Nyamwi255
JF-Expert Member
- Dec 2, 2022
- 4,848
- 12,776
Hadi nastaajabu jinsi mume wangu mtarajiwa alivobadilika na kuonesha upendo ambao sijawahi kuupata kutoka kwa mtu mwingine isipokuwa wazazi.
Iko hivi, huyu kijana nimekutana naye nina kama mwezi na wiki, na hii ni baada ya kujitunza kwa muda mrefu. Lakini toka tumeingia kwenye mahusiano, hakuwahi kunipa hata hamsini mbovu na mimi sikuwahi kumuomba.
Nilikuwa najipa moyo nikasema labda ananipima, lakini mpaka unatimia mwezi sijaona akinipa chochote.
Sasa wiki moja iliyopita amenishangaza baada ya kunambia anataka kunioa. Binafsi sikuamini, nikajua labda ananitania, kumbe alikuwa serious na ameshajiandaa.
Basi nilipomuona yuko serious, nikampa muongozo ndani ya wiki hii akapeleka posa.
Sasa toka anipose amekuwa akinipa pesa na kunihudumia mpaka nashangaa, yaani naletewa zawadi kila siku na leo kanambia niseme nataka mahari Tsh ngapi. Madai yake anasema hataki mwezi wa saba uishe kabla hatujaoana.
Binafsi nafarijika sana na namuomba Mungu ndoa yetu ipite salama.
Kuna situation fulani ka raha sana nakapitia.
TBH, I am so excited nimeamua ni ka share na ninyi.
Mwanaume akiwa na malengo na wewe kumbe anakuhudumia hivi 🤔.