Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Nakumbuka kuna dogo alikuwa amepimwa siku moja nyuma ila anaonekana kuzidiwa sana...ila wao hawajali kama ni mda wa kazi wanapga stori za michepuko yao na siasa waliniuzi kweli aisee na umati wa watu upo nje unasubiri majibu na vipimo ila wao hawaanzi kazi ni stori mbele mx player apk

Regards, mx player pro
 
Kuna huyu Msomali anaitwa Hussen, nadhani ndio mmiliki wa Sanitas Hospital Mikocheni. Huyu jamaa alijenga ukuta wa Hospital chini ya Viwango. Ukuta umeanguka umeharibu Mali za Watu. Jamaa ana jehuri sana na amegoma halipi na hakuna wanaloweza kumfanya. Hili jengo la Hospital litakuja kuuwa watu wengi sana. Tunaomba mamlaka husika waingilie kati. Maana huyu msomali inasemekana hagusiki
 
Kero yangu ni pale jengo la RITA. Rafiki yangu umri miaka 80 alitaka nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwaka 1976 cha mwanawe. Alizungushwa zaidi ya miezi sita akipandisha ngazi ya gorofa la kifahari. Kila mara aliambiwa ETI rekodi haionekani rudi baada ya wiki mbili. Alifika ofisi ya malalamiko mara kadha lakini hakukuta mtu ofisini. Meza tu na kiti. Akaacha barua lakini hakuna majibu. Mwishowe jamaa mmoja msamaria alimwambia atamsaidia. Baada ya wiki moja alimletea cheti rasmi chenye mhuri na saini. Ofisi ya RITA makao makuu inanuka rushwa. Utakuta foleni kibao wazee wakisumbuka. TAKUKURU angalieni hapa
 
Kuna majipu bado yapo mengi mfano:

Utafiti mdogo niliofanya, umeonesha kuna shule za msingi zinaendesha tuisheni, mfano.

Shule ya msingi Tumaini na Kimanga zote shule hizi zimeunganishwa pamoja. Walimu wao wamekuwa wakiendesha tuisheni, pembeni kidogo ya shule hizo.

Walimu hao huendesha tuisheni, katika majengo ya shule ya sekondari ya wazazi iliyoko maeneo ya sokoni huko huko tabata kimanga

Chanzo mimi mwenyewe nimefanya utafiti.
Pamoja na wizara husika kupiga marufuku tuition, mimi sioni ubaya wa tuition. Tuition inawasaidia watoto wa wenye kipato cha chini na kati kuwapa watoto wao elimu ya kuwavusha. Kwa wenyenazo hupeleka watoto wao kwenye supper/premium schools ambapo ushindi kwa kawaida ni 100%. Kama wanapiga marifuku tuition shule za serkali je, watadhtu kupiga marufuku shule za binafsi, ambazo mtoto analipia tuitio kama sehemu ya karo?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Pale Dodoma nashukuru Waziri wa Maji, Ndugu Aweso amefanya jambo. Dodoma maji yalikua yashida sana na hakuna sababu za maana zinazotolewa hakuna. Ila tangu Mkurugenzi wa DUWASA ahamishwe maji yanatoka kila siku na hata usiku ambao ulikua maji yanakatika sasa yanatoka.

Ila kiukweli ni kua Mkurugenzi alikua akihujumiwa na watendaji wa chini. Hivyo ipo haja hata wao wakamulikwa maana Mkurugenzi pekee bila waliochini yake waliokua wakikwamisha haiwezekani. Na kuna kauli kua mtu huyo alikua mkali na wakaamua kumhujumu.
 
Mhuuu
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Jipu linaanzia kwake yeye mwenyewe kuvuruga uchaguzi 2020 na kufuta mfumo wa vyama vingi sasa on athari yake viboko vya mkoloni kwa wakosaji vimezaliwa bila kufuata utaratibu,sheria na mwongozo wa nchi.
 
Tufuchue vijiwe vya wavuta bangi ktk maeneo/mitaa yetu,
Madanguro, pombe haramu nk
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
kero yangu kupanda kwa bei za vitu mfano wiki mbilizilizo pita mafuta ya kula lita ili kua 3800 ila hadi leo mafita lita ni 5000 tuna elekea wapi
 
294e065f-36df-4a2c-9093-7889459d70fb.jpg

Jamani hapa unaweza kusema changamoto
Kila jumamosi saa 3 usiku mpaka saa 5 kipindi LIVE
YAN NI PAPO KWA PAPO
 
Najaribu kuandika kwa uchungu sana ni kweli tunahitaji maendeleo kwenye taifa letu ila kusubiria maendeleo hayo iwe kero na maisha magumu kwa wahusika kwa mfano mm na wenzangu ni kati ya wananchi ambao nyumba zetu zimepimwa ili kubomolewa kwa ajili ya utanuzi wa barabara ya sengerema nyehunge Nzela ni muda mrefu sasa tangu wameweka zile alama zao na nguzo za zege sasa mwaka wa 3 tunashindwa kuendeleza nyumba zetu tunashindwa kukarabati nyumba zetu kwa maana hiyo serekali ituambie lini wanafanya tasimini kwa ajili ya fidia au tuendelee na maisha yetu kama zamani tukarabati na kupangisha ili tupate chakula
 
Jipu au Nero ni tumeya ajira zinatolewa kwakujuana hasa hasa katika nafasi nzuri nzuri mfano BOT,Airport n.k wanawapa kazi wajomba zao na watoto wao hali kwamba hawana sifa.mfano wadumu ktk ndege wamenenepeana kama vifusi...
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama Watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.

Habari
kumekuwa na changamoto sana kwenye soko la ajira vijana wengi sana wapo mtaani na wanasiasa wamenukuliwa mala kadhaa waki waambia vijana wajiajiri. Laba ushauri wao ni bora lakini leo nita ongelea kwa upande mwingine
Kwa research fupi nilio fanya vijana wengi ambao wamemaliza masomo wamekuwa waki hangaika sana kwenya swala la ajira ambayo ni changamoto kubwa sana ambayo sioni serikali kama ina lifanyia ufumbuzi ukifatilia
Tasisi nyingi za serikali zikitaka kuajiri ni kupitia utumishi na kumekuwa na wingi wa vijana inapo tokea kazi kutangazwa ila taasisi nyingi zina intern sasa namba nizungumzie kuhusu hawa vijana wanao jitolea kwenye mashirika ya serikali
Vijana wengin wanao jitolea wanapata faida ya uzoefu kazini ila wamekuwa wanafanya kazi na kuwa faida sana kwenye baadhi ya taasisi ila kwann vijana hawa hawapati ajira za moja kwa moja wamekuwa wakipew ahadi kadha wa kadha kipi kinacho kwamisha vijana hawa kuajiliwa kuna taasisi ambazo zina intern wengi unakuta kitengo kizima asilimia kubwa kina endeshwa na vijana wanao jitolea je serikali bado aijaona manufaa ya vijana hao au ni kipi hasa kina kwamisha kuawapa ajira ya kudumu maana wamekuwa ni chachu ya mafanikio ya taasisi nyingi mfano TTCL,NSSF,WCF nk
Leo nimeona niongelee ilo kuna siku nitakuja kuongelea kazi wanazo fanyishwa vijana hawa
 
Back
Top Bottom