Tofauti ya baby shower ya Diamond Platnumz na Mark Zuckerberg

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Waafrika mbumbumbu sana inapofika suala la kuiga mambo ya kizungu hadi kufikia kuwa kichekesho, sasa baby shower ya mtoto mtu kafanya ya makungwi. Ndo utajua tofauti ya mtu mwenye pesa na mtu anayefilisika.

We jamaa utakua una matatiza sehemu tena makubwa sana, yaani unataka kuwalinganisha Mark Zuckerberg na Diamond, yaani kabisa? Maskini wa Mungu ukute eti na wewe umeenda shule kabisa then unakuja na haya mambo.

Si kosa lako lakini.
 
Sasa hebu ona mark Zuckerberg ni billionea mkubwa sana ila baby shower yake hajatumia hata elfu 50, wakati diamond ni kama maskini tu kwa Zuckerberg lakini katumia kama millioni 100 hv kwenye baby shower huoni ni ulimbukeni wewe jamaa?
 
Ni kama jamaa hukumuelewa OP alimaanisha nini "yani pamoja ya unilionea wa Mark lakini amefanya hiyo "baby shower sjui" simple kwanza inaonyesha kama ni kwake na pia hakuwa na mambo mengi
Sasa hebu ona mark Zuckerberg ni billionea mkubwa sana ila baby shower yake hajatumia hata elfu 50, wakati diamond ni kama maskini tu kwa Zuckerberg lakini katumia kama millioni 100 hv kwenye baby shower huoni ni ulimbukeni wewe jamaa?
Jamaa hapo uliposena hajatumia hata elfu 50 umezingua [emoji23] 50,000 ni sawa na 21 USD, natumaini budget ya Mark haiwezi kuwa chini hivyo
We jamaa utakua una matatiza sehemu tena makubwa sana, yaani unataka kuwalinganisha Mark Zuckerberg na Diamond, yaani kabisa? Maskini wa Mungu ukute eti na wewe umeenda shule kabisa then unakuja na haya mambo.

Si kosa lako lakini.

Kama tunavyojua wabongo/wa Africa tunapenda sifa.. . Mark yupogo simple maana hata tshirt huvaaga ya rangi moja

Kingine unaweza kukuta hiyo baby shower imemuongizia Dai faida na sio hasara.
 
Wewe jaribu kuchunguza tu hizo picha za baby shower ya Zuckerberg, mapambo ya karatasi na hizo juice za baby bottle hazifiki hata elfu 50[emoji1787][emoji1787]
 
KILA MMOJA ANAFANYA JAMBO KULINGANA NA ANAVYOJISIKIA HAIJALISHI ANA KIPATO AU MALI KIASI GANI.WANASEMA RAHA JIPE MWENYEWE
Lengo la baby shower ni kupeana vizawadi kwa ajili ya mtoto mtarajiwa kama vi nguo nguo, na kutangaza jinsia ya mtoto mtarajiwa. Na mara nyingi huwa ni simple indoor event ya ki home home. Najua diamond ushamba tu umechangia. We fuatilia hata mastaa wengi duniani baby shower huwa ni event ndogo sana hainaga mbwembwe kabisa
 
Kila mtu anaishi apendavyo hela za kwake anazitumia apendavyo kwa vipaumbele vyake sioni haja yoyote ya kufatilia maisha ya mtu ni kupoteza muda Tu wa kufanya mambo yako...
Ni ushauri tu ila unaweza kusaidia kubadili fikra hasi
 
Tajiri hata akiwa simple tu ila tayari yeye ni tajiri na anajulikana kua yeye ni tajiri tayari,

Masikini ndio hujitutumua ili nao waonekane wamo pia, But sio mbaya kila mtu anaishi apendavyo,kwani kuna formula ya jinsi ya kufanya hiyo Baby shower?

Mimi ndio mara yangu ya kwanza kusikia kua kumbe hua kuna kitu kinaitwa Baby shower!
 
Sasa hebu ona mark Zuckerberg ni billionea mkubwa sana ila baby shower yake hajatumia hata elfu 50, wakati diamond ni kama maskini tu kwa Zuckerberg lakini katumia kama millioni 100 hv kwenye baby shower huoni ni ulimbukeni wewe jamaa?

Basi nitakua siku note vizuri point yako kwa hapo naomba nisamehe
 
Kweli sikumuelewa jamaa ndio maana nimemwimba samahani
 
Lakini yote ni kwamba dai ndo anaweza akawa najua faida au hasara aliopata maana kama kuna watu au kampuni aliingia nao mkataba ili iweze kugharamia kila kitu na kujitangaza kibiashara atakuwa amepata faida na kinyume chake
 
Mimi nimepata bahati ya kufanya kazi na hawa wazungu na kufika kwao, ukweli hawa wenzetu wana nidhamu kubwa sana ya pesa haijalishi ana kiasi gani yeye anatumia tu panapohitajika. chukulia mfano mdogo lakini ndio ukweli. mkienda kwenye sherehe ya kula buffet sisi sahani itabeba kila kitu kama kuna kuku sijui wali hata kama chura tia tu katika sahani akikaa ndio sasa anachagua cha kula na kingine kinabaki kinatupwa. hawa jamaa akienda kuchukuwa chakula anachagua tu anachokitaka kula basi na utakuta sahani yake nyeupe kala alichokichukua. Hii ina reflect maisha yao toka utotoni, tusione hawa wa Japan mfano mambo yao na tabia zao wanafundishwa toka wakiwa vidudu. Tuko busy na show off na kushindana na vivuli vyetu. Sisi tunaona matajiri wa kweli Tz wako kimyaa utasema hawaishi nchi hii.
 
Best comment.
 
Faida!!!?
Aisee huendi mbinguni!! Ha ha aah!
Salama lakini Mkuu?
 
We jamaa utakua una matatiza sehemu tena makubwa sana, yaani unataka kuwalinganisha Mark Zuckerberg na Diamond, yaani kabisa? Maskini wa Mungu ukute eti na wewe umeenda shule kabisa then unakuja na haya mambo.

Si kosa lako lakini.

duh

nyie verified users, muwe makini na kejeli maana unaweza jidhalilisha
 
Diamond ni mwanamuziki na pia ni celebrity number 1 hapa nchini ,katika kukuza biashara yake ya Muziki lazima ayakuze na maisha yake ya kawaida ili watu wapende na wazidi kumfuatilia kila siku kwa sababu kwa kufanya hivyo thamani yake inaongezeka mara dufu.

Mark Zuckeberg sio Mwanamuziki wala sio mtu anayetegemea maisha yake ya kawaida kukuza thamani yake au ya biashara yake kwa ujumla, ndio maana Mark anaweza akavaa shati la rangi moja mwaka mzima ila isiwe issue kabisa kwake wala biashara yake haitaathirika hata kidogo lakini Jay z au Kanye West hawawezi kufanya hivyo japokuwa wameachwa mbali sana Mark Zuckeberg kwenye upande wa utajiri.

Next time ukitaka ufananishe watu/vitu tafuta ulinganyo kwanza , maana mwisho wa siku utakuja kuonekana huna uelewa na vitu vidogo vidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…