econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Baada ya Mh Mbowe na Wenzake kuachiliwa kumeibuka watu wanaodai na Sabaya naye aachiwe. Msingi wa madai yao Kama Mbowe ameachiwa kwanini na Sabaya asiachiwe. Naomba nitoe tofauti ya kesi ya mbowe na Sabaya.
1. Kwanza, kesi ya Sabaya ilishafika hukumu na akapatikana na hatia na kifungo Cha miaka 30. Ila kwa Mbowe ndio kwanza alikuwa anaanda ushahidi wake kujitetea.
2. Pili, kwa sehemu ilipokuwa imefikia kesi ya Mbowe alikuwa haitaji msamaha bali kufutiwa mashtaka maana hukumu ilikuwa bado haijasomwa. Ila kwa Sabaya kwasababu alishahukumiwa yeye anahitaji presidential pardon Yani huruma ya Rais.
3. Tatu, kwenye kesi ya mbowe kulikuwa hakuna ushahidi wa nguvu zaidi ya assumptions , lakini kwenye kesi ya Sabaya ushahidi upo dhahiri na victims walitoa ushahidi wao.
4. Nne, kwenye kesi ya Sabaya Sabaya amekata Rufaa, Hapo msamaha utasubiri mpaka rufaa isikilizwe na maamuzi kutolewa. Na Kama Rufaa itakazia hukumu, basi Sabaya itabidi asubirie huruma ya Rais.
5. Tano, Tatizo jingine Sabaya ana kesi nyingi Sana, hivyo itabidi ksubiri kusikiliza kesi zote za Arusha na Moshi, ndipo uamuzi wa kumsamehe utolewe. Ila Kuna kesi zingine zimekaa vibaya, Kama ubakaji.
6. Mwisho, kesi ya Sabaya imefunguliwa baada ya Rais kuingia madarakani 2021, lakini ya Mh Mbowe ilianza kabla ya 2021, Yani mwaka 2020 ndio maana Mbowe amepachikwa kwenye kesi katikati.
Mwisho, tumuombee Sabaya naye atolewe kwa msamaha wa Rais.