Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Uliomba risiti hukupewa??

Ni haki ya msingi kupewa risiti! Sio nibembeleze! Hii ni tendency mbovu ya mtumishi kufundishwa kazi! Mteja akisha lipia let's say 30,000/-(Tshs) anapaswa apewe receipt. Ndivyo sheria inavyo sema, sio adai!

Hii ya kuwahimiza watanzania wadai risiti halali siyo! Watoa huduma wanapaswa kutimiza jukumu lao kwa mujibu wa matakwa ya sheria! Ningemwomba angenipa najua! Ila imekuwa kawaida yao kutokutoa stakabadhi za malipo.

Watanzania tusiendelee kuishi kimazoea!
 
Kuna hili la Kampuni ya Lake Oil kutumia viwanja na majengo ya TAZARA kuwa Bandari ya nchi kavu, nadhani kama ni kweli sio suala la kufumbia macho.

Haiwezekani mali ya wananchi itumike ndivyo sivyo huku watumishi wachache wasio waaminifu wakijinufaisha na ufisadi huo.
 
Jipu lingine liko chuo cha technology DIT. Kuna gorofa la teaching complex linahengwa tangu mwaka 2006 mpaka sasa halijaisha na wanafunzi wanasonea juu ya machine badala ya kuwa na madarasani.

Ufanyike ukaguzi wa haraka saana watu wanakula PESA pale.

Lingine ni kwenye maswala ya mabweni, wanatoza pesa ambazo hazijulikani zinakwenda wapi.

Nyingine ni idara ya matengenezo, hakuna matengenezo ila wanakaa vikao vya kulipana posho kila mwezi.
 
Kero yangu ni kwamba, Shirika la umeme Tanzania (TANESCO). Nashindwa kuwaelewa kabisa, au ndo kwa vile wao wameishakuwa na jina ni kawinda yao na hawataki hatakubadilika.

Mimi ni mteja wao ambao natumia umeme chini ya UNIT 75 mbazo kiutaratibu mteja wa kundi hilo anapaswa atolewe gharama za huduma (SERVICE CHARGE).

Nanimekuwa mteja wao kwa muda wa miaka 3 sass. Nimeomba kutolewa gharama hizo bila mafanikio. Nilipeleka barua ya kwanza baada ya mwaka mmoja, nilipofika mapokezi wakaniambia ombi lako litashughulukiwa ndani ya miezi 3 kwa kuwa kuna foleni ya watu Walioomba kutolewa gharama hizo, pia. Wakaniambia sharti kwa kipindi cha miezi hiyo niwe nanunulia umeme kwenye ofisi zao.

Cha ajabu ikapita kipindi walichoniambia bila kutolewa. Nikaenda kukumbushia wakaniambia barua yangu haionekani, ikabidi niandike nyingine; kikapita kipindi walicho nihaidi nacho bila mafanikio. Ikalazimika niandike nyingine hali ikawa vile vile.

Nikawafuata ofisini wakanimbia watuniwengi, ninachojiuliza ni watu gani waliopo kwenye foleni wasio isha hao hasa nikifananisha na idadi ya mkoa wangu wa RUVUMA kwa uwingi gani tulionao? Au ndo wao ndo wanajifanya miungu watu?

Haitoshi mwezi uliopita waziri mwenye dhamana ametangaza kwa wale wote wanaotumia umeme chini ya 75 waondolewe gharama hizo mara moja na bila masharti lakini huku wanaweka tena kulikoni?

Nani mwenye kutoa mwongozo kati yavionvozi wa TANESCO na Waziri mwenye dhamana? Kwa kweli inaniumiza Sana! JF naomba mnisaidie kufikisha hili kwa wahusika. TANESCO bado ni jipu ambalo limetapakaa mwili mzima.
 
Naiomba serikali iangazie ili jambo la kuziwekea nyumba alama za X ili kupisha upanunuzi wa barabara na miradi mbalimbali.

Tathmini inafanyika na stop orders za kutosha, kisha wananchi wanakaa miaka nenda rudi bila kulipwa fidia. Wananchi wanadumazwa kiuchumi kwasababu hii.

Mfano maeneo ya Kipunguni, mradi wa barabara Gongo la Mboto- Ulongoni A hadi Kinyerezi nk nk.
Na kama ni bomoabomoa nadhani baa maarufu ya Rose Garden iko eneo la road reserve ama service road. Basi tingatinga litakapopita Mikocheni lisiishie mkwajuni tu na mwenge livunjevunje kabisa sehemu ya bar iliyozidi.

Mji unakuwa mchafu sababu ya biashara ndogondogo zisizokuwa na mipaka mara samaki,maji ya kunywa ilihali vituo vya basi vinanuka mikojo na joto hili vituo havieleweki.

Stendi za bodaboda na mabus zitengwe maalum. Angalia stendi ya kwenda Goba, au Ukonga Mombasa, Tandika nafasi hazieleweki.
 
UDA, UDA, UDA!!! Hili ni jipu.

Ni kwanini anahodhi route ya kwenda ferry peke yake na hana mabasi ya kutoka pande zote za jiji?

Watu tulikuwa tunatoka makwetu mpaka ferry kwa bei ya shilingi 500 tu lakini kwa sasa unashushwa Mnazi mmoja, kisa eti route ya Ferry ni ya UDA peke yake. Tunalazimika kulipa mara mbili au kutembea kwa miguu au kukodi usafiri wa taxi maana boda boda mjini wanapigwa marufuku.

Naomba hilo jipu litumbuliwe. Biashara ni huria, kama anataka ushindani ashindane na wenzake kwa kuweka magari mazuri na si kupendelewa.
 
DEREVA TAXI NA DEREVA BODA BODA WOTE WAPEWE PLATE NAMBA NYEUPE.

Dereva TAXI kwa sasa hawalipi kodi manake taxi zao hufanana za matumizi ya kawaida (private use).

Pia wote (Dereva TAXI na dereva Boda boda) vyombo vyao viwe na namaba ya utambulisho mf. KAR 234. Ikimaanisha ni Bodaboda ya Kariakoo no 234. Na wawe na uniform zenye no hiyo, na Rangi ya no hizo iwe ni ya NJANO KUBWA (ILIO KOLEA). AU YALE makava/jacket za POLISI TRAFFIC (Njano, nyeupe na nyeusi).

Lengo la hili ni kupunguza uharifu na upotevu wa mizigo za abiria.
 
Jipu uchungu nimeliona hospitali ya Mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa....

Mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini
Eti watu wanatoka nyumbani bila kunywa chai wakifika ofisini ndio wanatoka kabla ya kuanza kazi kwenda kunywa chai.

Imezoeleka kama ndio utaratibu wakati ni wizi wa muda wa kazi. Baada ya hapo wanasogoa na kujigeuzageuza kuuza sura ndio hiyo saa tano wanaanza kazi tena kwa spidi ndogo na maringo. Hizo ni tabia za kijipu.
 
Majibu yapo hila me nashauri tu swala la bomoa bomoa hili astishe
Hapana bomoabomoa iendelee tena kwa kasi. Tunataka miji yetu iwe katika mpango mzuri na waliojengamabondeni wote wabomolewe makazi yao.

Wahusika na vurugu ya mpabngo mji wasakwe hata kama wamestaafu watumbuliwe jipu.

Wanaobomolewa wawekwe kwenye makambi ya muda na wale watakaopenda kurudi mikoani wasaidiwe usafiri na kuhakikisha wanaondoka mjini sio kujipajika tena sehemu nyingine isiokua rasmi.
 
Jipu lingine lipo TANESCO jamani yaani ulipoti tatizo ,unapigwa kalenda mpaka wiki inaisha.

Hii ni shida sana, Mheshimiwa mwenye dhamani ya utumbuaji naomba watumbue hawa TANESCO Songea maana imekuwa kero kubwa sasa.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.

Asanteni na hongera ziwaendee Wamiliki na MODs kwa hatua hii!.

Jamani acheni Siasa!. Tanzania ni yetu sote tukipiga hatua moja mbele ni kwa faida yetu sote sasa na hata kesho ya watoto na wajukuu zetu!
 
Nadhani huu ni mwanzo mzuri!

Naamini MDS kadri tunavyokwenda watakuja na mfumo rahisi na friendly ya kupokea , kusambaza na kurudisha mrejesho wa member wa JF!

Ila kama itawapendeza kuna haja mwanzo kabisa wa hii thread kwa kuanzia kuna haja ya kuweka upadate ya list ya majipu yaliyoletwa na wanaJF kwenye mfumo wa 1----100(list) na comment kama imewasilishwa taasisi fulani na nk.

Jipu langu!

Makele ya Baa na kumbi ya muziki polisi wawezeshwe vyombo vya kupimia Viwango vya Sauti !
NEMC ichukue dhamana ya kununua vyombo hivyo! Hatuwezi kuwana sheria lakini utekelezaji ukashindikana kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi.

Anti-noise pollution law to take effect - National | The Citizen
The Citizen
Dec 22, 2014 - ... law regulations that seek to control noise and vibration levels whose ... National Environment Council (NEMC) and the Tanzania Bureau of ...

cc. Invisible ,Mhariri Active
 
Polisi dar na operation zao...

Kwa mfano, wanapita kwenye vijiwe za wauza bangi kukusanya ushuru kwa wauza bangi. wanavijua vijiwe vyote. Siku wakiamua i.e. karibu na siku kuu wanapita kukamata na kuwalundika wavutaji wote sero..kutoka sero ni kwa hela.

Jana Jumamosi maeneo ya Makonde wamekusanya vijana wowote wapo wengi sio wavuta bangi. Hawakuachii hadi utoe hela. Kijiwe kimoja cha wavuta bangi miaka zaidi ya kumi kiko uwanja usiojengwa miaka twende rudi usoni na kwangu Mbezi beach, Goig. Wamekuja wamemzoa mwanangu kwenye frame yake na wapangaji zangu kukoswa koswa eti bangi.

Hawasikii reason hata utambike ila hela tu ndio wanasikia.

Kijiwe hawakisafishi kwa sababu ni mtaji wao. Binafsi mara mbili nimefika Makonde kituoni juu ya kijiwe jirani cha wauza na wavuta bangi hawakisafishi.

Wacha tu, inaudhi kweli.

Huu naona sasa ndio utawala bora nchini petu.
 
Serikali ya mtaa kata ya Azimio Kusini, Tandika manispaa ya Temeke hili naona tuliite tambazi.

Huku mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwa kushirikiana na mtendaji wake na baadhi ya wajumbe wamekuwa wakifisadi pesa zinazotolewa kwa ajili ya familia zisizojiweza kupitia miradi ya TASAF,USAID nk.

Mwenyekiti amekuwa akiorodhesha majina ya watu wasiohusika(hususan wanawake) na kuwasainisha huku akiwapa elfu 20-30 kwa kusaini na fungu linalosalia hugawana na wajanja wenzie.

Na kwa kuongezea huyu m/kiti hajawahi kuitisha mkutano wa mapato wa katta hii kwa zaidi ya miaka 3.

Mkuu wa wilaya na TAMISEMI fuatilieni maana huku watu wengi uelewa wa masuala haya ni mdogo tatizo elimu na hapo ndipo jamaa anatumia udhaifu huo kujineemesha.
 
Tra ni tatizo kubwa kwa wajasiriamali wazawa/ wafanyabiashara SME’s

Wakuu wote wa janvi hili salamu zenu, Napenda kuwapa Hongera Hongera Sana kwa wafanyabiashara wote na hasa hao viongozi wao kwa kuweza kuonyesha dhahiri hisia zao kwa TRA jambo ambalo hapo nyuma lilikuwa halijawahi tokea kwa uwelewa wangu, hii ni dalili za kukuwa kwa fikra na uwelewa wa wafanyabiashara wetu sasa pia ni kukua kwa uhuru.

Cha kushangaza badala TRA kulipokea swala hili kwa nia njema kama njia iliobora ya kuwarahisishia upatikanaji wa kodi kwani sasa wamepata wadau wa kushilikiana nao bega kwa bega ilikutatua changamoto zilizopo na kufikia malengo ya kila mdau, hao wanaendelea kama walivyozoea kutisha wafanyabiashara na mabango /matangazo yaliojaa vitisho vingi nawakumbusha hakuna mwenye nguvu Zaidi ya mwananchi mwenyewe akiamua.

Wakati watu wakilalamika kuhusu mfumo wa kulipa kodi unavyowasumbua, unavyowaumiza, ulivyowadharirisha, unavyowanyanyasa, usivyojali maslahi yao na wakati mwingine tatizo sio ukubwa wa kodi wafanyabiashara wengi tu wakiulizwa wanadai kwa kuwa TRA hatuna uhakika na kodi zao zisizoisha inatubidi kukataa au kupinga kila wanachokudai kwa sababu hujui kesho watakuja na lipi tena la sivyo kama kungekuwa na Imani tuko tayari kulipa hata mara mbili Zaidi.

TRA kama walivyo zoea ni kutoa sheria kila kukicha (bila kuwashilikisha wadau husika) kwa wafanyabiashara zikiambatana na VITISHO vingi na watu kulipiswa faini kwa nguvu na RUSHWA kwa wingi sana wakifilisi wajasiriamali wazawa hatimaye wanatangaza wazi kuwa wamavuka malengo kwa Faini na Rushwa bila kujali ni wangapi wamefilisiwa na kufungunga biashara.

WAKATI UMEWADIA:

Nadhani wakati umewadia wafanyabiashara wa Tanzania wapate watetezi katika vyombo vyote husika Bungeni, Selikarini, wakiwa wadau wakuu wa maendeleo yeyote ya kiuchumi katika nchi yeyote (ETI NDIO INJINI YA MAENDELEO KIUCHUMI) inabidi wapewe fursa ya kutosha katika kuzitunga hizo sharia husika BUNGENI pia vilevile wahusishwe katika utekerezaji wake bila kuleta madhara kwa wadau wake.

TRA WABADILI FIKRA ZAO:

Kila mfanyabiashara kwa TRA anaonekana kama mwizi wa kodi (hata mwizi wa kuku ananafuu sana), afisa wa TRA anapokuja dukani kwako chochote atakachoona hakikukaa vizuri basi kwake yeye lengo ni kuiba kodi tu kinachofuata ni vitu viwili VITISHO VINGI SANA, FAINI ZA MAMILION, NA RUSHWA NYINGI SANA, ikibidi ukipona kiafya yaani wakikuacha unapumua basi biashara lazima utafunga na ukifuatilia chanzo cha tatizo ni kutokuelewa tu au ukosefu wa elimu ya kodi, TRA hakuna kitu onyo usirudie, wala wakuelimishe then waje wathibitishe kama kweli ulikuwa na nia mbaya..

MAPUNGUFU YA MFUMO WA TRA NI GHARAMA ZA MLIPA KODI:
Kwa wale wanaotumia mashine za VAT, ikitokea wakati wa kutoa risiti hakuna mtandao kwa nia nzuri tu ili ulipe kodi ukaandika risiti ya kitabu wanachokijua utapigwa utaambiwa faini sh 8,000,000 hapo utakuwa mhanga wa kuwabembeleza hatimaye faini ya serikali sh 3 mln na yao 3 mln vinginevyo unaambiwa kama hakuna mtandao uandike barua uipeleke ofisi ya TRA wakugongee mhuri ndio umpe mteja wako aondoke nayo kwa maana km ofisi ya TRA iko km 4 kila utakapouza kilo chupi ya motto unakenda TRA na barua mteja akisubiri, na pia huwezi jua ni wakati gani mtandao utakuwepo au la..

Kwa wale VAT wakati wa return kuto taarifa za biashara kila mwezi, zamani ilikuwa unajaza form kwa mkono unawapelekea haikuwa na usumbufu, wakabadili kutumia email wakalazimisha wafanyabiashara kununua makompyuta ili wawapelekee wanaweka program yao kwa siri sana na ndio unayoitumia kutuma email, kwanza HAKUNA MAFUNZO yeyote watu wamehangaika na vitisho vya faini ukichelewa watu hawakulala usiku wakituma haziendi network yao dhaifu,, hakuna feedback kuhakikisha kuwa imepokelewa au la pia baada ya muda miezi kadhaa wanakuja wakidadi hawana report zako na malimbikizo kibao ya penalty, faini kibao, sharia za kupandana zote zikitishia kufa biashara yako pia hata wewe mwenyewe Hatimaye rushwa na faini.

KUTOELEWA , UJINGA WAKO NDIO RUSHWA NA KODI TRA(auditing):

Pana wakati wanajua kabisa wafanyabiashara swala Fulani hawalielewi wao wana kaa kimya inapita muda wa kutosha kama miaka kama 3 hivi, then wana zua kitu wanaita ukaguzi (AUDITING)
Lengo kuu hapa kukusanya pesa wafikie malengo yao binafsi na TRA pia, hakuna kukuelimisha hapa, wala kukuonya hapa fikiria shughuli za biashara za miaka 3, hata kama ulipitiwa jibu lake ni rushwa, riba na faini iliyo na malimbikizo.

Mfano, ktk kuandika risiti bahati mbaya kibinadamu badala ya kuandika 200,000= ukaandika 20,000= yaani sifuri moja tu haikuonekana. Wao kwa makusudi mazima kwa wakati huo hawatakujulisha chochote.

Pili, watakuja baada ya miaka mitatu hiyo tofauti ya 180,000 wakati wa AUDITING watakudai riba @ mwezi, Faini yake @ mwezi hadi leo utakuta hilo kosa moja wanakudai 60,000,000= wanaiita kodi halali ? ? ? una kuta mtaji wako ni milioni 40 wana piga kodi wao wenyewe na hawataki mtu mwingine wanakuambia UNADAIWA KODI YA SH 320 MILLION. BADO HUJAFA TU..

NI HERI UKUTANE NA JAMBAZI MSITUNI KULIKO TRA.. kumbuka wewe huna elimu ya kupingana nao pia wewe kazi yako ni biashara kumhudumia mteja wako utafanya kazi ya kuwahudumia TRA utakula wapi ? ?

Hatuna nia ya kutolipa kodi hata kdg lakini hii ya mauzo ya sh 180,000= kodi yake iwe sh 60,000,000= kweli hapa pana haki ?

AUDITING TRA MAANA YAKE KUUWA WAJASIRIAMALI WA KATI-SME's WAZAWA

Sababu kuu, ndio mtaji mkuu wa makusanyo ya TRA
1. TRA wanajua hawana uwezo wa kuajiri wahasibu/wataalam
2. Hawana uwelewa hasa haki zao kuhusu kodi.
3. Ni waoga TRA tokana na sheria zisizotekelezeka kuwakandamizia hapo ili wapate rushwa na kufifkia malengo yao na kufilisi kabisa biashara husika.
4. Hawana uwakilishi wowote kwenye vyombo vya Dola (bunge n.k)
5. Mfumo wa uchumi, sheria, logistics vs kodi hautekelezeki kabisa hasa VAT
na ndio mbinu kuu ya RUSHWA na Ujasriamali Kudumaa TZ
6. Hawana uwezo wa kuwaita TRA na kukaa nao meza moja (km walivyo wenzao wakubwa hasa wa asia)na kufanya RECONCILIATION ili km pana tatizo lolote lirekebishwe mapema, badala yake ni fursa kwa TRA makusanyo na rushwa

Inaendelea nikipata muda . . . .
 
Ofisi za serikali ya mtaa wa Bunju B.

Nililipa 30,000/- kwa ajili ya kuwanyanyua wajumbe wakaangalie kiwanja changu. Sikupewa risiti. Mwenyekiti alikuweko na ndiye aliyenipa wajumbe wawili kwenda nao. Usafiri nilikuwa nao. Hiyo pesa ilibaki ofisini.

Serikali za mitaa ni kero. Kwengine unalazimishwa uchangie furniture za ofisi, majengo etc.

Hizi pesa wanazochukua kiulaini zinaniuma kwa vile hela yangu naipata kwa jasho langu kihalali.
 
Tra ni tatizo kubwa kwa wajasiriamali wazawa/ wafanyabiashara SME’s

Wakuu wote wa janvi hili salamu zenu, Napenda kuwapa Hongera Hongera Sana kwa wafanyabiashara wote na hasa hao viongozi wao kwa kuweza kuonyesha dhahiri hisia zao kwa TRA jambo ambalo hapo nyuma lilikuwa halijawahi tokea kwa uwelewa wangu, hii ni dalili za kukuwa kwa fikra na uwelewa wa wafanyabiashara wetu sasa pia ni kukua kwa uhuru.
Cha kushangaza badala TRA kulipokea swala hili kwa nia njema kama njia iliobora ya kuwarahisishia upatikanaji wa kodi kwani sasa wamepata wadau wa kushilikiana nao bega kwa bega ilikutatua changamoto zilizopo na kufikia malengo ya kila mdau, hao wanaendelea kama walivyozoea kutisha wafanyabiashara na mabango /matangazo yaliojaa vitisho vingi nawakumbusha hakuna mwenye nguvu Zaidi ya mwananchi mwenyewe akiamua.
Wakati watu wakilalamika kuhusu mfumo wa kulipa kodi unavyowasumbua, unavyowaumiza, ulivyowadharirisha, unavyowanyanyasa, usivyojali maslahi yao na wakati mwingine tatizo sio ukubwa wa kodi wafanyabiashara wengi tu wakiulizwa wanadai kwa kuwa TRA hatuna uhakika na kodi zao zisizoisha inatubidi kukataa au kupinga kila wanachokudai kwa sababu hujui kesho watakuja na lipi tena la sivyo kama kungekuwa na Imani tuko tayari kulipa hata mara mbili Zaidi.
TRA kama walivyo zoea ni kutoa sheria kila kukicha (bila kuwashilikisha wadau husika) kwa wafanyabiashara zikiambatana na VITISHO vingi na watu kulipiswa faini kwa nguvu na RUSHWA kwa wingi sana wakifilisi wajasiriamali wazawa hatimaye wanatangaza wazi kuwa wamavuka malengo kwa Faini na Rushwa bila kujali ni wangapi wamefilisiwa na kufungunga biashara.

WAKATI UMEWADIA:

Nadhani wakati umewadia wafanyabiashara wa Tanzania wapate watetezi katika vyombo vyote husika Bungeni, Selikarini, wakiwa wadau wakuu wa maendeleo yeyote ya kiuchumi katika nchi yeyote (ETI NDIO INJINI YA MAENDELEO KIUCHUMI) inabidi wapewe fursa ya kutosha katika kuzitunga hizo sharia husika BUNGENI pia vilevile wahusishwe katika utekerezaji wake bila kuleta madhara kwa wadau wake.

TRA WABADILI FIKRA ZAO:

Kila mfanyabiashara kwa TRA anaonekana kama mwizi wa kodi (hata mwizi wa kuku ananafuu sana), afisa wa TRA anapokuja dukani kwako chochote atakachoona hakikukaa vizuri basi kwake yeye lengo ni kuiba kodi tu kinachofuata ni vitu viwili VITISHO VINGI SANA, FAINI ZA MAMILION, NA RUSHWA NYINGI SANA, ikibidi ukipona kiafya yaani wakikuacha unapumua basi biashara lazima utafunga na ukifuatilia chanzo cha tatizo ni kutokuelewa tu au ukosefu wa elimu ya kodi, TRA hakuna kitu onyo usirudie, wala wakuelimishe then waje wathibitishe kama kweli ulikuwa na nia mbaya..

MAPUNGUFU YA MFUMO WA TRA NI GHARAMA ZA MLIPA KODI:
Kwa wale wanaotumia mashine za VAT, ikitokea wakati wa kutoa risiti hakuna mtandao kwa nia nzuri tu ili ulipe kodi ukaandika risiti ya kitabu wanachokijua utapigwa utaambiwa faini sh 8,000,000 hapo utakuwa mhanga wa kuwabembeleza hatimaye faini ya serikali sh 3 mln na yao 3 mln vinginevyo unaambiwa kama hakuna mtandao uandike barua uipeleke ofisi ya TRA wakugongee mhuri ndio umpe mteja wako aondoke nayo kwa maana km ofisi ya TRA iko km 4 kila utakapouza kilo chupi ya motto unakenda TRA na barua mteja akisubiri, na pia huwezi jua ni wakati gani mtandao utakuwepo au la..
Kwa wale VAT wakati wa return kuto taarifa za biashara kila mwezi, zamani ilikuwa unajaza form kwa mkono unawapelekea haikuwa na usumbufu, wakabadili kutumia email wakalazimisha wafanyabiashara kununua makompyuta ili wawapelekee wanaweka program yao kwa siri sana na ndio unayoitumia kutuma email, kwanza HAKUNA MAFUNZO yeyote watu wamehangaika na vitisho vya faini ukichelewa watu hawakulala usiku wakituma haziendi network yao dhaifu,, hakuna feedback kuhakikisha kuwa imepokelewa au la pia baada ya muda miezi kadhaa wanakuja wakidadi hawana report zako na malimbikizo kibao ya penalty, faini kibao, sharia za kupandana zote zikitishia kufa biashara yako pia hata wewe mwenyewe Hatimaye rushwa na faini.

KUTOELEWA , UJINGA WAKO NDIO RUSHWA NA KODI TRA(auditing):
Pana wakati wanajua kabisa wafanyabiashara swala Fulani hawalielewi wao wana kaa kimya inapita muda wa kutosha kama miaka kama 3 hivi, then wana zua kitu wanaita ukaguzi (AUDITING)
Lengo kuu hapa kukusanya pesa wafikie malengo yao binafsi na TRA pia, hakuna kukuelimisha hapa, wala kukuonya hapa fikiria shughuli za biashara za miaka 3, hata kama ulipitiwa jibu lake ni rushwa, riba na faini iliyo na malimbikizo,
mfano ktk kuandika risiti bahati mbaya kibinadamu badala ya kuandika 200,000= ukaandika 20,000= yaani sifuri moja tu haikuonekana,
Wao kwa makusudi mazima kwa wakati huo hawatakujulisha chochote,
Pili, watakuja baada ya miaka mitatu hiyo tofauti ya 180,000 wakati wa AUDITING watakudai riba @ mwezi, Faini yake @ mwezi hadi leo utakuta hilo kosa moja wanakudai 60,000,000= wanaiita kodi halali ? ? ? una kuta mtaji wako ni milioni 40 wana piga kodi wao wenyewe na hawataki mtu mwingine wanakuambia UNADAIWA KODI YA SH 320 MILLION. BADO HUJAFA TU.. NI HERI UKUTANE NA JAMBAZI MSITUNI KULIKO TRA.. kumbuka wewe huna elimu ya kupingana nao pia wewe kazi yako ni biashara kumhudumia mteja wako utafanya kazi ya kuwahudumia TRA utakula wapi ? ?

Hatuna nia ya kutolipa kodi hata kdg lakini hii ya mauzo ya sh 180,000= kodi yake iwe sh 60,000,000= kweli hapa pana haki ?

AUDITING TRA MAANA YAKE KUUWA WAJASIRIAMALI WA KATI-SME's WAZAWA

Sababu kuu, ndio mtaji mkuu wa makusanyo ya TRA
1. TRA wanajua hawana uwezo wa kuajiri wahasibu/wataalam
2. Hawana uwelewa hasa haki zao kuhusu kodi.
3. Ni waoga TRA tokana na sheria zisizotekelezeka kuwakandamizia hapo ili wapate rushwa na kufifkia malengo yao na kufilisi kabisa biashara husika.
4. Hawana uwakilishi wowote kwenye vyombo vya Dola (bunge n.k)
5. Mfumo wa uchumi, sheria, logistics vs kodi hautekelezeki kabisa hasa VAT
na ndio mbinu kuu ya RUSHWA na Ujasriamali Kudumaa TZ
6. Hawana uwezo wa kuwaita TRA na kukaa nao meza moja (km walivyo wenzao wakubwa hasa wa asia)na kufanya RECONCILIATION ili km pana tatizo lolote lirekebishwe mapema, badala yake ni fursa kwa TRA makusanyo na rushwa

Inaendelea nikipata muda . . . .
VAT ni kero kubwa. Kuna wafanyabiashara wakubwa hawana Efd mashine hawa wanatuumiza tunaonunua vifaa kutoka kwao. Malipo yetu ya vat yanapanda.
 
Back
Top Bottom