Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Jipu lingine lipo mgongo ni kwa mheshimiwa rais.

Vitengo vya TRA vinafanya kazi kama vilipewa target ya kuingiza kiwango flani cha pesa kwa siku au wiki. Yasipofikiwa malengo basi mkuu wa kitenge hicho anageuzwa jipu. Kero yangu, nimeingiza magari ya huduma kwa jamii.

TRA waliniambia yana exemption moja wapo gari la majitaka. Walinitwanga ushuru bila exemption na kuambiwa hakuna lolote naweza kufanya baada ya kuwekwa siku 10 storage nikalazimika kushindwa kujiteteya. Hali hii ndio ukusanyaji kweli wa mapato anayoyaagiza Mh. rais? mbona uonevu mkubwa?

Jipu kama hili la kufuata maagizo atumbuwe nani? Maanake sikutoa hata chembe ya rushwa, kwa hiyo walifanya hivo kwa maagizo au kwa kunikomowa sababu siku onyesha kichozo cha kutowa rushwa.

Ila kwa hali kama hii, mara nyingine nakuakikishiya sintoweza kujiziwiya na nitatowa rushwa. Sababu wamepewa madaraka makubwa na sijatengenezewa mazingira rahisi ya kupeleka malalamiko yangu. Kukuza rushwa halitokuwa kosa langu bali la serekali.

Naomba sababu ya kunifanya nibaki na msimamo wangu wa kupinga rushwa kama hamna basi nitatowa, I'm sorry.

Ukitaka more information niambie.
 
Tra mko wapi na hii mimashine yenu wafanyabiashara kariakoo hasa wahindi ukienda kununua vitu kwa mfano ukitoa laki kununua vitu utaandikiwa risti ya elfu ishilini
Hili jambo hata mimi limenikuta.ila suluhisho la hawa watu aidha ni kuwakazia wakuandikie risit halali au kuwaweka hadharani kwa smartphone,wanakwepa sana kodi.
 
Jamani tuendelee kuibua kero mbalimbali tunazoziona kwenye maeneo mbalimbali ili ziweze kutatuliwa. Serikali ya awamu hii ni ya wananchi na tumeshaona haifumbii macho uovu wala maovu. Tuipe taarifa
 
Jipu ni ile hera ya DECI serikari ipo kimya mpaka leo. Watoe taarifa kama ilitumika kwa shughuri za kiseikari au wajanja wachache wamegawana kama ile ya EPA?
 
Jipu ni ile hera ya DECI serikari ipo kimya mpaka leo. Watoe taarifa kama ilitumika kwa shughuri za kiseikari au wajanja wachache wamegawana kama ile ya EPA?
Hiyo kama pesa ilitumika kwa mambo ya kiserikari ni sawa kabisa, hakuna kuwapa wana DECI hata senti moja, iwe fundisho kwa wajinga wanaoendekeza kupata pesa bila kufanya kazi.

Eti unapanda pesa halafu baada ya mwezi unavuna mara mbili, elimu ya wapi hii. Hawa ndio wanaokuwa tayari kuuza viungo vya albino
 
Hiyo kama pesa ilitumika kwa mambo ya kiserikari ni sawa kabisa, hakuna kuwapa wana DECI hata senti moja, iwe fundisho kwa wajinga wanaoendekeza kupata pesa bila kufanya kazi. Eti unapanda pesa halafu baada ya mwezi unavuna mara mbili, elimu ya wapi hii. Hawa ndio wanaokuwa tayari kuuza viungo vya albino
Ndo nnachokisema hata mimi mkuu. Tujue imeenda wapi ile hera. Habar ya walikuwa au hawakuwa wajinga waliopanda hizo mbegu lilishazungumzwa sana kipindi hicho. kwa sasa tujue tu imeenda wapi?

kama ipo kwenye account imefikia sh ngapi kwa sasa!!???
 
Tamasha la Nyamachoma Festival, walikwepa kodi. Kiingilio elfu 10 wanatoa risit magumashi ambazo hazikukatwa kodi.

Bei ya vinywaji na chakula ilikuwa juu maradufu na malipo yalifanyika bila risiti za TRA.

Bei ya bia mathalani ilikua Tsh 4,000/=
Nyama robo mguu wa mbuzi elft. 30 kwa elfu 40.
Na watu walikuwa ni wengi kwelikweli
 
Jipu langu ni Manispaa ya Temeke.

Walimu na askari waliosimamia mitihani ya Kidato cha Nne mwaka jana baadhi yao hawajalipwa. Pesa iliyotoka kwa bajeti haijulikani imekwenda wapi.
 
Hapa Dodoma kuna barabara mbovu kushinda zote hapa mjini, hii barabara ni ya kutoka keepleft cha Independence inapita pembezoni mwa soko kuu.

Hii barabara ina mashimo ni balaa sijui Halmashauri yetu imevaa miwani ya mbao , kwa kweli najiuliza mara nyingi sipati majibu.

Tunaomba barabara hii irekebishwe mapema sana maana ushuru wa soko unachukuliwa na barabara za kuzunguka soko hazirekebishwi.

Hivi huu Mkoa hauna viongozi?
 
Jipu langu ni TCRA: Local channels za bure zinapunguzwa kila Siku na makampuni ya ving'amuzi ila wako kimya tu..!
 
Rais Magufuli, angaza mfuko wa bima ya afya NHIF hasa kwenye miradi ya ujenzi. Kuna miradi ambayo haina tija inaanzishwa kwa sababu watu wanataka kula rushwa
 
JIPU! JIPU! JIPU!

Jamani mimi ni mlezi wa mwanafunzi nimejitolea kumsomesha, mwaka huu yupo kidato cha pili. Mkuu wa shule ya NAMDMKONGO iliyopo pwani Ni jipu. Kila wiki anataka 34,600/= ya chakula mimi amenichosha.

Halafu anafukuza wanafunzi, sasa mara ya pili.

Naomba waziri wa Elimu anisaidie, nimechoka. Kwani serikali haijapeleka pesa ya chakula hapo?

Naomba atumbuliwe haraka. Shule yenyewe walimu hawafundishi, mkuu wa shule ameshindwa kusimamia shule aondolewe bwana!
 
KWA NINI DSTV wao local channel zinalipiwa wakati wengine hawatulipishi? ili nalo jipu TCRA MPOOO?
 
Iliyokuwa SCOPO irejeshwe chini ya Msajili wa hazina ili kupanga maslahi ya watumishi wa umma. Kwa sasa ni vurugu tupu.

Kila bodi ya Shirika inapanga maslahi ya watumishi na nyingine ni kufuru tupu. Watu wanalipwa kwa dola au mishahara hadi tzs 36.5m na posho za vikao vya bodi tzs 1.5m kwa siku!
 
DAWA YAKE TAA ZIACHWE ZIFANYE KAZI YAKE KWANNI IMETIMIKA FEHDA NYINGI KUZIWEKA PALE......KAMA VP ZING'OENI TUJUE KIMOJA KWAMBA HAZINA MAANA KWETU.
Pale Tazara kuna taa upande wa kutokea mjini kurudi uwanja wa ndege uwa inawaka in less than a minute! Sijui ni mechanical error au nini?

Irekebishwe ili kuepusha msongamano wa magari.
 
1. National Housing Corporation (NHC): Bei za pango hazimlengi mtanzania wa hali ya chini. Nyumba zao wanazouza hazinunuliki na mtumishi wa kawaida wa umma.

2. Rushwa iliyokithiri katika Jeshi la Polisi. Watumbuliwe nao.

3. Uendelezaji wa Kigamboni nia ni kuumiza wananchi maskini.
 
Duka linalouza nyaraka za serikali maeneo ya posta mpya wanauza magazeti, sheria mbalimbali nk bila kutoa risiti!

Huwa ninajiuliza, pesa hii ni ya umma au ya mifukoni mwa hawa watumishi?
 
Naiomba serikali iangazie ili jambo la kuziwekea nyumba alama za X ili kupisha upanunuzi wa barabara na miradi mbalimbali.

Tathmini inafanyika na stop orders za kutosha, kisha wananchi wanakaa miaka nenda rudi bila kulipwa fidia. Wananchi wanadumazwa kiuchumi kwasababu hii.

Mfano maeneo ya Kipunguni, mradi wa barabara Gongo la Mboto- Ulongoni A hadi Kinyerezi nk nk.
 
.....MRADI WA BARABARA UMEFIKA LAKINI NGUZO BADO KUHAMISHWA!!!!!!.......MFANO KUANZIA MOMBASA KWENDA MOSHI BAR....
 
Back
Top Bottom