Tulitegemea huyu rais aje na utatuzi wa mitanziko mikubwa iliyojitokeza ktk awamu ya 5 baada ya mwendazake kutumia katiba yetu mbovu na sheria zetu mbaya kuliyumbisha taifa. Hivyo tulitarajia yafuatayo:-
1. Abatilishe na kubadilisha sheria zinazowaweka watuhumiwa rumande kimabavu, mfano;- mashekhe, Harbinder Seth, Papaa Msofe, n.k
2. Aibadilishe katiba ili isitoe mwanya kwa mtu mmoja (rais) ama chama tawala kuharibu uchaguzi kama ilivyokuwa 2020.
3. Atoe tamko hata la kulaani tu kama sheria haimpi uwezo wa kuwatumbua kabisa Covid-19 waliopo bungeni. Lkn anaonekana kudemka ngoma ya mtangulizi wake. Nimeona alipokuwa Mwanza amemtambua Nusrat kama mbunge anayewakilisha vijana mkoa wa Singida na akapewa nafasi ya kutoa neno.
4. Ajitenge na makada wa chadema walionunuliwa na akina Bashiru na Polepole. Lkn naona bado anawapa uwaziri, uDC, n.k. Nadhani atawatumia huko mbeleni kwa staili zile zile za awamu ya 5.
5. Afanye teuzi kwa misingi ya weledi. Lkn naona anaangalia zaidi wale wanaoweza kumsogeza mbele kisiasa.
Ndiyo maana anaondoa wasiyo wake na anapachika walio wakwake. Akina Bashiru, Polepole, Heri James pamoja na katibu wa UVCCM amewatoa na anatia chachandu yake.
My take.
Kwa jinsi tunavyoenda, huyu rais wetu hana nia ya kubadilisha katiba na sheria kandamizi.