DZUDZUKU
JF-Expert Member
- Nov 8, 2012
- 3,909
- 2,115
Amini alichokoza makusudi na nyerere alivumilia mengi kutoka kwa amino maana alielewa taifa linaingizwa kwenye umasikini ishu ni kwamba kila binadamu anakiwango cha uvumilivu ndio maana mzee akaona liwalo na liwe.Mkuu unaweza kuwa sawa, lakini mfano ulioutumia wa vita ya Kagera sio sawa na hauna uhalisia!
Chokochoko za Idd Amini ndizo zilizotusukuma kuingia kwenye vita ile, hata ungelikuwa wewe machukizo ya Idd Amini usingweza kuyavumilia!
Amini alifika mahala anamwambia Nyerere ni beautifull na kwamba angelikuwa mwanamke angemuoa! Wakati wa uvamizi wa kule Kagera kuna ndugu zetu waliuwa kinyama sana, mama mjamzito anachomwa kisu kikavu kikavu na kukata tumbo kutoa mtoto nje alafu wote wakiwa maiti wanatupwa mbe ya mamba!
Tena katika uvamizi ule Amini alishusha bendera yetu na kupandisha ya Uganda huku akijitapa kuwa Nyerere akisema fyoo....atamtandika mpaka Dar es salaam!
Hivi wewe uwe ni kiongozi mwenye roho ya aina gani ya kuvumilia yote hayo huku mamia ya wananchi wako hawana makazi na wengine wameuawa??
Tuache kutungia mifano simple kwa hoja nzito! ....Hatukuwa na viwanda vya kutengeneza silaha za kivita za kukabiliana na Uganda ya Idd Amin ambayo ilikuwa imewekeza sana kwenye kuimarisha majeshi yake, hivyo kuomba msaada nje lilikuwa ni jambo lisiloepukika, vinginevyo waganda wangetusambaratisha na kuchukuwa Tanzania nzima!
Ile vite ilikuwa ya makusudi na ilitegemewa tupigwe (asante MUNGU) hatukupigwa.
Mfano nilio utoa umelenga kwenye behind the scene zaidi. Au hujawahi on a mtoto anatumwa aje akuulize unaondoka lini lakini wewe unaweza dhani mtoto amejiulizia tu kumbe wazazi wake wamemtuma.