Diamond ni mwanamuziki na pia ni celebrity number 1 hapa nchini ,katika kukuza biashara yake ya Muziki lazima ayakuze na maisha yake ya kawaida ili watu wapende na wazidi kumfuatilia kila siku kwa sababu kwa kufanya hivyo thamani yake inaongezeka mara dufu.
Mark Zuckeberg sio Mwanamuziki wala sio mtu anayetegemea maisha yake ya kawaida kukuza thamani yake au ya biashara yake kwa ujumla, ndio maana Mark anaweza akavaa shati la rangi moja mwaka mzima ila isiwe issue kabisa kwake wala biashara yake haitaathirika hata kidogo lakini Jay z au Kanye West hawawezi kufanya hivyo japokuwa wameachwa mbali sana Mark Zuckeberg kwenye upande wa utajiri.
Next time ukitaka ufananishe watu/vitu tafuta ulinganyo kwanza , maana mwisho wa siku utakuja kuonekana huna uelewa na vitu vidogo vidogo