Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Shule ya Muhimbili iliyoko barabara ya umoja wa mataifa ina tatizo la maji machafu ambayo sasa ni miaka yanamwagika kupitia geti la shule.

Naomba wahusika washughulikie kero hii sugu haraka. Afya za watoto na wapita njia zisiendelee kuhatarishwa.
 
Hakuna adha ambayo huwa inanikera kama adha ya barabara.

Ukitoka Dar es Salaam kuja au sehemu zingine kuja kigoma ukifika eneo la Nyakanazi ndo utaanza kuona adha ya kusafiri kuja Kigoma. Barabara haipitiki, vifusi njiani karaha tupu. Hivi kigoma ni sehemu ya Tanzania? Umeme wa uhakika hakuna, maji safi na salama shida!

Wabunge wa Kigoma kazi yenu nini? Kula mishahara na posho tu au? Mmeisimamia serikali kwa lipi? Mbona mambo in yaleyale Kigoma.

Rais wa watu, Dr. Pombe Magufuli awamu hii tukumbuke na sisi. Kweli karne hii bado watu wa mkoa huu tunasafiri na mifuko ya rambo ili tufike tuendako walau mabegi yetu yasishikwe na vumbi sana alooo! Mikoa mingine unaweza kuhudhuria harusi kwa kutokea nyumbani ukiwa umevaa suti yako na sio Kigoma.

Magufuli tusaidie baba wabunge wetu wachumia tumbo tu, wao husafiri kwa ndege tu.

Nawasilisha!
 
Kero yangu nyingine ni jinsi barabara ya Bagamoyo kipande cha Mwenge/Tegeta inavyoharibiwa.

Mvua zilizonyeesha miezi ya nyuma ilishusha uchafu na mchanga eneo la Africana ambao mpaka Leo haujaondolewa na unaendelea kushindiliwa kwenye lami.

Eneo la Tanki Bovu kuna lami ilimwagikia barabarani haijaondolewa.

Wanyama wanapokufa barabarani hawaondolewi, wataoza na kukaukia hapo hapo. Harufu inakuwa mbaya na chances za kupata maradhi zinaongezeka.
 
Wanyama wanaochungwa au kujichunga wenyewe mijini ni kero kubwa.

Eneo la Kunduchi kuna mbuzi na ng'ombe wanaodaiwa hawana mwenyewe. Usiku wa manane unaweza kushtukia ngombe huyo kalala barabarani. Mchana ndio kutwa kuvuka barabara. Ukichepuka kidogo unakutana na wale wenye wachungaji.

Naomba wahusika washughulikie tatizo hili.
 
Hapa ARUSHA kuna mapolisi wanatembea na kagari kadogo.

Hao mapolisi ni hatari sana wakikushiaka labda unakula mrungi au unavuta bangi ama wamekushika na kitu chochote kile ambacho kiko kinyume na sheria.

Cha kwabza wakikushika wanakupandisha gari lao alafu wanakusachi wanachukua hela zote au wanchukua hicho walicho kukuta nacho, alafu wanakutoa nje kabisa na mji wanaenda kukuacha huko.

Tena hii kazi inafanywa usiku, yaani hawa jamaa ni hatari kwa maana wanapokupelea kurudi pia ni hatari sana ukikutwa hauna cha kuwapa wanakupeleka polisi au unazunguka nao.

Hivi tunapotoa habari kama hizi usalama wetu unakuwaje au ndo kampango ka serika kukamata watu tunaojua mambo yao? Usalama wetu unakuwaje,
 
Jipu ofisi ya Manispaa ya Ilala kitengo cha ardhi dirisha la malipo ya leseni za makazi na kuongeza muda.

Mfano leseni yako inasoma kodi yako ni Tsh. 12,700/= pale utaambiwa ni Tsh. 32,700/= pia kodi ya kuongeza muda wa leseni ni Tsh.5,000/= ila Wao wanatuchaji tsh. 10,000/= ilhali risiti tunapewa mbili za Tsh. 5,000/= ukiuliza hawana majibu mazuri wanasema kasubiri kwenu majibu utapata utakapo taifishiwa Mali yako.

Nisaidieni nijue kodi imepanda lini?
 
Jipu la mishahara hewa ni hatari sana, hasa idara ya Elimu.

Hilo ni duka la wakuu wa idara hizo (maafisa Elimu) wakimgawia baba lao Mkurugenzi. Wanawajua vizuri wanaopokea mishahara wakati hawapo kwenye vituo vya Kazi.

Vyeti feki hasa kwenye idara ya Elimu.
Kuna walimu wengi wanafanya kazi kwa vyeti visivyo vyao. Watu tuliomaliza nao kidato cha nne wakiwa wamefeli, leo tunafanya nao kazi wakiwa na majina mengine.

Admn ni PM kwa evidence, sioni kitufe cha PM hapa.
 
Nyumba za Watanzania zaidi ya 8000 zilizojengwa kwa gharama kubwa na maeneo nyeti zilizogaiwa kwa wajanja wachache kama wakina Mussa na Sundi huku Taifa likiingia gharama ya mamilioni ya fedha kuwalipia watumishi wake hotel za kifahari na nyumba za kupanga ni jipu kubwa linalohitaji kutumbuliwa na kutibiwa.Kwa ufupi:#WeNeedBackOurHouses!!
Ili kujua ukubwa wa jipu, ni vema ukatoa gharama za ujenzi wa hizo nyumba, fedha zilizotumika kwa watumishi kuishi hotelini nk.

Je, fedha za ununuzi wa hizo nyumba zilienda mfukoni kwa nani?
 
Ikiwa haikuwa rahisi kupiga picha hiyo elfu tano uliiona kivipi?
Pamoja na kukosekana ushahidi kutokana na mazingira yanavyokuwa wakati wa tukio Traffic police kupokea rushwa kutoka kwa madereva.

Kwa mfano, kwenye barabara iendayo Gongolamboto maeneo ya Banana Traffic police husimamisha gari ndogo na daladala. Madereva wamekwishajua kwamba wanachohitajika kutoa ni elfu tano.

Kwa hiyo dreva hutoka na elfu 5 na kumfuata Traffic police nyuma ya gari na kukabidhiana hiyo pesa. Ktk mazingira hayo si rahisi mtu aliye ndani ya gari kuweza kupiga picha!

Ifike mahali wananchi waelewe kwamba mtoaji na mpokeaji wote wana makosa!
 
Kuna magari (Hiace) toka Mh Magufuli achukue hatua kudhibiti upotevu wa mapato hasa kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi zimekuwa zikipitisha mzigo usiku wa manane mkoani Mara kutoka nchi jirani Kenya. Watu hawa hushirikiana na Polisi na baadhi ya maafisa wa TRA.

Mfano, kila Jumatano na Ijumaa, Hiace zaidi ya tano huvuka mto Mara toka Tarime kwenda Serengeti usiku huku kukiwa na vizuizi vya polisi Nyamwaga na mto Mara.

Wanaojihusisha na biashara hii wengi ni wafanyabiashara ambao ni viongozi wa Chama changu CCM.

Mamlaka za Wilaya ya Serengeti zinajua ila hawana ubavu wa kuchukua hatua kwa kuwa wanakula pamoja kwa muda mrefu.
 
Jipu: Shirika la kimarekani la International Rescue Committee linavyopuuza wazawa na kuajiri wafanyakazi wa kimataifa kwa ngazi hata za kawaida kabisa ambazo tunaelewa wataalamu hao wapo inchini.

Shirika hili limezidi dharau
 
Kuna mtendaji wa kijiji cha Rung'abure anaitwa Sendy, huyu jamaa ni dizaini ya wale mchwa wakubwa tena wala vyuma.

Amekuwa na rekodi mbaya sana toka aingie kazini amesimamishwa mara nne kwa makosa tofauti.

Mwaka 2012 akiwa kijiji cha Bonchugu alikamatwa baada ya kuuza vocha za ruzuku ya pembejeo za wakulima na kupiga mpunga, baadae kesi ikaunguruma na kutokana na magumashi zilizokuwepo kipind kile anachokaga na kurudishwa kazini.

2. Mwaka 2014 baada ya kurudishwa kazini akapangiwa Ngoreme, huko akampa mwanafunzi wa shule mimba na akasimamishwa kazi, ajabu baadae akarudishwa kazini na kupangiwa Kijiji cha Nyamerama kama VEO. Huko nako alituhumiwa kwa kuuza ardhi /shamba la kijiji na baadae wakagombana na Mwenyekiti wa kijiji kabla ya kusogea kijiji cha Rung'abure . Hapa napo amefanya madudu mengi. Kwanza amejipa madaraka ya kugawa fedha za TASAF kinyume na taratibu na amekula Ile asilimia inayobaki kijijin na amekutwa na DC - Serengeti akikiuka huo utaratibu, pili DC amemkuta akikiuka taratibu za kazi, siku hiyo DC alifika ofisini kwake ikiwa saa tano asubuhi na kwenye daftar la mahudhurio alikuta huyo VEO amesaini ameingia kazin saa moja na nusu asubuhi na kuandika ametoka saa kumi jioni. Mda huo DC anashuhudia hayo ilikuwa saa tano asubuhi.

Juzi tarehe 28/3/2016 tena huyo VEO amedai vocha za ruzuku ya pembejeo za wakulima zimepotea tena.

Huyo ndo Jacob Sendy almaarufu John Sulusi anaetumia cheti cha mtu mwingine Jacob Tuguro kufanya figisufigisu serikalini. Na hapa ndipo Serengeti ambapo DC anashuhudia uozo kama huu halafu anapiga kimya.

Tuone kama Mh Magesa Mulongo atayaweza haya.
 
Swala la kodi linahitaji ubunifu tu...

Tunajua ukiwa na kampuni kila mwisho wa mwezi unapata retuen ya VAT.....nadhani hili swala la dai risiti lingefanikiwa sana kama Mh. Rais angepitisha return kwa watumiaji wa mwisho pia kama ilivyo kwa wenye makampuni...

Hapa ungewekwa mfumo wa kurudisha angalau 5% ya hiyo 18% kwa mtumiaji kupitia mitandao ya simu na serikali ichukue 13% tu.

Tunaelewa ni kwa kiasi gani watanzania wengi walivyonunua simu za mikononi, kwa kupitia makubaliano ya serikali na makampuni ya simu, mnunuzi anaweza akatuma namba ya risiti Yake aliyonunulia kitu ikiwa imekatwa 18% na kuweza kurudishiwa hiyo 5%.

Nina hakika kwa kufanya hivi serikali itakuwa imeleta muamuko mkubwa wa kudai risiti kwa wananchi.

Nawasilisha....
 
Askari wa Usalama Barabarani eneo la Sayansi Kijitonyama Jijini Dar ni jipu.

Wanalazimisha uwape rushwa. Wamebuni namna ya kupokea rushwa, unaambiwa uingie kwenye gari (ieleweke hilo gari linakuwa la trafiki, muda mwingi linakuwa limepaki hapo), Ukiingia kwenye gari wanalock, unatoa rushwa unaacha kwenye gari, wanakufungulia unaondoka.

Mimi nimefanyiwa hivyo so nina uhakika ninachokisema.

Tutafika tu.
 
Jipu jingine ni Mahakama ya Kazi...

Utakuta kesi zinakaa miaka 10 baada ya mfanyakazi kushinda na kuna sera inayoitwa "kukazia hukumu" .... halafu baadaye mfanya kazi anaambiwa hukumu haitekelezeki.

Sio mtaalamu wa sheria za kazi lakini hapa kuna mchezo kati ya mawakili, mahakama na shirika au kampuni iliyoshtakiwa...
 
TRA tembeleeni duka la madawa ya binadamu linaitwa The Pharmacy, hapa jengo la Ben Mkapa, hawatoi risiti za EFD.
 
Ni kwanini miji mingi hapa Tanzania kuna maeneo mengi yamejengwa kiholela?

Nadhani serikali imeajiri maafisa ardhi katika Halmashauri. Je, kazi yao ni nini?

Miji mingi haipendezi, imejengwa kiholela sana.
Mfano, DSM ukiona maeneo mengi utadhani ni mahindi yamechanganywa na kunde, maharage, njugu, mbaazi n.k yakapikwa na kusongwasongwa
 
Naombeni wadau kuuliza kama kuna utaratibu wowote wa kuanzisha nyumba za ibada maeneo mbalimbali.

Nasema hivi kwa kuwa kwa sasa mtu ukiamua hata kufungua kanisa au msikiti sebuleni mwako watu wanakuja wanapata ibada.

Mimi naona kama ni kero kuwa kwa jamii kwa sasa.
 
Jipu lipo kwa mwekezaji wa kuku katika Shirika la elimu Kibaha.

Mwekezaji wa kuzalisha kuku, hawa ni waarabu toka Misri, wanawatumikisha watanzania kama watumwa, wanawadharau watanzania, wafanyakazi wa kitanzania wakishtaki kwa Polisi, Polisi wanapewa hela hata hawashughuliki nao.

Waarabu hao huwaonesha ishara na kuwadhalilisha wanaume kingono kinyume na maumbile.

Jipu hili Waziri Mkuu aje azungumze na vibarua mengi watasema na hataamini wanavyofanyiwa watanzania.
 
Back
Top Bottom