (Kitab Al-Adab), Kitabu 025, Namba 5326)”
Kama tunavyoona kwa uwazi kutoka katika Kauli (Hadith) ya Mtume wetu kipenzi, suala hili lililetwa kwake hapo awali na akalijibu kwa uwazi. Dai la uwongo lililotolewa dhidi ya Mtume wetu kuhusu yeye kumaanisha kwamba Mariamu alikuwa dada wa kibiolojia wa Harun linakanushwa waziwazi.
Watu wa Isreal walikuwa wakiwaita watu kwa majina yao ya mwisho, au kwa kuongeza maneno kama wewe "Mwana wa..." au "Ndugu wa...." au "Dada wa...." Walipoita watu. "Ee Mwana wa...." hawakumaanisha mtu huyo awe mtoto halisi wa mtu ambaye walimtumia jina lake. Mtu mwingine anaweza kuwa tu katika mti wa familia au jina la mwisho.
Yesu alipoitwa "Yesu mwana wa Daudi" kwa mfano, Wayahudi hawakuwa na maana ya kumwita Yesu mwana halisi wa Daudi. Vile vile walipomwita Maryamu “Ewe dada yake Harun” walimaanisha kumwita dada yake Harun kwa imani! Sio dada halisi wa kibaolojia wa Haruni.
Quran Tukufu ilizungumza kuhusu Harun kuwa ndugu wa kibiolojia wa Musa na mjumbe kwa Firauni katika Aya za Mtukufu 2:248, 4:163, 6:84, 7:122, 7:142, 7:150-151, 10:75, 10:87 , 10:89, 19:28, 19:53, 20:30-35, 20:42, 20:70, 20:92-94, 21:48, 21:23, 21:45, 25:35-36 , 26:13, 26:48, 28:34-35, 37:114-122 na zaidi.....
Quran Tukufu pia inazungumza kuhusu Musa kuwa watu wa Isreal Mtume wa kwanza wa Mwenyezi Mungu katika Aya za Mtukufu 2:108, 2:248, 4:153, 5:20-26, 6:84, 14:8, 19:51-53 , 22:44, 25:35-36, 28:3, 37:114-122, 18:60-82, 20:9-48, 27:7-12, 28:29-35, 79:15-19 , 7:109-126, 10:79-82, 20:56-73, 26:38-51, 33:7, 2:53, 2:87, 2:136, 3:84, 6:91, 6 :154, 7:144-145, 10:87, 11:110, 14:5, 17:2, 21:48, na zaidi....
Quran Tukufu pia inazungumza juu ya Yesu kuja kwa watu wa Isreal miaka mingi sana baada ya Musa na Mitume wengine wengi wa Mwenyezi Mungu ambao walitumwa kwa watu wa Isreal katika Aya 3:49-51, 5:46, 5:72. 43:59, 61:6, 61:14, 4:171, 5:75, 43:59, 42:13, 4:172, 19:30, 43:64, 43:63, 3:52-54, 5:111-113, 57:27, 61:14, 61:6 na mengine mengi.....
Quran Tukufu pia inazungumza juu ya Mariamu kuwa Mama wa Yesu wa kibiolojia katika Aya 3:35-37, 19:22-26, 21:91, 66:12, 5:75, 21:91, 4:156, 4: 171, 5:17, 5:116, 21:91, 3:42-51, 19:16-21, na mengine mengi...
Kwa hiyo ikiwa Quran Tukufu inazungumza kwa uwazi kabisa kuhusu Harun kuwa ni ndugu wa kibiolojia wa Musa, na inazungumza kwa uwazi kuhusu Yesu kuja miaka mingi baada ya Musa na Mitume wengine wengi wa Mwenyezi Mungu waliotumwa kwa watu wa Isreal, na inazungumza waziwazi kuhusu Mariamu kuwa Mama wa Isa, basi Qur'ani Tukufu
(1) Inamtambua Mariamu kuwa ni mwanamke aliyezaliwa miaka mingi baada ya Harun, na
(2) Mayahudi walipomwita Maryamu 'Ewe dada yake Harun..', basi walimaanisha kuwa ni Dada yake Harun.
Haruni kwa imani tu na sio dada wa kibiolojia.
Nimekuambia yeye ndiyo Baba kwa Andiko sasa we unataka nini tenaWewe kichwani una togwa tu!!..Mimi nimekuuliza aliposema 'Baba wasamehe hawajui walitendalo'..alikua anamwambia Baba wa nani!?
Mbona unajibu nisicho kuuliza??Wala watu hawakuamrishwa kutibu kwa kutumia majina ya wanadamu wenzao, bali watu wameamrishwa kumtegemea muumba wa mbingu na nchi peke yake na hilo ni ibada.
Hata yeye mwenyewe hakuwaamrisha wanafunzi wake wamtukuze kwa kiasi hiki.
Kumbe Yesu aliwahi sema hivyo?Wewe kichwani una togwa tu!!..Mimi nimekuuliza aliposema 'Baba wasamehe hawajui walitendalo'..alikua anamwambia Baba wa nani!?
Msemaji nani??"Na hizo ndizo hoja zetu tulizompa ibrahim kuhojiana na watu wake, tunamnyanyua kwa daraja tumtakaye, hakika mola wako ni mwenye hekima mwenye elimu."
"Na tukamtunukia {Ibrahim} is-haq na yaakub, kila mmoja wao tulimwongoa, na nuhu tulimwongoa kabla, na katika kizazi chake tulimwongoa daudi na suleiman na ayyub na yuusuf na musa na harun, na kama hivi ndivyo tunavyowalipa watendao wema"
Qur'an 6:83-84
Mpaka mwisho wa habari hizi, ukitizama hapo utaona mitume wote waliopewa vitabu tulivyotajiwa habari zake wametajwa hapo na hii ni katika kushinda kwa Qur'an.
Injili hizi zinaeleza maisha ya Yesu, kifo chake na jinsi alivyofufuliwa na Mungu Mkuu na kupaa Mbinguni.
Inatuonyesha jinsi Yesu alivokuwa anawasiliana na Mungu Baba yake kwa maombi yasiyokoma huku Mungu akimthibjtisha kuwa ni Mashiach Kwa miujiza na Matendo ya ajabu yasiyo ya kibinadamu.
Hivi anayezungumza kwenye Torati ni Nani?Mbona umeikimbia aya ya 34 ??
Hata hivyo, pale Wayahudi walipomtuhumu kwa kudai uungu, kwa kutegemea sentesi hiyo,
Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je, haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu;"
Amewabainishia, kwa mfano wa maandiko unaojulikana sana kwao, kuwa yeye alikuwa anatumia lugha ya kistiari ya manabii ambayo haipaswi kufasiriwa kwa kujipachika uungu yeye mwenyewe au kwa mtu mwingine yoyote.
Ushahidi zaidi unachukuliwa kutoka katika mstari wa kumi na wa kumi na moja wa Injili kwa mujibu wa Yohana, sura ya 14, pale watu walipomtaka Yesu awaonyeshe Baba, naye inaaminiwa alisema:
"Husadiki ya kwambi mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwambi mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.”
Ibara hizi zingeashiria uungu wa Yesu, kama sehemu iliyobakia ya Injili hiyo hiyo inapuuzwa.
Hata hivyo, aya tisa baadaye, katika Yohana 14:20, pia Yesu anarekodiwa akiwaambia wanafunzi wake,
"Siku ile mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.” Kwa hiyo, kama maelezo ya Yesu "Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; yanamaanisha kuwa yeye ni Mungu, basi vivyo hivyo iwe kwa wanafunzi wa Yesu.
Hii sentensi ya kiishara inamaanisha umoja wa lengo na sio umoja wa asili.
Tafsiri ya kiishara inasisitizwa zaidi katika Yohana 17:20-21, pale Yesu aliposema,
"Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Tokea lini Mariamu awe dada wa Haruni Kwa Imani?
Kwa Wayahudi, hakuna undugu wa Imani ila undugu wa damu.
Pili Mariamu alikuwa wa kabila la Yuda, uzao wa Daudi kutoka kwa mtoto wake Nathani.
kisilamu silamu umepata patia mtu wanguBorn in a Stable?
Was Jesus born in a stable? Or a barn? Or a cave?
Luke* says only a manger. There was no room for him in the kataluma ("inn" or guest room).
But Joseph supposedly had returned to his ancestral home, "the lineage of David". So the place should have been chock-full with his own relatives. And not one of them would accommodate a heavily pregnant woman? Tut-tut.
The reality is that the story of Jesus is enhanced by the "humble birth".
Early Christians were taken by the idea that he was, in fact, born in a cave. Can you get any more humble than that?
* Matthew, a tad more realistic, says, "And when they had come into the house ..." (2.11).
Mlitaka maelezo ya Qur'an kuhusu Isa yawe sawa na ya Biblia kuhusu Yesu ndio mkubali kwamba Isa anyekusudiwa kwenye Qur'an ndio Yesu anayezungumziwa kwenye Biblia?Amefanya hivyo kwa lengo moja tu la kupotosha.
Kwa maana hiyo Qur an ilikuwepo kabla ya kuumbwa kwa binadamukwani we hujui kuwa mapepo na majini yanaumbwa kwa aya za Quran?
Hivi anayezungumza kwenye Torati ni Nani?
Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je, haikuandikwa katika Torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu;"
Kutokana na hilo andiko uliloliweka huoni kuwa Yesu anasema kuwa Yeye kasema kwenye Torati.
Kasema " Ndinyi Miungu"
Jiulize sasa Yesu alikuwepo wakati wa Torati ?
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako,[emoji117]mimi niko.
Kutoka 3:14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; [emoji117]MIMI NIKO amenituma kwenu.
Nyie Mtume ashawachanganya hamuwezi kuielewa Biblia.
kwishneykisilamu silamu umepata patia mtu wangu
Kwa mujibu wa Wayahudi, nadhani unaijua filamu ya Matendo ya Yesu imetengenezwa na Ndugu zake Wayahudi.Mlitaka maelezo ya Qur'an kuhusu Isa yawe sawa na ya Biblia kuhusu Yesu ndio mkubali kwamba Isa anyekusudiwa kwenye Qur'an ndio Yesu anayezungumziwa kwenye Biblia?
Mtanziko!!.. abracadabra siyo!!..yeah,ndo Imani yenu ilivyo,ukiichimba kidogo tu sharti upate kizunguzungu..ndiyo maana wazungu wameachana na dini wanasema hakuna Mungu maana vitu havieleweki...endelea kujificha kwenye hicho kichaka ulichoamua kujificha badala ya kujibu hojaKumbe Yesu aliwahi sema hivyo?
Si mnaamini hakufa?
Kwanini mnatumia Maandiko hayo wakati yalikuwa maneno ya Yesu akimuomba Mungu wake ambaye alimuita Baba akiwa pale msalabani?