Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Mwaka wa kutoa hesabu huu,vipi bado inatafunwa
 
Mkuu
Kuna hii ufisadi mkubwa unafanywa na huyu wakili msomi aliyekula viapo vyote vya uaminifu.
Na inaelekea ana mtandao mkubwa maana madai yote dhidi yake tena ya jinai iliyo wazi yanaishia polisi oysterbay.
Msomi anaitwa Victor P... anatoa hati feki...tena za serikali kama vile hati za wageni kufanya kazi nchini, hati za biashara....leseni na hata huko ardhi ana mtandao..
Ajabu hapo oysterbay tu ana RB kadhaa lkn zimeishia hapo !
Huyu anachafua sifa ya nchi yetu nje, na sijui ni vipi ktk awamu hii bado anadunda tu na kula bata Dubai..
Kuwasaidia nendeni kampuni ya REA wapo Masaki wanatoka nchi moja ya kiafrika.. hawa walipigwa hati za kufanya kazi nchini feki..
 
Wizara ya Elimu baada ya kuona changamoto zinazowapata Wanafunzi kutokana na kuongeza saa 2 za masomo kila siku kwa Shule za Msingi na Sekondari, ilibatilisha na kuagiza kurudi kwenye ratiba ya zamani( Vipindi 8) kwa siku, Shule za Msingi.
SWALI:- Ni kwa nini baadhi ya Halmashauri zimekaidi agizo la Waziri wa Elimu kwa kutotoa kibali cha kufuata ratiba ya awali( Vipindi 8) ?
Tukumbuke, wanafunzi wanatoka majumbani mwao kwenda shuleni asubuhi kukiwa giza na kurudi wanafika majumbani mwao kukiwa giza.
Je, Wakipata madhara yoyote humo njiani, sisi wazazi tumlaumu nani?
Haya yote yanatendeka, Afisa Elimu Kata yupo, Afisa Elimu Wilaya yupo, Mkurugenzi yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo na wateule wengine wapo.
Tunaomba Waziri wa Elimu atoke na atoe tamko kali, yawezekana hawajamwelewa.
 
Kata ya Manolo wilaya ya Lushoto imebaguliwa kwa kutowekewa umeme wa REA. Mfano vitongoji vya Manka, Kweeka, Mkunki, Nywelo, Madala, Lokome, Hekanda viko gizani mpaka Sasa. Vijiji vyote hivi viko katika kata moja ya Manolo. Umeme umefika makao makuu ya kata Hiyo kwa kuwa ni njiani mwa Barabara kuu ya TANROAODS ya kwenda Mtae. Kwa maneno mengine, Kama Barabara Hiyo ya Tanroads isingepitia hapo umeme wa REA katika kata Hiyo ya Manolo ingekuwa ndoto. Waziri wa Nishati upo?
 
Kipande Cha Barabara kati Zaghati na Manolo kutoka Lukozi kwenda Mtae, wilaya ya Lushoto, ni sugu kwa ubovu. Wala si kwa sababu ya mvua za mwaka 2019/2020. Miaka nenda rudi ni hivohivo. Inazibwazibwa tu, hapa na pale. Mvua ikinyesha hali ya barabara inarudi vilevile. Barabara hii ni muhimu sana kwa wakulima. Mazao yao hayapati bei nzuri kwa sababu ya Barabara hii. Hata wenye mabasi mazuri wanashindwa kupitisha mabasi yao kwenye Barabara hii. Hata hayo yanayopita kwenye Barabara hii kwenye kipande hiki yanapita kwa taabu sana. Miaka yote wakati wa mvua za masika mabasi yanashindwa kupita ktk njia hii kwa sababu ya ubovu wa kipande hichi cha barabara. Ubovu wa kipande hichi ni wa miaka mingi sana. Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads, Mfugale, upo?
 
Barabara kuu ya kata ya Manolo kutoka makao makuu ya kata, Manolo, kwenda Shume Nywelo ni mbovu miaka nenda rudi. Wakulima wa kata hii wana bidii sana ya kulima. Wanakatishwa tamaa ya maendeleo na barabara hii. Mazao yao ya nyanya na viazi mviringo na maharagwe yanauzwa kwa bei ndogo kwa sababu ya ubovu wa barabara hii. (Wilaya ya Lushoto). Mkurugenzi Mkuu, Tarura, upo?
 
Utakua ulianzia hospital nyingine pale ulienda Kwa vipimo tu nini?! Maana hawawapendi watu wa namna hii wanawafanyia kusud
 
Si mmeng'ang'ania shangazi. Anapenda misifa na kujikweza
 
Kero:Rushwa bado ipo maeeneo mengi mfano;Ajra utolewa kwa kujuana,Rushwa karibu taassi zote za umma na binafsi n.k
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Tatizo la wakulima na wafugaji bado ni kubwa.Hapa kiukweli kazi bado ni mbichi,na wateule wa Rais wameshindwa kabisa .Katika maeneo yenye wafugaji kwa wingi hasa Wamasai,wanafanya wanavyotaka.Na hii ni kwa sababu wafugaji hawa,hasa Wamasai kama nilivyosema,wamewaweka viongozi mifukoni,iwe Polisi au viongozi wa kisiasa.Imefika mahali sasa ni kama wao ndio wanaosimika viongozi wa kisiasa.Wanachanga hela wanampa mgombea ambaye wanaamini atasimamia maslahi yao ili akahonge wajumbe.Hili limekuwa jambo la kawaida sasa,hata katika msimu huu wa uchaguzi.No naomba serikali isiruhusu Wamasai ku-take hostage wakulima,this is a situation which has the potential of breaking peace.Sema sisi wakulima tunakua wavumilivu,ila naomba nitoe angalizo,uvumilivu una mwisho,na isichukuliwe as a sign of weakness.
 
Watanzania wamechoka kuendelea kusikiliza kauli chafu zitokazo kwa baadhi ya Wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Tunaonba serikali ifanye kazi yake. Hatuwezi kuvumilia lugha chafu zinazoashiria uvunjifu wa Amani.
 
Keri kubwa ni hivi vibali vya ujenzi. Mtu unaongeza chumba chako kimoja . Mtendaji anakuja anataka rushes ukikataa anakupiga faini na barua limetoka manispaa na muhuri ameligonga. Huu ni utapeli maeneo yetu hayajapimwa iweje ulazimishe kibali na hizi hela wanakuja mgambo wa kata na Mtendaji.

Ikiwezekana futa kabisa Mambo ya watendaji wa kata hawana Cha maana wanachofanya zaidi ya fitina na kukamua wananachi pesa. Misharahara yenyewe haipandi bado Kila mtu anageuka zakayo mtoza ushuru
 
Watanzania wamechoka kuendelea kusikiliza kauli chafu zitokazo kwa baadhi ya Wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Tunaonba serikali ifanye kazi yake. Hatuwezi kuvumilia lugha chafu zinazoashiria uvunjifu wa Amani.

Hizo lugha chafu ni zipi? Na ni mgombea gani kazitoa?
 
Watanzania wamechoka kuendelea kusikiliza kauli chafu zitokazo kwa baadhi ya Wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020. Tunaonba serikali ifanye kazi yake. Hatuwezi kuvumilia lugha chafu zinazoashiria uvunjifu wa Amani.
Na imekuwa kama utaratibu wa hawa wagombea kufanya haya mambo hakika ni mambo yasiyovumilika kwa namna moja au nyingine
 
Barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha SIMU 2000 ( mawasiliano) iwekwe lamiharaka ni kero kubwa.
2. Kitua chamabasi yaendyomikoani Ubungo kijengwe haraka.
Hiyo ya barabara, tayari mkuu lami imewekwa
 
Back
Top Bottom