Tony Blair amefuata nini Tanzania?

Tony Blair amefuata nini Tanzania?

nimefuatilia pia hizo Pandora leaks, hamna ufisadi wa Blair ulotajwa mle zaid ya kutokulipa cooperate tax which also is okey kwa mujibu wa sheria na namna manunuzi yalivofanyika…Soma tena mkuu labda tukushauri tena.
Ripoti inasema Blair na mkewe walikwepa kodi katika manunuzi hayo ya nyumba. Mkuu wewe ndo unatakiwa utulie uielewe vizuri ripoti. Ukwepaji ni ukwepaji hakuna ukwepaji ulio okey ndugu.
 
View attachment 1962432



Still sijaona ufisadi wa Blair may be quote paragraph wanayosema Blair ni fisadi
 
Ripoti inasema Blair na mkewe walikwepa kodi katika manunuzi hayo ya nyumba. Mkuu wewe ndo unatakiwa utulie uielewe vizuri ripoti. Ukwepaji ni ukwepaji hakuna ukwepaji ulio okey ndugu.
Je walivunja sheria?kama sheria zako zina loop holes huwez sema wamekosea.
 
Unalazimisha watu waanze kuweka kumbukumbu ya orodha ya 'chawa' wa 'Maza Mizinguo'. Inabidi nianze na wewe.
Habari ndo hiyo mama ameshakalia kiti mpaka 2030 nyie sumbukeni Tu na vilanga vyenu
 
Je walivunja sheria?kama sheria zako zina loop holes huwez sema wamekosea.
Bado wamekosea mkuu. Walipoona Kuna loop holes ndo wanapitia hapo ili kujustify makosa yao. Wao walitaka nyumba Ila wakagundua wakinunua nyumba pekee itawabidi kulipa kodi so ili kuikwepa hiyo kodi ikabidi wainunue kampuni nzima kitu ambacho ambacho kulikuwa kinawa-exempt kulipa kodi husika. Walifanya hivyo kwakuwa wao walikuwa na privelege hiyo tofauti na ordinary citizens. So what about the integrity kwa kiongozi kama Blair?

Sasa hilo kwa wenzetu ni kosa kubwa sana la kimaadili mana Britons wamewaka wanasema inakuwaje hiyo kwa mtu aliyeingia madarakani akijipambanua kupambana na ufisadi je kwa upendeleo huo na huo sio ufisadi?

Je sisi raia wa kawaida tungeweza kupata upendeleo huo kama yeye? So my friend huyu alitenda kosa. Kama hujanielewa hadi hapo sijui nikelezeje ndugu.
 
Tony Blair kwa wazalendo wana mapinduzi Tanzania, na Afrika ni bwanyenye wa kizungu muwakilishi wa ubeberu. Ni mtu laghai tu. Alipokuja kimyakimya kumuona mama Samia mara baada ya yeye kuapishwa kua rais na watanzania kutangaziwa eti ameteuliwa kua balozi wa corona wa tanzania tunaoelewa tukajua mama kapigwa. Mwenyewe huko nje akasema amepewa kazi kuisafisha tanzania jina baada ya jina la nchi eti kuchafuliwa na magufuli. Huko nje wakasema eti ujira kapewa bilioni 100 shilingi za kitanzania. Hakika wengi tukachukia.

Afrika ya kusini mjadala kwenye television ya taifa wakahoji kwa nini Tony Blair. Tony Blair ni mtu alipokua waziri mkuu wa uingereza aliunga mkono fitna na uongo wa George Bush aliyekua rais wa marekani kwamba Sadam Hussein wa Iraq alikua na silaha za maangamizi licha ya nchi zingine ulaya kuonesha mashaka. Kisha marekani ikiungwa mkono na Uingereza wakaivamia iraq na kuichakaza nchi ya kiarabu ya Iraq iliyokua na maendeleo mazuri na utajiri hadi kubakia jivu.

Zaidi ya hapo wakamuua Sadam Hussein kiongozi wa kimapinduzi kwa kumnyonga kwa kamba kwa kuhukumiwa na mahakama waliyoiunda wenyewe.

Safari za Tony nchini hakika zinaleta mashaka. Tungeomba rais wetu mama Samia kujihadhari na mabwanyeye wa vita maana hatimae umma wataweza kujua dili sisizofaa zinazoweza kufanyika hivyo kuharibu heshima ya viongozi wetu.
 
Wanamkaribisha shetani mlangoni, Ndugai pamoja na uchizi wake kuna Maneno ameyasema nadhani ni suala la wakati tu, eti Tony Blair ndio mshauri wa raisi!!!! Shame on you Tz Govt.
 
Mama yenu kashapigwa, subirini kichapo kingine
 
Back
Top Bottom