Mimi ninadhani madini na wanyama ni rasilimali nyeti sana za nchi na ni mali ya watanzania wote.
Ninatamani kusikia kuhusu mikataba ya madini na mbugani sijui uwindaji ijadiliwe bungeni na wananchi tusikie na kujua madini yanayochimbwa ni kiasi gani yana thamani gani na nchi inapata kiasi gani kutokana na kiasi gani cha madini.
Na mikataba ya uwindaji wa wanyama kama ipo nayo iwekwe wazi bungeni na tutajiwe majina ya wamiliki wa kampuni za uwindaji si majina ya kampuni, bali majina ya watu!
Natamani kusikia viongozi wa juu wa nchi yetu wakilizungumzia hilila madini na ujangili.
Ninaamini nchi ikisimamia hizo sekta ( utalii na madini) tu vizuri sana na kuziba mianya ya wajanja wanaotafuna hizo sekta kweli hatuhitaji msaada wa kutoka nje.
Natamani kuiona Tanzania ikiwa nchi tajiri, na hilo linawezekana ufisadi ukizimwa kila ofisi nchi nzima, sasa nina miaka 40 wimbo ni mmoja tu Tanzania ni nchi masikini!
Mimi binafsi nimechoka mno kusikia wimbo huu!