1⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA PEOPLES SINGIDA MJINI NA MWL MWAKASEGE*
SOMO MWONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO*
TAR 4 JULY 2017
SIKU YA KWANZA.
Mungu wetu uliye hai tunakushukuru mno kwa nafasi uliyotupa siku ya leo ili tufanye kile ambacho unataka tufanye chini ya uongozi wako wa Roho wako Mtakatifu. Ahsante kwa ajili ya neema hii uliyonipa kusimama tena katikati ya kusanyiko la watu wako, na wateule wako na watoto wako. Unijalie ee Bwana katika neema hiyo kusema kile ninachotakiwa kusema, kufundisha kile ninachotakiwa kufundisha.
Ufahamu na ufunuo kutoka kwako sawa sawa na makusudi yako ili katika neno hili ee Bwana Upate mavuno, matunda na watu wako wakakuone Wewe sawa sawa na neno lako. Heshima ni za kwako na watu wote tuseme Ameeen.
Bwana Yesu asifiwe! Kichwa cha somo tulichonacho katika semina hii kinasema.
MWONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO
LENGO KUBWA LA SOMO HILI NI
Kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu.
Lengo la somo hili sio kukufundisha juu ya ndoto, ila ni kutumia mafundisho ya ndoto yaliyoko ndani ya Biblia kuimarisha uhusiano wako katika Kristo Yesu. Kumbuka hilo litakusaidia kadri tutakavyokua tunaendelea ili uweze kuona na kutathmini wewe mwenyewe kwamba kwa kadri semina inavyoendelea inaelekea jinsi Mungu anavyotaka kuona kama kila tunapojifunza kila siku kuna namna fulani yakusogea kwa Mungu zaidi katika Kristo Yesu. Pamoja na kwamba utajifunza mambo kadha wa kadha juu ya ndoto lakini bado Mungu alichokusudia ni zaidi ya hicho. Bwana Yesu asifiwe!
Na leo ni siku yetu ya kwanza na Mungu atatuongoza katika kile anachotaka tuangalie.
Fungua na mimi katika kitabu cha Mwanzo 41;1-8 “1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto.
2 Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. 3 Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto.4 Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. 5 Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema.
6 Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. 7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. 8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.
Alafu nitasoma ule msitari wa 14 mpaka wa 16 alafu nitakupa maelezo sawasawa na Roho Mtakatifu atavyoniongoza.
Msitari wa 14 unaendelea unasema
14 Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao. 15 Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri. 16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.
Kadri ninapopata nafasi ya kufundisha hili somo, ninashangaa kwamba bado hatumalizi kila kitu ambacho Mungu ameweka ndani yangu. Sijajua atakiachilia mpaka lini kwa staili hii, tumekuwa tukifundisha hili somo karibu kwa mfululizo karibu miaka miwili sasa, Sehemu hii tulikuwa hatujalifundisha kwa undani, lakini tumefundisha maeneo tofauti tofauti siku zingine siku nane na hatujamaliza na si kitu ambacho nilitegemea Mungu angenipa kukifundisha kwa sababu wakati Mungu alipokua anasema nami kwa njia ya ndoto na kwa njia ya maono mbalimbali, alipokua ananiita kwenye utumishi na sikujua kitu cha kufanya na sikujua nitapata wapi tafsiri kama vile ilivyokua kwa farao na mimi nilitafuta waganga ambao wanaweza wakafasiri ndoto nikaenda nikatafuta wanieleze maana yake nao wakajaribu kueleza maana yake baadae nilipokuja kupata maana ya hizo ndoto ndani ya Biblia nikaona kuna vitu vilikuwa vimepungua katika tafsiri yao na hawakutaka kukubali kwamba hawajui, afadhali hata wao waganga waliokuwa wanamzunguka farao walikua na ujasiri wa kukiri ya kwamba hawajui, lakini mimi niliokutana nao wakasema mimi ninajua.
Wakajaribu kunitafsiria na nikajaribu kutafuta vitabu vinavyotafsiri ndoto nilishangaa sana wakati ule sikuona kitabu cha kikristo kinachoweza kumsaidia mkristo akaweza akatizama ndoto kibiblia lakini pia sikuona kitabu ambacho kinamsaidia mtu ambae hata sio Mkristo kiweze kutafsiri ndoto kiusahihi kibiblia, Maana tafsiri ziko nyingi za ndoto na si zote zinatoka kwa Mungu kama tutakavyokua tunaendelea kuona.
Na ilinisumbua pia kuona kwamba hayo mafundisho hayakuwepo kanisani wakati ule, Sijajua kama kwenye kanisa lako mnapata mafundisho ya staili hiyo sijui. Lakini miaka ile ya 80 kule mwanzoni tulipokua tunaokoa na sehemu nilipokua ninasali na kuenda hata baada ya kukoka sikupata mafundisho ya kunisadia kwenda hata ndani ya Biblia ili niweze kujua Mungu anazungumza nini juu ya ndoto.
Na ilinichukua muda nilipoanza kumlilia Mungu kutaka kujua maana kuna vitu viko ndani ya zile ndoto ambazo zingenisaidia na sikuwa na mtu wa kunisaidia kuvitoa kule ndani niweze kupata na katika kukimbizana na Mungu usiku na mchana nikitaka kujua,
Na katika kusoma Biblia ghafla Mungu akaanza kunipa ufahamu kidogokidogo juu ya ndoto ambazo zilinisadia kujua vitu vingi sana ambavyo Mungu alikua ananisemesha juu ya wito ambao ametuitia na bado anaendelea kutufundisha mpaka leo, siwezi kukwambia najua kila kitu,
Najua vitu vingi lakini sijui kila kitu na katika hivyo vitu ambavyo Mungu amenipa kuvijua ameniruhusu kuanza kufundisha hivi karibuni miaka kadhaa kama miwili mitatu hivi na nitaenda nalo taratibu kadri Mungu anavyonipa niweze kulifundisha kwenye maeneo tofauti tofauti.
Bwana Yesu asifiwe.
Kwahiyo ninataka nikueleze hiyo kitu ili uweze kufahamu hiki kitu kilitokea wapi na Mungu anaporuhusu kidogo na kujifunza uweze kuelewa maana yake nini. Katika siku hii ya kwanza kwa kusoma hizi ndoto mbili za farao nataka kuzungumza na wewe kama vitu vinne tu vya utangulizi ambavyo ni …
GHARAMA AMBAZO ZINAWEZA ZIKAMPATA MTU KWA KUTOKUJUA KUTAFSIRI NA KUIOMBEA NDOTO KIBIBLIA
Kwahiyo kwa lugha ya kawaida tungesema gharama ambazo zingeweza kumpata Farao haijalishi ni kiongozi, haijalishi ni mtu wa kawaida, mchukulie farao katika ngazi hizo mbili, Farao kama kiongozi Farao kama mtu wa kawaida kabisa kuna gamharama ambazo kama asungepata tafsiri sahihi hizo gharama zingekuja kwenye maisha yake,
Ziko nyingi lakini nimeona nikuwekee mtaji kidogo wa mahali Roho mtakatifu anataka tuendelee.
Ya kwanza
1.KUTOKUJUA KILICHOKUSUDIWA KITOKEE KATIKA MAISHA YAKO.
Sasa tuna tizama picha ya farao lakini nataka uone huu ujumbe kama ni ujumbe wa kwako binafsi.
Mwanzo 41;28 na 32
Msitari wa28 unasema hivi
28 Ndivyo nilivyo mwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.
Mwanzo 41 :28
Angalia huo msitari vizuri
Huyu ni Yusufu anaongea, sasa angalia msitari wa 32
32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.
Mwanzo 41 :32
Kwahiyo kama unaota ndoto inajirudia ,.kuna sababu nyingi lakini sababu mojawapo ni hiyo hapo kwamba hicho kitu unachokiona kwenye ndoto kitatokea sasa usipojua namna ya kuomba kisitokee hilo ni jambo lingine tutalizungumza polepole,
Lakini ni njia moja wapo ya kukwambia ya kwamba kitatokea.
Angalia kile kitabu cha
Ayubu 33:14 - 15
14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Kwahiyo ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu anasema na mtu na usiposikia katika ndoto ya kwanza anakuletea ndoto mara ya pili, hiyo ni Ayubu sura ya 33 msitari wa 14 na 15, kwahiyo anakurudishia mara ya pili, saa nyingine hata mara ya tatu,
Saa nyingine hata mara ya nne.
Ndoto inajirudia, inaweza ikajirudia kwa kufanana inaweza ikajirudia kwa tofauti kidogo kama vile ambavyo unaona ya farao ilivyojirudia unaona katika ndoto ya kwanza kuna ngombe na ndoto ya pili kuna masuke, ukiitizama unaweza kufikiri ni ndoto mbili,
Lakini hizo ndoto zina ujumbe unaofanana ukiendelea kujifunza namna ya kutafsiri ndoto ni rahisi sana kuona kitu cha namna hiyo, saa nyingine wanaponiambia nimeota ndoto hii, nimeota ndoto hii saa nyingine inaweza jirudia usiku huohuo, anasema nikalaa alafu nikaota tena ndoto nyingine alafu nina mwambia hiyo ni ndoto moja, ina ujumbe unaofanana alafu namweleza ujumbe ulioko.
Saa nyingine mtu anaweza akaota usikiu huo akaota ndoto moja akakaa saa nyingine siku nyingine akaota au baada ya wiki mbili tatu akaota tena akiweza kunieleeza hizo zote mbili saa nyigine ninaona kabisa ndani yake, namwambia aanhaa hii ndoto inafanana na ile ya kwanza inamaanisha kuna kitu ambacho hukuona kwenye ile ya kwanza,
Mungu anajaribu kukusemesha tena kwa sababu ndivyo Bilia inavyosema ya kwamba atakusemesha mara ya kwanza, mara ya pili hata kama hujali,
Huyu ndugu anaeitwa Farao alipoamka angalia kitu alichotoka nacho USIKU, Biblia haitu ambii ni saa ngapi aliota ndoto, alipo ota ndoto akaamka akalala akaota tena ndivyo msitari wa tano unavyo tuambia
5 Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama,
Aka amka akalala akaota ndoto mara ya pili hiyo inahusu masuke, alipoamka Biblia inasemaje, alidharau akasema kumbe ndoto tu.
Na kama vile unavyoota ndoto alafu na wewe mwenyewe unasema afadhari kumbe ndoto tu unaiacha hapo mpaka asubuhi alipoamka roho ikafadhaika ambayo nitakueleza maana yake nini baadae,lakini nilitaka uone ya kwamba kuna kitu ambacho Mungu alikua amekikusudia kwa ajiri ya eneo lile a dunia wakati ule, si tu kwa ajiri ya misri, lakini pia unaweza uka fuatilia kwenye Biblia utagundua ya kwamba mpaka nchi za jirani zilipata shida ya namna hiyo, na kama unasoma Biblia yako vizuri utagundua ya kwamba alipoota ndoto ilichukua miaka saba ndipo njaa ikaja, kwa sababu kwenye chakula kingi asingeshituka,
Lakini ile njaa iliyokuja baada ya miaka saba ya shibe ile ndio iliomshtua , ile ndio kwahiyo miaka saba ya shibe si rahisi sana ukaona lakin Mungu alikua anajaribu kuzungumza nae vitu vita kavyokuja baadae, hata Yusufu ndicho alichonwambia anasema Mungu anazungumza na farao atakayoyafanya hivi karibu sasa “ hivi karibu” ni miaka saba ijayo lakini unaona kabisa kipindi cha chakula kilianza mara moja.
Kwahiyo kama Mungu anatumia ndoto kama ni mojawapo ya kukusemesha juu yakitu kinachokuja mbele yako na kama usipojua tafsiri yake, kama ni ndoto inayojua.moja kwa moja na tafsiri yake, kadri tutakavyokua tunaona kuna ndoto zingine zinakuja zina tafsirinmoja kwa moja huhitaji kufuatilia wala mahali pengine popote inazungumza moja kwa moja
Angalia kile kitabu cha
Mathayo 1: 18-24 18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri
20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, 23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. 24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;
Nilitaka uone ya kwamba hii ndoto haikuhiataji tafsiri ilikua na melekezo moja kwa moja, Haikua na mafumbo ndani haikua na fumbo lolote ndani ni maelekezo moja kwa moja,
Sasa ziko ndoto za namna hii lakini ziko zingine zina mafumbo yake na usipojua namna ya kufahamu utakosa kitu kikubwa sana k kilichoko mbele yako.
Gharama ya pili.
2. KUTOPATA MSAADA WA MUNGU KWA AJIRI YA KUJIANDAA JUU YA ULICHOOTA
kitabu cha
Mwanzo 41: 31 na 3433 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.Mstari wa 34a Farao na afanye hivi
Nilitaka uone hilo “Farao na afanye hivi" akapewa maelekezo pale ya kitu cha kufanya, sasa cheki uelewe vizuri hayo maelekezo hayakuwepo ndani ya ndoto kwa kuota, yalikuweko ndani ya ndoto kama ujumbe , ujumbe utaupata tu saa wakati unatafsiri kama umefichwa.
Gharama ya tatu ni hii
3. KUNA UWEZEKANO MKUBWA KWA KUYUMBISHWA IMANI YAKO.
Kumbukumbu la Torati 13:1-4 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye._
Sasa unaweza ukaendelea kusoma hapo. ila Ngoja turudi Mwanzo 41: 8 “Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo”.
Kwanini Farao aliwakimbilia waganga, ni kwa sababu walikuwa wamejihudhurisha mbele katika jamii kuwa wanaweza wakatafsiri ndoto. na kwa nini aliwafuata wenye hekima ni kwa sababu walijihudhurisha mbele ya jamii kuwa wanaweza wakatafsiri ndoto. Wakina Yusufu waliokuwepo lakini walikuwa gerezani na yule ambaye alikuwa anajua habari za Yusufu yaani mnyweshaji wa mfalme alipotafsiriwa ndoto yake akiwa jela na alipopata nafasi ya kurudi akasahau. Ametoka jela na amerudishwa kwenye nafasi yake sawa sawa na alivyotafsiriwa na Yusufu akasahau.
Biblia inaanza kwenye Sura ya 41 Kitabu cha Mwanzo “ Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto” ina maana katikati ya wale watu walioota wakiwa gerezani ili kuwajulisha ya kwamba kuna mwingine ana roho ya Mungu anaweza akatafsiri kwa katika nchi ya kwenu .Ilipita miaka miwili na alinyamaza kimya.
Mpaka pale waganga na wachawi na wenye hekima waliposhindwa kutafsiri ndipo unamuona yule Mnyweshaji alisema sasa nimefahamu kosa langu na ndicho alichosema. Angalia ule mstari wa 9 Kitabu cha Mwanzo 41 “Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema, Nayakumbuka makosa yangu leo”. Lakini ilipita maika miwili.
Tatizo la kutafsiriwa ndoto na mtu wa imani nyingine haiko kwenye tafsiri bali ilo kwenye ujumbe. Ngoja nijaribu kusema tena nasema hivi “Tatizo la kutafsiriwa ndoto na mtu ambaye ni wa imani nyingine tatizo halipo kwenye tafisiri balo kwenye ujumbe.
Yalinipata mimi haya wakati Mungu alipokuwa ananisemesha Mwanzoni kabisa sitakuja sahau. Niliota ndoto niko ndani ya chumba, akaja mtu akapita kwenye mlango na namtazama mimi nimekaa kwenye kiti na akaja kwangu moja kwa moja amevaa nguo nyeupe ndefu, saa hiyo sijaokoka aliponisogelea akatoa mkono wake na nilipotazama ulikuwa na jiwe jeupe alafu akaning’iniza ilikuwa na kamba , ilikaa kama yai lakini niliona kama ni jiwe. Akaleta moja kwa moja kama vile anataka kunipa na kwa hiyo nilikunjua mikono yangu kama vile nataka kupokea. Akataremsha lile jiwe karibu mpaka linanifikia akanyenyua juu alafu akanitazama akasema “dhambi zimezidi duniani”.
Akageuka kueleka mlangoni nikaamka
Nilipoamka ile ndoto ilinifadhaisha, sasa cheki mahali nilipoenda nilikimbilia moja kwa moja kwa mganga na yule mganga alikuwa wa imani nyingine. Nilipofika nilimueleza na alikuwa ni mtu Mzima kabisa nikamwambia mzee “Nimeota ndoto na ile ndoto imenisumbua sana” kwa hiyo nikamsimulia ile ndoto na akanitazama, akaniambia yule aliyekuja alikuwa ni malaika na lile jiwe ni tuzo kwa ajili yako na hawezi kukupa si kwa sababu duniani dhambi zimezidi bali ni kwa sababu wewe ndio umezisha dhambi. Sasa nikamuuliza kuwa “sasa ndio nafanyaje”?. Sasa sikia, hana namna ya kunielekeza kwa Yesu, sasa akaanza kunifundisha kutubu kwa dini yao. na ilikuwa ni shule kabisa alifundisha kutubu, na yale maneno siwezi kusema hapa na sijayasahau mpaka leo.
Biblia inasema si kila mwotaji wa ndoto,hata yale mambo aliyo yaota na yametukia. Usikimbilie kusema haa hii kitu ni sahihi. Biblia inasema cheki ujumbe unaokuja unakuleta karibu na Mungu katika Kristo Yesu au unakupeleka mbali?. Kama unakuwa mbali biblia inasema usiyasikilize maono ya muotaji wa hiyo ndoto na hata kwako wewe mwenyewe. Imenichukua muda mrefu sana nikihangaika sana nikaja nikaokoka baadae na nikaanza kuomba Mungu anioneshe kwa kuwa alikuwa ananionesha kitu gani.
Baadae nikaja nikakuta ndani ya biblia iko “Yeye ashindaje nitampake jiwe jeupe” Kasome biblia yako. utaona iko kwa Barua kwa kanisa la Peligramo andika ..na jina ambalo hakuna anayejua na nitampa jina jipya
“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea” Ufunuo wa Yohana 2:17
kwahiyo ina maanisha ningekuwa na mtu wa kunieleza kanisani nisingeenda kwa mganga. kama haya mambo ninayokueleza ningefundishwa kanisani au Jumapili au kwenue bible study au mahali popote ingenisaidia. Lakini sikuwa na huo msaada na msaada uliokuwepo ni waganga.
Na unaweza ukoona kabisa shida sio tafsiri bali shida ni ujumbe maana kulikuwa hamna namna anaweza kunileta kwenye toba kwa Yesu. Hana namna ya kunileta kwenye toba kwa Yesu kwa hiyo hakunileta kwa Yesu bali alinipeleka kwenye toba ya kwao. Ahsante Yesu kwa sababu neema ya Mungu ilinikamata na sikuzamia huko. Lakini watu wengi sana wanazamia huko na hiyo ndiyo inayowavuruga katika sehemu mbali mbali na imani yao. Bwana Yesu asifiwee.
Okay, ninapoandika kwenye notes zangu na ninaposoma habari za Farao, na habari ya kuyumbishwa nimeiweka kwenye (mabano) kwa sababu Farao alikuwa na imani ja wachawi na waganga na miungu yao na Mungu akamletea ndoto. na Mungu hakumletea ndoto Yusufu bali alimletea Farao kwa sababu ndoto ilimhusu Farao. Lakini sasa Mungu hawezi akaruhusu huyo mganga awe na vyote viwili. Yaani kutafsiri na kutoa ujumbe. wakanyimwa vyote viwili yaani tafsiri na ujumbe. Nia yake Mungu ni kitu gani alikuwa anatafuta ni kumuondoa Farao kwenye imani yake kwa waganga ili amtafute Mungu aliyehai. na kwa sababu hiyo ilibid lazima amlete mtu mwemye Roho wa Mungu.
Na Yusufu alijua ili asijeaweke imani yake kwa Yusufu alipoambiwa kuwa nasikia wewe ukisimuliwa ndoto unaweza ukatafasiri kwa hiyo nimeona nikusimulie ndoto ili uweze kutafsiri. lakini Yusufu alijibu “Yusufu akamjibu Farao, akisema, *Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani” Mwanzo. 41:16.
Ili ajue ya kwamba yuko Mungu na ilibidi aelekezwe macho yake kwa Mungu kitu gani kilitokea. ilipofika anaambiwa tafuta mtu mwenye akili atakaye simamia masuala haya na maelekezo haya. Farao alisema “Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake”Mwanzo. 41:38
Ina maanisha aligundua wale wachawi na waganga waliokuwa wamemzunguka kuna vitu walivyokuwa wamepungukiwa. na walijua kuwa watu wengine wana Roho wa Mungu ambao wanaweza mumsaidia. inaweza ikawa ni ngazi ya familia yako inategemea umejizungushia watu gani wa kukusaidia.
Unaweza ukaona nilikuwa nimezungushiwa watu gani wa kunisaidia na saa hiyo nilikuwa chuo kikuu. na watu wengi sana wamepotea kwa sababu hiyo kwa sababu hakuna msaada wa kibliblia wa Mungu wa moja kwa moja unaosema kuwa haya masuala ni halisi na yanaweza yakavuruga imani za watu. Bwana Yesu asifiwe… Ngoja nikueleze jambo la nne.
Gharama ya nne.
4.KUTOKUJUA UOMBEJE AU UNAOMBAJE JUU YA KITU KILICHOKUJA AU KITAKACHO KUJA NA NDOTO AMBACHO KINAWEZA KUGUSA ROHO, NAFSI AU MWILI WAKO.
Daniel 2 katika sura hii tunamuona Nebukadreza akiota ndoto na mbaya zaidi aliota ndoto iliyomsumbua na alipoamka asubuh akawa amesahau. Na alipoamka kama kawaida akawa ametafuta waganga na wachawi waliokuwepo Babeli wakati ule. Katikati ya watu wenye hekima wakina Daniel walikuwepo. Bahati Mbaya sana wale waganga na wachawi walipoitwa mbele ya mfalme kwa ajili ya kutafsiri ndoto akina Daniel hawakuitwa.
Walipofika pale Nebukadreza aliwaambia nimeota ndoto naomba tafsiri nao wakasema tueleze ndoto. Akasema nimesahau na akawaambia mnieleze ndoto niliyoota na tafsiri yake. wakamwambia hamna kitu cha namna hiyo. wakamwambia tueleze ndoto uliyoota na sisi tutakupa tafsiri yake.. akasema msifanye mchezo nataka mnieleze ndoto niliyoota na tafsiri yake lasivyo ntawashughulikia ninyi na familia zenu. Ntawaua kabisa akasema lazima mniambie ndoto niliyoota na tafsiri yake , lakini wao walimwambia hapana hii haiwezekani ni miungu peke yake ambayo haikaagi na wanadamu.
Sisi tunachoweza ni kuwa tueleze ulichoota tutakutafsiria .Kasome biblia yako ilitolewa amri wauawe . Ilipotolewa amri yule askari wa Nebukadreza aliyepewa amri ya kwenda kuwaua biblia haisemi ila kwa namna fulani alienda kwa Daniel. Kwanini hakuanza mara moja na kuwaua, ila biblia haituambii ila tunaona alienda kwa akina Daniel kuwambia kuwa na wao wako kwenye list ya kuuawa kwa sababu walikuwa kwenye ngazi ya wenye hekima. Daniel aliuliza hii hasira kali ya mfalme namna hii imetoka wapi? tumekosea nini. Si ndio akaelezwa baada ya kuelezwa sasa..soma hapo chini
Daniel 2:16-18 “Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli”
Ninachokataka nikuoneshe hapa ni kuwa akina Daniel waliijua siri ni kuomba na Katika kuomba kunahitaji muda kwa hiyo ni lazima utenge muda wa kuombea ndoto unazoota. wengi sana wanazidharau ndoto wanazoota na hawajajua kitu kilichoko ndani yake. Tunaona Daniel akiongea na wenzake akisema “tupe muda” na ukitaka kujua mkono wa Mungu ulikuwepo pale tunaona hasira yote ya mfalme ilitulia maana angeweza kusema kama mmeshindwa kunitafsiria na angemwambia yule askari wake kuwa maliza hawa jamaa hawahitaji muda ndio maana wana hekima, ndio maana ni waganga na ndio maana ni wachawi. wauawe lakini Daniel alienda akiwa amefunikwa na nguvu za Mungu akamwambia mfalme naomba muda. Ulikiwa ni muda wa kufanya nini? ulikuwa ni muda wa kwenda kuombea ile ndoto.
Hakumwambia kila mtu bali alitafuta wenzake wawili watatu ambao walikuwa na mzigo pamoja na yeye na wanaweza wakaomba. Na aliwashirikia ili waombe ukiendelea kusoma utaona biblia inasema “Mungu akawajibu kwa njia ya ndoto na Mungu alimwaotesha Daniel ndoto ile ile ambayo Nebukadreza aliota lakini hakuishia hapo alimpa na tafsiri yake na ujumbe uliokuweko ndani yake.Bwana Yesu asifiwe..haleluyaa haleluyaa.
Ni nidhamu ngumu kidogo lakini ukiendelea nayo itakusaidia. unaona hii shida kwa Farao pia, Hakimbilii kuomba bali anakimbilia kutafuta tafsiri.
Ni watu wengi mpaka leo wakiota ndoto hawakimbilii kuomba bali wanakimbilia watafsiri na si kila mtafsiri atakueleza sahihi, si kila mtafsiri atajua tafsiri na si kila tafisiri utapewa na ujumbe saa hiyo hiyo zingine unapewa ujumbe saa hiyo hiyo mtu anakueleza na Mungu anakupa ufahamu saa hiyo hiyo. Lakini zingine inabid ung’ang’ane uombe mara ya kwanza mara ya pili. Zingine zinanichukua hata wiki nzima ninaomba juu ya hiyo ndoto kila siku baada ya wiki ghafla ninapata unaweza ukafikiri ni kama mtu fulani hivi kanishushia kitu ndani na napata ufahamu kabisa kuwa ni kitu gani kiko ndani.Lakini unahitaji nidhamu ya kibiblia.
wewe unafikiri ni kwa nini Farao alipoamka aladharau ndoto na alisema “Kumbe ndoto tu”.Kitu gani kilitokea, kulipokucha asubuhi roho yake ikafadhaika. ile ni roho iliyokuja na ndoto na ni ndoto ambayo imekuja na roho wa Mungu uwe na uhakika roho Mtakatifu anaingia ndani na haondoki mpaka au umepata au umekataa kwa hiyo ile kumfadhaisha kuwa asiidharau hii ndoto imekuja kwa ajili yake. Hiki kilikuwa ni kiashiria kilichokuwa kinamsukuma yeye kutafuta uso wa Mungu. sasa yeye kilipomjia alitafuta watu badala ya kutafuta uso wa Mungu. sasa Najua si nidhamu ambayo watu wengi wanaipenda lakini nataka nikusidie maana unaweza ukaja ukakaa mahali ambapo hutakuwa na mtu wa kumuuliza na au utamwambia na atakuambia kuwa sijui. Sasa unaweza jikuta umepoteza ujumbe mkubwa sana kwa ajili yako, na kwa ajili ya familia yako na usijue kitu cha kufanya.
Hata kama ndoto ibilisi kaipenyeza kama tunavyoona katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 13 :1-3 .Usije ukafikiri kuwa ukienda mahali pengine penye msaada wa roho kipepo ambayo inatoa tafsiri usije ukafikiri kama ulivyoambiwa kwenye kitabu cha kumbu kumbu la Torati kuwa chunga ujumbe unaopewa. utabaniwa tu hapo na utaelezwa tafsiri yake na utabanwa kisawa sawa ni Roho Mtakatifu peke yake ndiyo anaweza akakusaidia .Bwana Yesu asifiwe.
Kuna mtu mmoja aliponisikia nafundisha mahali aliniandika ndoto akisema “ Mwalimu nimeota ndoto na nipo kwenye shehere na hiyo shehere ina chakula kingi sana kimefunikwa na kitambaa juu, juu ya kile kitambaa kulikuwa na fuvu la kichwa na kikafunuliwa kile chakula na watu waliokuwepo pale wakala kile chakula na yeye. Pamoja na kwamba kile chakula hakikuwa kitamu mdomoni lakini nakumbuka tu nilikula. Lakini kile kitambaa kilichokuwa juu yake kilichokuwa na picha ya fuvu la kichwa sijakisahau. basi akaamka kutoka ndotoni na hakuja kitu cha kufanya .Huyu mtu aliyeota ndoto hakumaliza hata mwezi kiu yake ya kwenda kanisani iliisha, hamu ya kuomba ikaisha, Kiu ya kusoma biblia iliisha na hakujua kuwa ni matokeo ya ndoto ile mpaka aliposikia nikifundisha somo hili la ndoto. alafu akaniambia tena baada ya miezi kadhaa tena kupita akaota ndoto nyingine.
Sasa amewezaje kuunganisha ndoto zingine na inamaanisha hapa katikati aliota tena ndoto nyingine akaota mtu kaja na damu anataka kumnywesha kwenye ndoto akakataa. na sasa aliniuliza Mwalimu sasa ndio naombaje sasa maana hizi ndoto zinanitesa.
Na niliposoma nilielewa mara moja maana yake nini na yote hiyo ni kwa sababu nimesoma kwenye biblia na kujua maana yake nini.
Kwa sababu kile chakula hakikuwa sherehe ya kawaida. Mungu alikuwa anamuonesha katika ulimwengu wa roho kitu kinachosukwa na adui kwa sababu si kila chakula unachokula kwenye ndoto ni kizuri. kuna chakula cha kipepo, kuna chakula ambacho kinaweza kikawa kinakuonesha juu ya agano lililoko au mpango wa adui kukuingiza kwenye agano. Biblia inasema mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Bwana. kwa hiyo ina maanisha ambacho unaweza ukapewa na kikavuruga imani yako. na Mungu anakuonesha kuwa kuna kitu katika ulimwengu wa roho umepewa na ni kitu kinatokea.Bwana Yesu asifiwe.
Kilichomsaidia wakati wameona ameanza kukwepa kwenda kanisani walijua amepoa kabisa kwa hiyo walimtetea damu ili wamwingize kwenye agano kwa sababu ile damu angekunywa ingemuingiza kwenye agano. unasema unapata wapi ipo kwenye biblia, Yesu alisemaje “Damu mnayo kunywa ipo kwenye agano”.Ahsante Yesu alikataa, na zile ndoto zilimpitisha mahali pagumu kidogo maana zile ndoto zilikuwa zinafanana.
nilienda mahali pengine mwingine aliniambia kuwa “Mwalimu nimeota ndoto na kuna chakula nimekula, sikutaka kula kile chakula na wamenilazimisha kula kile chakula na nikamuuliza kimetokea kitu gani baada ya kuota hiyo ndoto. alisema siwezi kuomba kanisani naenda na sielewi kile wanachofundisha kanisani. Nikamwambia weka mkono wako juu ya kinywa chako na nilipoachilia damu ya Yesu pepo likalipuka ndani yake saa hiyo hiyo nikakemea na akafunguka. lakini hakujua ya kwamba alipolishwa ndani ya ndoto kuna kitu kilikuwa kinaingia pia.
Mwingine aliota ndoto kaumwa na nyoka kwenye kidole cha pili cha mguu wake na maumivu yalikuwa makli sana kwenye ndoto na azindika na alipozinduka akakuta anasikia maumivu kwenye mguu, akatoa shuka yake alafu akamulika na tochi. na aliona pale alipoumwa na nyoka panatoa damu. na aliona halisi, na kesho yake alipoenda kansan kuombewa walikemea pepo la mauti likitoka ndani yake. lakini ni kitu kilichotokea kwenye ndoto.
mwingine aliota ndoto yuko porini kakutana na mama mmoja na alipewa karatasi. alipoamka ana ile karatasi mkononi. Lakini amepewa kwenye ndoto. na usipojua kitu cha kufanya ni hatari sana.
Kila kimoja unachoota kwenye ndoto majibu yapo kwenye biblia katika upana wake. Biblia inasema kusikia huja kwa neno la Kristo kwa hiyo hakikisha unakuwa na neno la kutosha ndani yako.
Mwingine aliota anakatwa na msumeno kwenye kidole gumba na makali ya msumeno ndiyo yanaanza kuingia akashtuka kwenye ndoto akaweka mkono juu ya kile kidole na kuomba. Baada ya mwezi mmoja pale alipoota anakatwa kidole pamekuwa peusi na akaniambia sasa Mwalimu ni kitu gani hiki. nilimwambia ulikemea na roho ilitoka ila kuna sumu iliingizwa.
Nilienda mkoa mmoja na mtu mmoja aliniambia Mwalimu nimeota ndoto nimepigwa risasi kwenye ndoto nikamwambia okay, nikamuuliza je risasi ilitoka huko kwenye ndoto akisema hapana. Nikamuuliza tena je ulipigwa upande upi? na akaniambia mguu huu na nikamuuliza je ulipoamka ukijisikiaje akasema mpaka leo nina maumivu upande huu.
Naweza nikakusumulia na kukusimulia.
Mwingine aliota ndoto usiku ni mdada kaibiwa pochi (wallet) si unajua akina mama wanakuwa na pochi mbili yaani ile ndogo na ile kubwa yake. sasa aliibiwa ile pochi(wallet) ya ndani iliyokuwa na hela sasa asubuh anafika ofisini anashangaa kanga’anywa nafasi yake ya kazi na kapewa mtu mwingine. yeye alipewa mahali ambapo kuna mshahara kidogo na hamna marupurupu. na aliniandikia hiyo ndoto ila shida yake ni nini ni kwa sababu hakuomba usiku saa ile ameota ile ndoto. na Mungu alikuwa anamsemesha kuwa si halali wewe kunyang’anywa kipato chako yaani unaibiwa si halali kwako kunyang’anywa hiyo nafasi.
lakini hakujua na hamna mtu aliyemweleza tafsiri yake. kwa hiyo ililazimu tuanze kuomba kwa style nyingine kabisa. ili aweze kurudi kwenye nafasi yake.
Sasa kuna mwingine alinisikia nae nikisimilia alisema sasa ndio nimeelewa kuwa na mimi niliibiwa pochi (wallet) yangu iliyokuwà inapesa ndani na kufika ofisini nilibadilishiwa kazi. na alipewa kazi ambayo haiko sawa na kitu alichosomea na mshahara wake ukaenda chini na hamna maelezo waliyompa na kila akiuliza maswali wanakuwa wakali. Labda wangejua wanajua hizi siri mapema wangekua kitu cha kufanya.
Ngoja niulize hapa wangapi ambao hapa wameota ndoto wamekula chakula kwenye ndoto na hawajajua kitu cha kufanya nyosha mkono
sasa si kila chakula unachokula kwenye ndoto ni kibaya.
Biblia inasema hata Yesu alikuwa chakula pamoja na wanafunzi wake. kwa hiyo kuna chakula cha Bwana. na kuna chakula cha mashetani. pia ukienda kwenye biblia kuna kula chakula ambacho ni kukuonesha kuwa siku zako za kuishi zimeisha au unaarifiwa na Mungu kwamba ndugu yako ameamua kuondoka na ameomba Mungu akamtishie maisha yake. kwa hiyo utaona kama ni baba yako anakula chakula na unaona akikurushia sahani kamaliza kula. Kasome biblia yako Zaburi ya 91 “Nitakushibisha kwa wingi wa siku “ kwa hiyo anayesema nimeshiba sio yule anayetoa chakula bali anayekula hicho chakula. kuna ndoto zingine hazina shida ila zingine zina shida.
Biblia inasema kwa wana wa Israel walipokuwa wametengeneza ndama walikula na kunywa na kucheza hakikuwa chakula cha kawaida. ilikuwa ni meza ya mashetani.
sasa kama umekula chakula usichokijua kwenye ndoto ambacho kwa jinsi ya kawaida usingekula ujue kuwa kuna kitu kinapitishwa. sasa kamuulize Petro kwanini aliletewa maono ya wanyama na yeye alisema siwezi kula kitu najisi. katika ulimwengu wa roho kuna kitu alikuwa analetewa na kama wasingetafsiri katika biblia ingekuwa ngumu sana kujua.
Wangapi hapa ambao wameumwa na Nyoka au wamefukuzwa na nyoka kwenye ndoto.
Glory to God Glory to God.
Ngoja tufanye zoezi hapa, kama uliota ndoto unakula chakula na hujajua ni kitu gani weka mkono wako kwenye kidevu chako. kama uliumwa na nyoka nyika mahali umeumwa.
Kuna mtu aliumwa na nyoka kwenye pete ya kidole chake cha ndoa na ndoa yake ilikufa baada ya mwezi. na hakujua mpaka aliposikia nafundisha. mwingine aliota nyoka kapita tumboni kwake na baada ya pale siku za mwezi zilivurugika kuanzia pale.
Kuna mwingine aliota nyoka kaingia kwenye mguu wake na kapotelea huko. Hakujua kitu cha kufanya hadi aliponisikia nikifundisha na alikuwa ananisikiliza kwa njia ya mtandao. na nilipokuwa nakemea na mguu wake ukaanza kutetemeka ndipo alikuja kuelewa kuwa kumbe haikuwa ndoto ya kawaida kuna kitu kimeingia ndani yake maana alikuwa anaishiwa nguvu upande wa kushoto kwa hiyo kama ni mkono au mguu shika. nataka tufanye zoezi ili tuone.
Kama kuna nguvu za giza zilipita na pepo ambalo limekaa huko ndani kuna namna nitakavyoomba yataondoka tu mengine kwa kupiga kelele na mengine kimya kimya. Mungu atakusemesha baadae au sasa hii baada ya maombi haya na utapata ufahamu wa kitu cha kufanya.
kwa sababu kitu cha msingi hapa kama utakuwa unaelewa hapa pole pole na tutaangalia kwemye lango la ndoto kuwa kuna mahali vitu vinapita. kama ni chakula ina maana imepita kwenye mdomo. Kama ni viungo kawaida au mguu nilikuwa nasimuliwa na mtu mmoja nilikuwa nimeenda kufundisha habari za ndoto na nikawa nafundisha habari za kuombea lango la ndoto na yeye akaanza kuombea lango la ndoto ya kwake.Ghafla usiku akaota ndoto.
Ameenda mahali kwenye kijiwe anachokula na mtu anayeuza chakula pale siku hiyo baada ya kuona chakula anachouza ghafla aliona madudu fulani. sasa anaona yeye tu wengine wote hawaoni. na yeye akashtuka na akaanza kusema kumbe nakula chakula hapa kwenye ndoto kumbe si kizuri. Sasa anajaribu kuwaelesa wemzake kuwa msile kile chakula jamani hapo au hamuoni sasa wenzake wakawa hawaoni.
Yule anayeuza chakula akamfuata na akamwambia kuwa wewe kama umeona ondoka kimya kimya usiniharibie biashara hapa. na akajua kuwa Mungu anamsehesha kuwa asiende tena kula chakula pale.
MAOMBI
Mungu katika jina la Yesu, Ahsante kwa sababu ya nafasi hii na asante kwa sababu ya neno lako ee Bwana wewe peke yako ndio ulifuatana na wanafunzi wako kila mahali wameenda kotekote biblia ndivyo inavyotuambia wakihubiri lile neno na wewe ukilithibitisha lile neno. kwa ishara zilizofuatana nao.
Nami naomba ee Bwana sawa sawa na neno ulilonipa katikati ya watu wako na watoto wako nikiwa hapa singida ee Bwana tunaomba mkono wako wenye nguvu upate kutusamehe na kuturehemu sawa sawa na neno lako, mahali popote ambapo nguvu za giza zilipata mlango na kupitisha vitu vya kwake tunajua lango la ndoto uliliumba wewe kwa ajili ya mwanadamu kwa ajili ya kusudi lako. lakini Ee Bwana adui analitumia kwa ajili ya kupitisha vitu vya kwake.
Ninaomba toba kwa ajili yangu na kwa ajili ya kila mmoja aliyeko mahali hapa anayeombewa na tunaomba mahali hapa Ee Bwana upate kuturehemu katika jina la Yesu Kristo. ninaomba toba ee Bwana kwa ajili ya maovu yote katika familia ambayo kuna maagano ambayo yanawafutailia ambayo yalifanyika kwenye vyakula au yalifanyika kwenye vinywaji ee Mungu katika jina la Yesu Kristo. hizo nguvu za giza zinajaribu kuzungumza na hawa watu na kuwaambia hawa ni wa agano hili na zinajaribu kuwaingiza katika agano hilo au wameingizwa kwenye agano na kwa sababu hiyo kuna mapepo ambayo yamepewa kufuatilia kila eneo ee Mungu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth wewe uonae siri ninaomba rehema zako tunapoomba toba kwako na msahama kwa ajili ya dhambi zetu na dhambi za kila mmoja ninaomba ee Bwana toba kwa ajili ya uovu wa waliotutangulia na kutuingiza katika maagano yanayotufuatilia katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Tunaomba toba kwa ajili ya jambo lolote ambalo lilitoa nafasi owa adui na akapita kwa roho ya nyoka na kuingia katika miili ya watu ja kuwagonga na kuachilia sumu yake katika damu ya Yesu Kristo. na nyunyiza damu ya Yesu kuanzia kwenye kinywa chake na damu ya Yesu Kristo katika kinywa chake ipite ee Bwana kwa mtu wa nje na mtu wa ndani na kusafisha sasa inaondoa dhambi na roho mbali mbali ndani ya watu ee Bwana katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth ×5 Nina nyunyiza damu ya Yesu kwenye utumbo mkubwa na mdogo mahali ambapo giza zimebana kwa damu ya Yesu Kristo wa Nazareth.
Nanyunyiza damu ya Yesu katika Fikra mahali ambapo ibilisi amebana. nanyunyiza damu katika roho yake ambapo nyoka amengonga huyu mtu katika ndoto kwa damu ya Yesu Kristo ninaachilia moto wako na kuondoa hiyo sumu na kufuta kila uhalali wa adui kushambulia. katika jina la Yesu.. endelea kuomba.
Biblia inasema palipo na msahama pana kuwekwa huru. palipo na msahama pana ukombozi Ahsante Mungu wa sababu unasamehe. kwa mamlaka niliyopewa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth tunakwenda kinyume kabisa na nguvu zote za mapepo na nguvu zote za za giza zilizopita kwa njia ya hizo ndoto tulizozitaja. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth. pepo majini na roho zote za uchawi zilizopita kwenye mwili wake toka kwa jina la Yesu × 3 endelea kuomba Toka jina la Yesu Kristo kemea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Tukiwa tumefunika macho nauliza hili swali muhimu. Unajua hujaokoka Yesu si Bwana na mwokozi wa maisha yako au ulikuwa umeokoka na ukarudi nyuma na hujapata nafasi ya kutengeneza. Nataka niombe kwa ajili yako jion ya leo mahali popote ulipo.
Soma sala hii.
Ee Mungu baba nimekuja mbele zako, ninaomba unipokee, ninatubu kwako dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu.Ninaomba toba kwako. Ninaomba unisamehe, ninaomba unirehemu, ninaomba unitakase kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu. Ee Bwana Yesu nimefungua moyo wangu, nakukaribisha sasa ingia ndani yangu kwa uweza wa Roho wako uwe mwokozi, uwe kiongozi, uwe Bwana Kwangu.
Kuanzia sasa na siku zote unisaidie nidumu ndani yako siku zote za maisha yangu. Shetani asinishinde, majaribu yasinishinde, dhambi isinishinde katika jina la Yesu. Nikuishie wewe peke yako katika jina la Yesu.
FUATISHA MAOMBI HAYA NA SOMA KWA IMANI
Mungu katika jina la Yesu. Ninakushukuru kwa sababu ya uaminifu wako. Ahsante ee Bwana kwa ajili ya wale waliofanya sala hii kwa mara yao ya kwanza na wengine mara ya pili na wengine mara ya tatu mara ya nne. Lakini kwa vyovyote vile ee Bwana neema yako ya wokovu imefunuliwa juu yao ahsante kwa ajili ya kila mmoja ahsante kwa ajili ya uzima wa milele ulioko ndani yao. Ahsante kwa majina yao kuandikwa ndani ya kitabu cha uzima.
Ahsante ee Bwana kwa Yesu Kristo kuingia ndani yao upate kuishi na kuweka matunda na upate kujifunua . Hicho ndicho tunachoomba ee Bwana. Tembea pamoja nao ukiwapa ushindi wa maisha ee Bwana katika jina la Yesu tembea pamoja nao upate kujifunua wapate kukujua wewe na kukuishia wewe katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth tunakwenda kinyume kabisa na nguvu zote za giza na nguvu zote za mapepo na roho zote za majini na maagano yote ya kipepo ambayo yatataka kuinuka ili kuzuia nyendo zao hawa watu katika Kristo Yesu. Tunafuta maagano yote ya kipepo kwa damu ya Yesu yafutike kabisa na nguvu za giza tunakuamuru achia hatua za watu hawa achia roho zao, achia nafsi zao, achia miili yoa sasa, achia maisha yao, uchumi wao na viatu vyao sasa katika jina la Yesu.
Pepo tunakuamuru toooka. Hawa sio wa kwako tena kwa jina la Yesu. Tooka toka toka toka toka kwa jina la Yesu. Achia tumbo lake achia kifua chake, pepo toka. Ee Bwana tunawakabidhi kwako watunze popote watakapokuwa katika jina la Yesu Kristo. Na kila mwemye pumzi aseme Ameeen.
Kama umefanya hii sala mara ya kwanza ndio umeokoa tayari. Kama ulikoka ukarudi nyuma basi Mungu amekusamehe na wewe jisamehe na akisamehe anasahau kwa hiyo usijihukumu kabisa
Somo katibu cha HONGERA KWA KUOKOKA NIMEKUWEKEA LINK PALE JUU.
GLORY TO GOD. TUONANE TENA KIPINDI KIJACHO KATIKA MFULULULIZO WA SEMINA HII HAPA SINGIDA NA WATUMIE NA WENGINE.
=GLORY TO GOD GLORY TO GOD=