Tofauti na tafsiri ya kula na kulishwa nyama ndotoni

Tofauti na tafsiri ya kula na kulishwa nyama ndotoni

Ahsante sana mkuu nimekusoma kidogo, ila kabla sijajaribu kukujibu swali lako nakuomba kama nimekosea unisamehe sana.
Suala la kuota ndoa sihafaham ulikusudia vipi, " kuota kwamba umeifunga au imevunjika? Naomba unisaidie hapo ili twende sawa.
Kwenye kuota ndoa ni lazima kwanza ujue msingi wa ndoa ninini.

Hii ndio siri iliyopo kwenye tafsiri yoyote ya ndoto. Msingi wa kitu. Ndoa ni agano. Ndoa ni patano. Ndoa ni kiunganishi chenye kuleta matunda ya ongezeko.

Ndoto za ndoa huashiria craving for bonding that can be productive...
NB: not all dreams can have this meaning
 
Mkuu mshana jr, nakubaliana nadhana ya kufa kwasababu kipo, kifo hakihitaji sayansi kutuelezea tunaona watu wanakufa na tunazika, na kisingekuwepo nahisi dunia ingeshajaa.
Swali langu kwako.

Wewe ni mkristo unasema ni mcha mungu. Haya mambo uliyajua zamani kabla, hujamgeukia mungu?! Au una yasoma sehemu unayaleta humu au bado una practice uchawi na kumcha mungu?

Sijui unayafahamu vipi haya mambo au ni hallucinations zako tu unaziweka kwenye maandishi?!
 
Ahsante sana mkuu nimekusoma kidogo, ila kabla sijajaribu kukujibu swali lako nakuomba kama nimekosea unisamehe sana.
Suala la kuota ndoa sihafaham ulikusudia vipi, " kuota kwamba umeifunga au imevunjika? Naomba unisaidie hapo ili twende sawa.
Mara nyingi ukiongea na wanajimu wa elimu zinazohusu anga na nyota watakuambia mara zote mambo tunayoota hutukia kinyume na tulivyoota, mathalan unaota kufa kwenye ajali inakuwa kinyume chake, ama unaota mgonjwa wako amefariki ila ndo tunaambwa kwamba status yake ya kuishi ndo inaongezeka, swali likaja ikiwa hivyo ndivyo vipi kwa kumwota binti mara kwa mara kama mwandani wako?

Hii ina maana hutomwoa yeye ama?
 
Vema tukarejea kwenye mada zetu hizi... Huko siasani ni tabu tupu... Kunaweza kukufanya mtu sometimes uwe na frustration zako... Nitajitahidi nisiende tena kule.... Japo naona kama naidhulumu nafsi...

Jr[emoji769]
Dah.... Bora umestuka profesa..unaowaamini hawaaminiki...[emoji87]
 
Je ukiota nyumba yako ambayo haina hata mwaka alafu ina "expansion joints" ina maanisha nin mkuu??
 
Asante mkuu...naomba nitoke nje ya mada niulize...niliwah kuota nimekufa na nimewekwa kwenye jeneza ina maan gani ndoto hii?!
Naomba nikujibu kibliblia,

~hiyo ndoto ina maana kuna roho ya mauti ipo kwako na inazengea kukuua kabisa kiroho na wakati mwingine kimwili japo si sana.

~hapo hiyo mauti inakuwa imetumwa kwenye,uchumi,maisha ya kawaida,ardhi,uzao wako,anga nk.ss unatakiwa kwa kuiondoa kwa kufanya vitu vifuatavyo.

1.nyunyiza damu ya Yesu sawasawa na waebrania 12:24

2.Omba toba kwa kuacha milango ya ndoto wazi.yaani kutakuwa na ulinzi juu ya hilo lango.

3.okoka kama huja okoka ili kukabiliana na hiyo laana maana ipo kihalali.

4.ondoa laana hiyo kwako

5.Futa hiyo laana

6.Batilisha hiyo laana sawa na waebrania 9:10 na waebrania 2:14-15

7.Kemea pepo lililo tumwa kuiguatilia hiyo laana na kuitekeleza.

8.ombea baraka kwako na eneo ulilo liona ndotoni.tena baraka za ndani ya agano.
Ufunuo 11:12

9.Mshukuru Mungu
 
Vema tukarejea kwenye mada zetu hizi... Huko siasani ni tabu tupu... Kunaweza kukufanya mtu sometimes uwe na frustration zako... Nitajitahidi nisiende tena kule.... Japo naona kama naidhulumu nafsi.....

============================================
Dhana ya kula chakula ndotoni si jambo baya si jambo la ajabu japo kuna wakati huambatana na matatizo ya kisaikolojia kwa sehemu! Lakini lazima tutambue kuwa lazima tuote kuota ni lazima na kuna ndoto baadhi hazina maana yoyote zaidi ya kumbukumbu ya yaliyopita.....
Kuota mara kwa mara unakula ni ishara ya kutamani kufanikisha jambo fulani katika maisha, hamu ya kuwa na mahusiano , mali ama mafanikio yoyote yale.. Chakula ni uhai bila chakula uhai uko shakani hivyo kuota unakula ni dalili za kutaka kupata uhai kwenye jambo fulani
Lakini vilevile kuota unakula hutokana na kutamani chakula fulani lakini ikatokea hukukipata lakini ufahamu wako ukahifadhi ile hamu na usiku unapolala roho yako huondoka na kwenda kutafuta chakula husika na kuiridhisha nafsi tamanifu....
Sasa turudi kwenye mada... Kuota unakula nyama na kulishwa nyama... Kuna tofauti kubwa hapa
Kuota unakula nyama ni tafsiri ni dalili ya kutaka mafanikio ama kufanikisha jambo lako kwa njia ya kudhuru ama kuumiza wengine.. Yani ufanikiwe wewe lakini ukiacha wengine na madhara... Nyama inatokana na kuondosha uhai wa kiumbe hai kingine... Hii hutokana na mawazo tuwazayo bila kujua madhara yake kiroho... Kwa mfano penzi linazingua unatamani kurekebisha mambo lakini masharti ya mtaalam unatakiwa upate kuku wa kafara.... Ni kitu kama hiki... Unatamani cheo kazini, mvuto ama umaarufu nk unaambiwa dawa yake lazima itengenezwe na damu na mzoga wa mbuzi... Ni vitu kama hivi... Hivyo kupitia ndotoni hujidhihiri kwa njia ya kula nyama. Kwamba unashibisha nafsi huku kiumbe kikipoteza uhai

Sasa linapokuja suala la kulishwa nyama ndotoni... Hiki ni kitu tofauti kabisa.. Hizi ni ndoto zenye kuakisi uhalisia.. Ni ndoto za kichawi na unacholishwa ni nyama halisi kwa njia za kishirikina na nyama hizo si nzuri si nyama za wanyama tulao bali ni nyama za mizoga ya kenge nyani mbweha fisi konokono hata panya nk...
Sio nyama nzuri kwakuwa zina madawa ya kudhuru kiroho na hushibisha na hata kuvimbiza.. Hujaza tumbo kabisa na kukufanya ushindwe kula chochote.... Na tafsiri yake ni moja tu kukufunga usifanikiwe tena kwenye lolote.. Kwamba ukishakula na kushiba huwezi kula tena....

Namna bora ya kutatua tatizo hili ni kitunguu saumu na ndimu tuu... Kabla ya kulala hakikisha unalamba ndimu au kutafuna kipande cha kitunguu saumu ama vyote kwa pamoja... Kwa njia hii utakuwa umeidhibiti hiyo hali

Jr[emoji769]
Mshana Jr nipo nje ya mada yako....

Naomba unisaidie tafsiri ya jambo hili limenichanganya, toka usiku wa manane, jicho langu la Kulia, upande wa juu linacheza cheza sana, ambapo si kawaida yangu mzee, vipi tafsiri yake hapa yaweza kuwa ninini?

Maana sijielewi elewi na imekuwa too much.
 
Back
Top Bottom