Mara nyingi ukiongea na wanajimu wa elimu zinazohusu anga na nyota watakuambia mara zote mambo tunayoota hutukia kinyume na tulivyoota, mathalan unaota kufa kwenye ajali inakuwa kinyume chake, ama unaota mgonjwa wako amefariki ila ndo tunaambwa kwamba status yake ya kuishi ndo inaongezeka, swali likaja ikiwa hivyo ndivyo vipi kwa kumwota binti mara kwa mara kama mwandani wako? Hii ina maana hutomwoa yeye ama?
Good; NTAKUJIBU MKUU. wasomi wa dini zote mbili wapo wachache sana waliobakia wanasaka hela tu, na ndio maana kila kukicha watu wanagombaniana kibla ili apate tonge iende mdomoni, sio kwa kumpenda Mungu.
SUALA LA NYOTA: Mashekhe wengi wamefanya kwamba ndo sheria ila hapana huu ni ushirikina, unaambia ukitaka kuowa uowe Ijumaa kwamba siku zingine nyota ya mwanamke huyo haiko sawa, huu ni ushirikina. Hakuna siku mbaya, matendo yako ndo mabaya.
JIBU LAKO; Ndoto zote zinatokana na shetani alielaaniwa, kwa hiyo hakuna ukweli wa hilo bali huja na kukupotezea mda wako wa kumkimbuka Mungu tu.
Kwa waislam ambao ni swala tano, mara nyingi inapofika swala ya asubuhi ndoto nzuri haziishi. Lengo sala iwapite tu.
Watu wengine wanaota wanakua matajiri ila akiamka hamna kitu mfukoni, huyo ni shetani anakuchezea akili yako.
Vile vile unaweza kujikuta unafanya mapenzi na mtu hatimae kujipiga bao, pia ni shetani kakutawala kitandani.
Kuota umeowa haina maana ya kwamba utaowa karibuni bali ni mawazo yako mwenyewe uliyonayo kwenye akili yako.
Na shetani mara nyingi anacheza na akili zetu, ukiwazacho ndicho anachokufanyia unapolala.