Tofauti ya baby shower ya Diamond Platnumz na Mark Zuckerberg

Ukiuliza nini unaambiwa nakuza/nalinda brand [emoji3] jambo dogo shuguli kubwa matusi kama yote
Watu wakipata ahueni ya maisha tabu sana hasa sisi weusi
 
Ingeleeta maana sana kama ungelinganisha baby shower ya diamond na msanii mwenzake wa nje (mzungu)
 
Kwaio hujaona kwamba huyo mke wa zuckerberg kajaza watu wenye asili ya asia tu au
 
"cyrustheruler,
Hivi Zurckerbeg ile T-shirt yake pendwa haibadilishwi au anazo nyingi?


Anazo nyingi ila zina rangi mbili ni kama zinaelekeana elekeana hivyo hivyo, kuna siku aliweka picha ya sanduku lake la nguo la ukutani. Asilimia kubwa hata viongozi wakubwa wasiopenda kuchosha akili mapema kabisa asubuhi kufikiria nivae nini leo huwa na nguo maalumu za kuvaa kama sare kwa wiki nzima na ndo maana utaona baadhi ya watu wazito hupendelea kuvaa nguo za aina moja. Mfano wa baadhi ya watu ni rais mstaafu wa marekani Barack Obama alikua anabadilisha rangi ya tai tu pamoja na bilionea Richard Branson.
Wengi wao hukwepa kuwa na decision fatique mapema kabisa asubuhi maana Maisha yao yanaongozwa na kufanya maamuzi mengi kwa siku juu ya majukumu yao wanayotekeleza na kuyasimamia.
 

We bwege kweli, kwahiyo maana ya mimi kufafanua ni ipi?
 
 
Ally Kiba tu ndio sio MSHAMBA, hata huyo Mark nae alifanya ndogo ya nini kama ni sherehe sherehesha haswa kama hutaki garama acha kama kiba alivyo mpokea wa bi Amina kimya kimya.
 
Were acha masihala hamna familia yenye matumizi mabaya ya fedha kama ya akina kardashian,juzi kati Kylie Jenner kafanya birthday ambayo imejumuisha watu 30 katika boti ya kukodi imekatika dola mil 1.So usione mkusanyiko wa watu wachache ukazani hela inayotumika ni ndogo.

Yale mapumziko binafsi ya Jiga na familia yake ktk boti ukipigiwa mahesabu yake unaweza ukakuta Diamond katika hiyo Baby shower yake hayajagusa hata robo.We mtu shingoni tu ana cheni thamani yake zaidi ya dola laki 3,ana Maybach thamani yake 8mil dollars ,yote haya anayafanya sababu ya branding yake.

Tena hiyo familia ya Kardashian kila kitu kwao ni biashara ndio wanao ongoza kwa SHOW OFF hollywood yote na ndio maana maisha yao yote wameyaweka kwenye TV.

Diamond hizi show off ndizo zinazo mpa mikataba ya PEPSI, Coca Cola,DSTV,Parimatch,GSM,Nice One ili azitangaze bidhaa kwani marketing ya bidhaa yoyote inahitaji mtu anaye trend.

Mark Zuckerburg yy haitaji hizi SHOW OFF zaidi ya hapo atajikita katika kucreate new technology ili apige hela,ndio maana yy mwaka mzima anavaa nguo za rangi moja kwake haina athari kwenye biashara yake.
 
We bwege kweli, kwahiyo maana ya mimi kufafanua ni ipi?
Kama ulifafanua ulifafanua kibwege sana.Halafu hueleweki upo upande gani.Ndio maana ume-apologize baada ya kuona umejichanganya kibwege.

Hongera sana.
 
Sasa hebu ona mark Zuckerberg ni billionea mkubwa sana ila baby shower yake hajatumia hata elfu 50, wakati diamond ni kama maskini tu kwa Zuckerberg lakini katumia kama millioni 100 hv kwenye baby shower huoni ni ulimbukeni wewe jamaa?
Nafikiri kuna kitu unakisahau, linapokuja suala la matumizi ya fedha yawe makubwa au madogo kuna mambo makuu mawili.

1. Kiasi cha fedha ulichonacho

2. Maamuzi yako juu kiasi cha fedha ulichonacho.

Zuckberberg ana kiasi kingi lakini anaamua kufanya matumizi madogo ndani ya uwezo wake vile vile diamond ana kiasi kidogo kulinganisha na Zuckberg lakini anafanya matumizi ndani ya uwezo wake tu.

Kumbuka kipimo sahihi cha matumizi ya fedha si tajiri fulani, ulimbukeni na ushamba ni kufikiri pesa yako uitumie kama tajiri fulani.

As long as you earn more than what you spend no problem.

Kwa nchi yenye uchumi mdogo kama wetu inapotokea mtu kama Diamond anafanya matumizi makubwa inasaidia sana kiuchumi maana mzunguko wa fedha unaongezeka na kulainisha grisi mnyororo wa vyuma vya umasikini. Kama wote matajiri na maskini watafanya shughuli za elfu 50 kama udaivyo alivyofanya Zuckberg basi ukumbi kama wa Mlimani City hautapata wateja.
 
Sawa mtunza kabati wa Zuckerberg
 
Hivi nimeongelea birthday au baby shower mbona hunielewi, birthday ni sawa ila kuwa muelewa
 
Hahaaaaahaaaaa...
Mkuu umenifurahisha sana hapo mwishoni,maana hata nami haya mambo ndio nayajua sasa.
 
Hivi nimeongelea birthday au baby shower mbona hunielewi, birthday ni sawa ila kuwa muelewa
Kwa hiyo kutumia gharama kubwa kwenye birthday sawa,ila kwenye baby shower sio sawa?

Haya msome khloe kadarshian huyu hapo,gharama zake alizotumia ktk baby shower yake ambayo imedhaminiwa na Amazon.


Kama hujui hata Diamond events zake zote anadhaminiwa na GSM na wadhamini wengine.
 
Sasa hebu ona mark Zuckerberg ni billionea mkubwa sana ila baby shower yake hajatumia hata elfu 50, wakati diamond ni kama maskini tu kwa Zuckerberg lakini katumia kama millioni 100 hv kwenye baby shower huoni ni ulimbukeni wewe jamaa?
Mtu pesa katafuta kwa jasho lake why apangiwe kuzitumia, hapo ndipo wabongo tunapokwama [emoji23] ina maana mkuu wewe umeumia sana kuliko ndugu zake wa karibu
 
Sure. Watu hawashangai kuna harusi lilipigwa India, wizikid akalipwa zaidi ya 500M + za kibongo ili awepo tu pale kwa wiki.
 
Sasa hebu ona mark Zuckerberg ni billionea mkubwa sana ila baby shower yake hajatumia hata elfu 50, wakati diamond ni kama maskini tu kwa Zuckerberg lakini katumia kama millioni 100 hv kwenye baby shower huoni ni ulimbukeni wewe jamaa?
Hata diamond angekuw mark angefanya hivyo na hata mark angekuwa diamond anvefanya hivyo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…