Wizara ya Elimu baada ya kuona changamoto zinazowapata Wanafunzi kutokana na kuongeza saa 2 za masomo kila siku kwa Shule za Msingi na Sekondari, ilibatilisha na kuagiza kurudi kwenye ratiba ya zamani( Vipindi 8) kwa siku, Shule za Msingi.
SWALI:- Ni kwa nini baadhi ya Halmashauri zimekaidi agizo la Waziri wa Elimu kwa kutotoa kibali cha kufuata ratiba ya awali( Vipindi 8) ?
Tukumbuke, wanafunzi wanatoka majumbani mwao kwenda shuleni asubuhi kukiwa giza na kurudi wanafika majumbani mwao kukiwa giza.
Je, Wakipata madhara yoyote humo njiani, sisi wazazi tumlaumu nani?
Haya yote yanatendeka, Afisa Elimu Kata yupo, Afisa Elimu Wilaya yupo, Mkurugenzi yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo na wateule wengine wapo.
Tunaomba Waziri wa Elimu atoke na atoe tamko kali, yawezekana hawajamwelewa.