Diva Beyonce
JF-Expert Member
- Mar 6, 2014
- 12,913
- 11,271
Wewe una uelewa mdogo kama Lowassa yumo mbona hatujasikia akikamatwa na yupo nje ya ccm? wewe unafikiri Lowassa angekuwa amefisadi kama alivyofanya Kikwete wangekuwa wamemwacha hadi leo? na kama amefisadi nchi basi wahusika wakubwa wapo ccm ndio maana wanashindwa kumkamata maana mambo yote yatakuwa hadharaniLowasa na genge lake chini ya rostam azizi umelisahau
Magu na CCM, CCM na Magu. CCM ni nguo ya Magufuli.Kama ana nia ya dhati ya kumaliza ufisadi nchini afute Chama Cha Mapinduzi!
aguse anate?Kama ana nia ya dhati ya kumaliza ufisadi nchini afute Chama Cha Mapinduzi!
Chama cha mapinduzi hakina shida hata kidogo!Kama ana nia ya dhati ya kumaliza ufisadi nchini afute Chama Cha Mapinduzi!
Chama cha mapinduzi hakina shida hata kidogo!
In fact hiki ni chama imara, bora na chenye misingi imara ya uongozi kuliko chama chochote nchini! Tazama mfumo wake wa uongozi!
Ila kuna shida ktk ccm kwa baadhi ya viongozi wake, kama Magufuli atachukua chama na kukifanya kama ilivyo serikali, then ccm itaimarika zaidi!
Tukiwagusa mafisadi nchi itayumbakupambana na ufisadi nchii hii ni ngumu sana. maana wahusika wakuu ni vigogo....
Sasa vyama vingine vifutwe kwa sababu zipi?Kwa muktadha huo unaonaje ukamshauri msajili wa vyama vya siasa afute vyama vingine ibaki tu CCM?
Afute? Acha UTANI. Mpango uliopo ni kuwa Mwenyekiti Mapema iwezekanavyo...Kama ana nia ya dhati ya kumaliza ufisadi nchini afute Chama Cha Mapinduzi!
Mimi ninadhani madini na wanyama ni rasilimali nyeti sana za nchi na ni mali ya watanzania wote.
Ninatamani kusikia kuhusu mikataba ya madini na mbugani sijui uwindaji ijadiliwe bungeni na wananchi tusikie na kujua madini yanayochimbwa ni kiasi gani yana thamani gani na nchi inapata kiasi gani kutokana na kiasi gani cha madini.
Na mikataba ya uwindaji wa wanyama kama ipo nayo iwekwe wazi bungeni na tutajiwe majina ya wamiliki wa kampuni za uwindaji si majina ya kampuni, bali majina ya watu!
Natamani kusikia viongozi wa juu wa nchi yetu wakilizungumzia hilila madini na ujangili.
Ninaamini nchi ikisimamia hizo sekta ( utalii na madini) tu vizuri sana na kuziba mianya ya wajanja wanaotafuna hizo sekta kweli hatuhitaji msaada wa kutoka nje.
Natamani kuiona Tanzania ikiwa nchi tajiri, na hilo linawezekana ufisadi ukizimwa kila ofisi nchi nzima, sasa nina miaka 40 wimbo ni mmoja tu Tanzania ni nchi masikini!
Mimi binafsi nimechoka mno kusikia wimbo huu!
Ninaunga mkono hoja.Wafanyakazi wa kitengo cha mipango miji Halmashauri ya Kinondoni wanatakiwa watumbiliwe haraka iwezekanavyo.
Hawa wafanyakazi hasa cartographers ambao wengi wao ni wakina mama wa makamo wakiongozwa na mama mmoja wa kipare wanakalia kazi walizoambiwa warekebishe na wizara ili kuwawezesha wananchi wapewe hati zao.
Hati nyingi hazijakamilika kule wizarani kwasasababu "VIZIDUO" vilivyoambatanishwa toka wizarani havijafanyiwa kazi na wahusika wanaomba rushwa mpaka ya shs.700,000 mpaka shs 800,000 ili wawakamilishie wahusika vizuduo vyao na kuvipeleka wizarani!!
Kuna umuhimu wa kuwamulika vizuri hawa cartographers ambao ni watu wazima na heshima zao lakini wanawasumbua wananchi kwa kutotimiza wajibu wao na kuomba rushwa.
Mimi ni muhanga wa tatizo hili na natarajia kwenda kumuona mkurugenzi wa halmashauri nione nae atalishuhulikia vipi kwani ninafuatilia hati yangu toka mwaka 2010 NA SIKO TAYARI KUHONGA!!!
Hawa cartographers hawajui kuwa kwa ufisadi wao huo wanaikosesha serikali mapato kutokana na land rent ambayo hailipwi kwani wananchi hawajapewa hati zao!!