Kwanini aitwe bin Yussuf? hakumzaa wala hana nasaba nae. Kwanini umpe ubin ambao hauhusiki na yeye hata kisheria! hivi unaelewa maana ya Bin?

Je Issa ni Mwana wa Mariam au hapana? Jibu hili
 
Mbona hamjibu swali

Hatujibu swali gani ?

Unajua kama hii mada ilipaswa iwe imeshaisha tangu kitambo sana ?

Na kama ukifatilia mada utaona kabisa mtoa mada anataka tujadili uungu wa YESU. Kwanini nasema hivyo ? Ukirejea kichwa cha mada ameuliza swali kwa waislamu kwanini wanamuita YESU mwana wa MARIAM ?Tukamjibu,wakati huo huo anasema ya kuwa YESU baba ake ni YUSUFU kwa kumlea sasa kama anajua hilo anachotaka kujadili kiakuwa kimeangushwa na kujua kwake kuwa YUSUFU ni baba mlezi wa YESU.
 
Sisi tunafahamu kwamba Yesu hakuzaliwa kwa namna ya kawaida inayofahamika kwa kuwa ni Mungu. Sasa tunawauliza wanaosema sio Mungu kwa nini basi yanamuita kwa jina la mama yake na sio la mume wa mama yake?
Adam na Hawa, hawana Baba wala Mama. achilia mbali kuzaliwa, hawa ndio hawakuzaliwa kabisa lakini wamekuja duniani, kwanini basi hawa wasiwe Waungu? Naomba jibu.

Jibu la swali lako, limetumika jina la Mamake kwa sababu hana baba. Halijatumika la mume wake kwa sababu mumewe hajahusiana kabisa na Issa. Huwezi kumpa mtu ubin ambao haumhusu
 
Nikisoma na kusikia habari za Quran na Biblia jinsi zilivyofanana huwa najua kabisa kuna uongo umefichwa katikati ya ukweli na ndio maana ni ngumu sana kujua usahihi wa maandiko kati ya dini mbili hizi. Mungu yupo ila kuna sehemu hizi habari zimekuwa twisted kumuhusu na ndio maana kuna madhehebu katika uislamu na ukristu.
 
Yusuf siyo baba'ke Yesu. Kiislam baba ni yule "biologically" tu.

Yesu hakuwa na baba "biologically" kwa hiyo ni lazima aitwe kwa ubini wa mama'ke.

Uislam unafundisha kuwa Yesu kazaliwa kwa neno tu "kun fa yakun" kuwa na inakuwa.

Adam hakuwa na baba wala mama ndiyo maana Kiislam hana ubini wa baba wala mama isipokuwa sisi sote tuna u bini wa Adam, Bin Adam.

Yesu mwenyewe hajawahi kumuita Yusuf "baba".
 
17. Tukampelekea Roho wetu, HAWA wengi walikuwa kina nani maana inaonesha walikuwa mobu kubwa , Yesu na huyo issa sio wamoja wapo tofauti kabisa,

Huo ni ufasaha wa lugha,yaani wngi kumaanisha moja katika lugha ni maarufu sana hata kwa Waswahili.

Unspo kataa kuwa YESU si ISSA huku ni kuihujumu elimu na kuukata Ukweli wazi wazi. Na huwezi kapinga hili kielimu hata ukipewa miaka mia. Huwezi kumtofautisha YESU na ISSA kielimu zaidi ujinga na mapenzi ya upofu.

Anaezungumziwa ni mmoja bali kwa maelezo tofauti.
 
Biblia ni kama maktaba ya vitabu na toka mwanzo kuna baadhi ya vitabu vilienguliwa kutokana na vigezo fulani ili kutengeneza biblia ya kwanza. Fuatilia historia ya utengenezaji wa biblia personally na uache kuyumbishwa na maneno ya kusikia. Unaruhusiwa kuwa na OPINION ila kama mtu muerevu yakupasa kutumia FACTS katika mambo muhimu. By the way hakuna mabishano ya kiimani yaliyowahi kuisha hivyo, focus kwenye kuwa mwema na kuamini imani yako
 
Sababu hapa tunaongelea elimu na elimu iko wazi,naomba uonyeshe huo uongo uliofichwa na umejuaje hilo ?

Pili,naomba uniambie wewe huwa unatumia njia gani kujua habari gani ya kweli na ipi ya uongo ? Jitahidi kuandika kielimu na usiandike kihisia.
 
Na hakuna kipengele chochote katika elimu ya mijadala kinachosema kwamba muafaka mwisho wa mjadala ni lazima.

Cha msingi katika mjadala ni hoja,na mwenye kuelewa ataona ukweli uko wapi,akiamua ataufata asipoamua hta ufata.

Tuendelee...
 
Tatizo hujanielewa, ninachomaanisha ni kuwa kama habari za Quran na Biblia zingekuwa hazina mfanano au la zinafanana kwa kila kitu hivyo, tungesema hizi habari zimejaa ukweli maana hakuna COMPARISON. Kuwepo kwa mfanano wa habari Issa na Yesu au Mussa, Ayoub au Suleiman katika vitabu vyote viwili inaonesha dhahiri kuwa habari za vitabu hivi vyote viwili vina asilia MOJA lakini pia utofauti wake katika muendelezo au simulizi zake ambao huleta mkanganyiko huonesha dhahiri kuwa, Kuna habari ya uongo ndani yake na ndio concept yangu ya "uongo uliofichika ndani ya ukweli huja".
 
Na hakuna kipengele chochote katika elimu ya mijadala kinachosema kwamba muafaka mwisho wa mjadala ni lazima.

Cha msingi katika mjadala ni hoja,na mwenye kuelewa ataona ukweli uko wapi,akiamua ataufata asipoamua hta ufata.

Tuendelee...

nadhani katika kila kanuni kuna EXCEPTIONS na hizo ndizo nilizozitumia kumjibu
 
Kwa hiyo apo ww ukitaka kusema umepeleka kitu flani , utasema nimepeleka kitu changu au utasema nimepeleka kitu chetu embu weka sawa
 
Kazaliwa kwa namna ipi bila ya Baba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…