UBALOZI WA TANZANIA LONDON, UNITED KINGDOM pt 1
Madereva wa watumishi wa ubalozi.
Ukitazama structure ya Jiji la London na ukiwa unafanya Kazi kwenye City, hakuna ulazima zima wa kuwa Na Gari let alone kuwa Na Dereva wa kukuendesha.
Jiji ambalo meya wake anatembea kwa baiskeli, Waziri mkuu na Chancellor of exchequer mara kwa mara wanasafiri kwa Train.
Tufanye Hesabu kidogo:
Mshahara wa dereva wastani ni £9 kwa saa. Congestion charge(gari kuingia kati kati ya jiji) £11 kwa siku. Mafuta £15 kwa siku.
£9 x 7.5 masaa ya kazi kwa siku =£67.5 kwa siku x 5 siku za kazi kwa wiki= £335 kwa wiki.
£11x 5 siku=£55 kwa wiki
£15x5 siku= £75 kwa wiki
Jumla £465 kwa wiki x 52 wiki kwa mwaka= £24180x 3200 change ya pound kwa shilings= 77,376,000 shillings kwa mwaka.
Nawafahamu wafanyakazi wanne ambao wana Madereva.
77,376,000 x 4 watumishi=
309,504,000 tsh kwa mwaka gharama za kuendeshwa na gari kwa watumishi wa 4 wa ubalozi.
Nyumba wanazoishi:
Baadhi ya watumishi wa Ubalozi wanaishi maeneo ya Hendon, Finchley na Golders Green, ukiingia kwenye website ya
http://www.rightmove.co.uk ukiangalia rent ya nyumba ya vyumba vi 3 maeneo hayo ni kati £2,000 hadi £3,000.
Council tax(kodi ya serikali za mitaa) Maeneo hayo ya Hendon ni Band B ambapo wanatakiwa kulipa £857 kwa mwaka.
Ikiwa kama serikali ndio inawalipia kodi watumishi wake hesabu ina kuwa hivi.
£2000 x 12= £24,000 + £857 Council Tax=£24,857.
Ikiwa kama watalipiwa umeme na gesi, umeme na gesi wastani ni £30 kwa wiki x 52=£1560 kwa mwaka.
£24,857 x 3200 pound kwa shilling = 79,542,400 shilling kodi ya nyumba 1.
£1560 x 3200 pound kwa shilling = 4,992,000 shilling gharama za umeme na gesi.
Watu 4 for sure watakuwa wanalipiwa kodi na serikali.
79,542,400 x 4 (balozi, naibu, admin na mwambata) =
318,169,600 kwa mwaka.
Kama wanalipiwa gas na umeme 4,992,000 x 4 =
19,968,000 kwa mwaka.
Hitimisho:
Nyumba na gari watumishi wa 4 jumla ni
627,673,600 shilling kwa mwaka.
Tuanze na hivi kwanza halafu tutaendelea na pt 2.