Top 3 GOAT Tanzania Rappers, Serikali itambue mchango wao ikibidi watunukiwe Phd

Top 3 GOAT Tanzania Rappers, Serikali itambue mchango wao ikibidi watunukiwe Phd

John Gregory

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2019
Posts
1,137
Reaction score
2,147
Kama BAKITA kweli taasisi zingine za Lugha na sanaa zinatambua na kuenzi kazi za sanaa, basi nadhani wasanii hawa walipaswa kuenziwa na ikibidi kuthaminiwa sana na serikali kwa kuwashirikisha katika matukio muhimu ya sanaa badala kuwashirikisha watumbuizaji peke yao ambao hawana mchango wowote zaidi ya burudani pekee.

Laiti kama serikali ingetambua michango na maudhui ya wasanii hawa wangeweza kuwatumia zaidi si tu kuburudisha, bali kuelimisha jamii.

Hii ni orodha ya wasanii watatu wenye uandishi bora ambao ukisikiliza utajiuliza ukubwa wa IQ zao mpaka kupata hizi tenzi.

3. Fid Q
Haina ubishi, kila mmoja anamfahamu, huyu ni mmoja kati ya nguli na miamba ya rap Tanzania, uandishi wake una ladha ya aina yake.Mfano

"kutaka kujua ukwel ni sawa na kumenya kitunguu kila ganda litakutoa chozi na kubaki macho juu juu"
images - 2024-10-12T131453.707.jpeg


2. SONGA
Linapokuja suala la uandishi wa mistari, inajulikana Songa, pamoja na sauti yake ya upole isiyo na mbwembwe lakini IQ yake ni kubwa sana, mfano

"Wazazi wanasema nimeshakua
Ina maana… vibaya na vyema nimeshajua
Jua linazama tazama inanyesha mvua
Nakesha kwa dua kumuombea anayekesha akivua"

images - 2024-10-12T132316.874.jpeg


1. DIZASTA VINA
Huyu katika ulimwengu wa Rap ana dunia yake! Hakuna msanii yoyote anayeweza au aliyewahi hata kumsogelea katika uandishi na ubora wa mistari yake.Ni mmoja kati ya rappers wenye IQ kubwa sana, Tukianza kumuelezea sifa zake nadhani hatutamaliza leo, Ila itoshe kusema ni hazina kubwa sana kwa taifa. Hata uhalisia wa maisha yake unajieleza, si mtu wa kujipendekeza, kushiriki siasa, kutafuta umaarufu, mapenzi n.k ni rapper anayeishi misingi ya rap kweli, kazi yake kushika kalamu na kuelimisha jamii. Ingekuwa Marekani tungeweza kumfananisha na Kendrick Lamar
Baadhi ya Lyrics zake:

"Eyo eyo kwa Insha na methali
Nawazika ka Ujamaa ulivyozikwa na Ubepari
Nishachoka na uongo so nafoka mpaka mtondogoo
Kwa world class Protocal, Internationally"

"Hizi tenzi ni pure, Niko real toka enzi nakua
Nili-rap kabla mapenzi sijajua
Kwenye game wanavyoenzi majuha
Wana track mbovu na wanafanya Media tours"

"Niko shega Bro
Genius ni Understatement half Man half God Paradox
Niite Vina just for lack of the better words
Literally, yet metaphorically undebatable"

"Sikutaka kutoka niliingia chaka
Nikatulia nikaisoma dunia utafikiria NASA
Nikawa fear factor, nikashika njia
Wabia wakanihofia kama wanavyoihofia Cancer"

images - 2024-10-12T134246.473.jpeg
 
List ya hovyo kabisa, unamuachaje SUGU, JAY na NAY .
Unaelewa maana ya Rappers? Sugu ni myu aliyeishi kwenye misingi ya Hiphop lakini kiuandishi na rap hajafikia ubora wa dizasta vina, huyo Jay mo na Nay wa mitego wana content za kawaida sana kwenye uandishi wao wala sio rappers tishio
 
Back
Top Bottom